Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa
Gari la Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa likiwa limebonyea kwa ubavuni baada ya kupata ajali Jumapili asubuhi.
--
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Edward Lowassa Mh. Edward Lowassa amenusurika kifo, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kupata ajali eneo la Bwawani mkoani Morogoro.
Sio dreva kwa ustadi mkubwa, ni Mungu aliepusha, tujifunze kumweka Mungu mbele kabla ya kuongelea ustadi wetu.
ReplyDeleteHaihusiani na mungu wala nini! kama ingekuwa hivyo basi waumini wasingekuwa wanapata ajali... madereva wawe waangalifu tu barabarani na NDIYO, ustadi muhimu kuliko imani!
ReplyDeleteAmina mdau wa kwanza.
ReplyDeletepole sana rais wetu mtarajiwa,alah ni mkubwa
ReplyDeleteKwahiyo dreva alitakiwa atulie tu amwachie mungu?
ReplyDeleteduu mtaani huku kila kona lowasa yupo nairobi mahutihuti
ReplyDeleteat list umetupa habar kamili
POLE MHESHIMIWA LOWASA.
ReplyDeleteMdau wa kwanza umenena!
ReplyDeleteEhhh,
ReplyDeleteJamani Morogoro ina mzimu gani na Mawaziri Mkuu wetu?
Mwaka 1984 tuliomboleza, na leo yanatokea haya tena!
Au ni kwa sababu ya Mlima Kolelo?
Naungana na mdau wa kwanza. Ni bahati mbaya kuona watu tunamsahau Mungu kwa matukio kama haya na kujichukulia stahiki isiyowastahili, siyo ustadi mkubwa wa dreva bali ni mkono wa Mungu uliowanusuru. Ni madreva wangapi wenye ustadi ukubwa ambao wamepoteza maisha yao kwenye ajali. Tujifunze na kukumbuka kumshukuru Mungu kwa kila jambo
ReplyDeletenaungana na mdau wa hapo juu 100 kwa 100
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteHajakosea hata kidogo.Umahiri wa dereva ndio uliofanya wanusurike.Mungu anawezesha katika jitihada zetu.Ndio maana Mungu anasema niiteni nami nitawaitikia,bisheni nanyimtafunguliwa. Jitihada zetu ndizo Mungu anatufanyia.Kama wengine wanakufa katika ajali kwa nini Mungu huyo asiwanusuru basi? ufanye uzembe useme Mungu atakuokoa?kwa nini tunaajili wadereva walio na sifa njema katika udereva na kufuzu kozi kama kila dereva anaweza kuendesha na Mungu akamsimamia tu?
ReplyDeleteI love this discussion!. Kila kitu tumuachie Mungu, sasa akili katupa za nini?. Walioendelea wanatumia akili Mungu alizowapa(waChina, Wajapan, waZungu), sisi tumekalia Mungu atusaidie. Tutumie akili na uwezo aliotupa, tusimuachie mzigo wote mwenyewe!!
ReplyDeleteANON WA Tue Jan 29, 09:08:00 AM
ReplyDelete"Walioendelea wanatumia akili mungu alizowapa"
Wachina- Akili zao ziliwapeleka kuona uzazi ni mtoto mmoja tu, kuna msiba mkubwa uko mbele yao. Athari ya hizo akili zinapelekea uchumi wao kuporomoka baada ya muda sio mrefu. Maana kizazi kinachozalisha na kulipia kodi hakitakuwepo kwa muda Fulani. Na wenyewe wanalijua hili.
Wajapani- Pamoja na akili zote, wanaangamizwa kila mara, kwenye misiba yote inayowakuta huwasikii kumtaja mungu hata mara moja. Tafakari.
Wazungu- Wanafilisika na akili zao zooote, why? Dhulma!
Afrika?- Mtu kitu kidogo tu, ama "mama yangu wee" AU "ee mungu nisaidie". Mitikisiko kwetu tunadunda tu.
Vyovyote itakavyokuwa, Mungu lazima atangulie mbele kwanza, jitihada zetu zinafuatia. Sio kinyume chake. Mungu hana mzigo unaomshinda.
ANON WA Mon Jan 28, 10:08:00 PM
Madereva wangapi "mahiri" wanaumia? Siku ya kufa nyani miti yote inateleza! hakuna cha umahiri hapo, mungu mwanzo umahiri unafuatia. Kuhusu kifo, siku ikifika utaondoka tu, kama siku yako bado, na mwenyewe mungu hajataka hata uchubuke ndio yatatokea haya ya Mh. Lowassa.
Tunachosema hapa ni kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, hii haina maana kuwa tufanye uzembe na kudai kwamba Mungu atatusaidia/tuokoa na ajali. Dreva anauhodari gani wakati pumzi yake iko mikononi mwa Mungu. Nasisitiza tena na tena Mungu kwa uhodari wetu baadae
ReplyDeletePole mheshimiwa na kila la kher ktk shughuli zako
ReplyDelete
ReplyDeleteAmina!
Mungu ametupa utashi na mengine mengi. Mungu yupo nasi daima. Angetutelekeza kwa kile alichokwisha tupatia, Shetani angechukua usukani. Hivyo basi Mungu yupoa nasi. Dereva alikuwa mcha Mungu na ndiyo maana wakati wa tukio akaweza kukwepea alikokwepea na wote kupona. Ubarikiwe sana Dereva. Endelea kumuweka Mungu Mbele.