Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kati kati kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Matale, Kata ya Mvomero akiwemo Muunguzi wa Zahanati ya Kijiji, Margreth Ngole na Diwani wa Kata ya Mvomero, Seleman Miraji ( wa kwanza kulia) juzi ( Jan 10) baada ya kukabidhi vitanda viwili na magodoro kwa matumizi ya wagonjwa kwenye Zahanati hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Sungusungu Kijiji cha Ndole, Kata ya Kinda, Lucas Henry , vifaa vya aina mbalimbali vya ulinzi kwa ajili ya Askari wa Sungusungu ‘Polisi Jamii’ wa Kijiji hicho kwa lengo la kuimalisha ulinzi ndani ya Kata hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinda, katika Kata ya Kinda, Wilaya ya Mvomero, Garusi Manyaku ( kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ( kulia) ikiwa ni ishara ya kupokea madawati 25 yaliyotolewa na Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo walipofanya ziara juzi ( Jan 10),kwenye Kata hiyo,( kati kati ) ni Kaimu Ofisa Elimu Salum Masalanga na nyuma ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo akiwa ameketi katika dawati pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kinda, iliyopo katika Kata hiyo baada ya kuukabidhi uongozi wa Shule madawati 25 aliyoyatoa masaada kwa lengo la kupunguza tatizo hilo wakati alipofanya ziara juzi ( Jan 10) kwenye Kata hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kati kati kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Matale, Kata ya Mvomero akiwemo Muunguzi wa Zahanati ya Kijiji, Margreth Ngole na Diwani wa Kata ya Mvomero, Seleman Miraji ( wa kwanza kulia) juzi ( Jan 10) baada ya kukabidhi vitanda viwili na magodoro kwa matumizi ya wagonjwa kwenye Zahanati hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ebu mtazame basi unayemkabidhi, we kila saa kutazama kamera tu.

    ReplyDelete
  2. Haya mambo ya mtu kiongozi kutoa hela ya mfukoni kwake kusaidia maendeleo naona ni ujinga tuu. Viongozi inabidi waweke sera na vivutio ili serikali au mashirika yaweze kusaidia shughuli za maendeleo na misaada ya maana iliyo endelevu kwa watu wote. Haya mambo ya kutoa vitanda viwili kutoka mfukoni kwake na kupigwa pigwa vipicha hayatatufikisha popote! Ina maana akiondoka leo basi hakuna vitanda zaidi vitatolewa?
    Acheni kutuhadaa wananchi. Michuzi najua utabania hii maana jamaa ni mshkaji wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...