Kwa kweli wachina wamenifurahisha jinsi wanavyohifadhi na kuuenzi utamaduni wao, pili jinsi wanavyozitumia fursa kuzalisha ajira tatu jinsi wao wenyewe walivyolijenga soko la ndani la bidhaa zao.
Hapa ni eneo la KAIFENG katika jimbo la Kusini mwa China ambako kuna eneo la makumbusho na utamaduni liitwalo MILLENIUM CITY PARK, yaani ni vitu vidogo vidogo lakini wamevigeuza kuwa katika thamani unaingia kwa pesa na utaona kuku wakipigana, sarakasi, kupanda farasi, michezo ya majini, majengo ya zamani nk.
Inavutia sana, nadhani kitu kama hiki hata sisi tuweza ni suala la kuamua. Na wateja wakuu ni wachina wenyewe, bahati mbaya tu wakati huu ni wa baridi kali kwa hiyo hakuna nyomi ya watu
Wadau tupo pamoja
Gerson Msigwa
Chunga sana na uchafuzi wao wa mazingira na ajira za wafungwa.
ReplyDeleteKweli tukiamua tunaweza.Tena huko China mbali sana embu tembelea kainchi kadogo ka jirani ketu Rwanda uone walivyofanya katika miaka 10 tu, maamuzi, discpline na maadili. Yaani ukivuka mpaka tu meter kadhaa unaona manadiriko makubwa.
ReplyDeleteAnyway change start with me and you...i am playing my part and this is my new year resolution
sisi kwetu huku afrika na hasa tanzania ukitakakuyaendereza mambo ya asili unaambiwa ni ushirikina tena nyinyi waandishi wa habari ndio vimbelembele mkienda kwa wenzetu mnajidai kusifia
ReplyDeletewachina ni wachafu sana hasa kimazingira na air polution ni mbaya sana kuna maeneo kama una ugonjwa wa pumu uwezi kuishi...sio nchi ya kuigwa kabisa...
ReplyDelete