Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi
wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa
zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi
kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo.
Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya
Ndugumbi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa
Barabara ya Mandela.
|
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na
kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.
|
Meya wa Manipaa, Yusuph Mwenda (kulia)
akimkabidhi shilingi 10,000 bibi kizee ambaye ni mkazi wa mtaa huo baada ya
kufurahishwa na hatua yake ya kujitolea kufanya usafi wa mazingira.
|
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda sambamba na viongozi wa Kata ya Ndugumbi wakikatiza mitaa mbalimbali ya
Kata hiyo wakiwa na mifagio na machepeo.
|
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na
kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.
|
Mifereji ilizibuliwa. |
Moja ya vitendea kazi vilivyotumika kwenye zoezi hilo. |
Watanzania tuache tabia ya Uchafu, na Uchafuzi wa mazingira. Tufanye na kuhimiza usafi kama desturi na siyo uwanja wa siasa
ReplyDeleteDuh! Kumbe meya Wetu ni shabiki wa mtaa wa Jangwani!!!
ReplyDeletekutokana kutowawajibisha watendaji wenu, MTAFAGIA SANA MWAKA HUU.
ReplyDeleteNi wakati wa kuwapa meno wajumbe wa nyumba kumi, na viongozi wa vitongoji,kata,wilaya nk.
wa TZ tulivyo, tunakuona chapakaaazi kweli kweli.
mdau znz
MEYA YUSUF MWENDA HONGERA KWA KUONYESHA MFANO.WEWE NI KIONGOZI WA KUIGWA,UNANIKUMBUSHA ENZI ZA JERRY RAWLINGS WA GHANA,ALIKUWA ANASAFISHA MIFEREJI HUKO GHANA.HILI NI SOMO KWA WAVAA SUTI HATA WAKIENDA VIJIJINI.NI WACHACHE KAMA NYIE.VIONGOZI WETU WENGI WAMEACHA UTAMADUNI HUU,HATA WAKIPANDA MTI WANATANDIKIWA ZULIA.TUTAFIKA?
ReplyDelete