Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yusuf Mwenda (mwenye shati la kitenge) hivi karibuni alifanya ziara katika Kata ya Makuburi,jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7. Barabara hiyo inajengwa na Manispaa hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 300. Pichani ni sehemu ya ziara hiyo akiwa na viongozi mbalimbali wa Serijkali za Mitaa, Madiwani na Wahandisi wakikagua sehemu mbalimbali za barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni na Kampuni ya ukandarasi ya Gwema Decorator Co. Limited

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akimuuliza kijana aliekuwa akiuza nyama ya kuchoma aliekuwepo kwenye Kata hiyo ya Makuburi wakati alipokuwa katika ziara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 hivi karibuni.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia) akizungumza na Mmoja wa Waendesha boda boda aliekuwepo kwenye moja ya vituo vyao katika Kata ya Makuburi wakati alipokuwa katika ziara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 hivi karibuni.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia) akipewa maelezo na Diwani wa Kata ya Makuburi, William Mwangwa (kushoto) kuhusu ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 kwa gharama ya Sh milioni 300 wakati alipofanya ziara katika barabara hiyo, Dar es Salaam jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Abbas Tarimba (wa pili kushoto) na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Gerald Urio. (Picha na Fadhili Akida).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mhe. meya umeshuhudia mwenyewe kanuni za usafi wa chakula zikipindishwa!

    Uchomaji wa nyama huku Mitaro ya maji machafu ikitiririika kwa mafuriko ya maji taka?

    ReplyDelete
  2. Hizi nyama choma za pembezoni mwa barabara balaa, tutakufa wengi!

    ReplyDelete
  3. Ohhh nyama choma za barabarani ile finyango moja tu mdomoni, tumbo linaanza kuunguruama hadi uharo!!!

    ReplyDelete
  4. kama matumbo yenu mabovu shauri yenu!!!wenyewe tunakula hatuumwi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...