Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda amefanya ziara ya uhamasishaji utunzaji wa usafi wa mazingira kwa wakazi
wa kata ya Ndugumbi, jijini leo (Jan 27). Pamoja na Mambo mengine ameahidi kuwa
zoezi hilo litakuwa ni endelevu ambapo kila mwisho wa wiki, wakazi wanaoishi
kwenye Kata mbalimbali za Manispaa hiyo watakuwa wakitekeleza zoezi hilo.
Pichani ni zoezi hilo lilivyotekelezwa leo kwa viongozi na wakazi wa Kata ya
Ndugumbi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda (Suruali ya njano) akisimamia uondoaji wa taka zilizokuwa zimetelekezwa pembezoni mwa
Barabara ya Mandela.
|
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda sambamba na viongozi na wakazi wa Kata ya Ndugumbi wakisafisha na
kuzibua mitaro katika Mtaa wa Ndugumbi.
|
Meya wa Manipaa, Yusuph Mwenda (kulia)
akimkabidhi shilingi 10,000 bibi kizee ambaye ni mkazi wa mtaa huo baada ya
kufurahishwa na hatua yake ya kujitolea kufanya usafi wa mazingira.
|
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph
Mwenda sambamba na viongozi wa Kata ya Ndugumbi wakikatiza mitaa mbalimbali ya
Kata hiyo wakiwa na mifagio na machepeo.
|
Mifereji ilizibuliwa. |
Mheshimiwa Meya, huyo anayezibua anahitaji Buti pia (vitendea kazini muhimu ili kufanikisha zoezi hilo kuwa endelevu)
ReplyDeleteMeya wetu wa Ilala yuko wapi? Mitaa ya Ilala Bungoni, Amana, Buguruni inanuka
ReplyDelete