Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzbar Msham Abdulla Khamis akifungua mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 kwa niaba ya Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Zainab Omar Mohammed leo mjini Zanzibar.Mkutano huo umewashirikisha viongozi na waratibu wa mbio za mwenge kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.
Mwenyekiti wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akiongoza mkutano huo leo mjini Zanzibar. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ali Nassoro Lufunga mkoa ambao ulikua mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2012.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge mwaka 2012 wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo kuhusu , mafanikio, changamoto na namna ya kufanikisha shughuli za mbio za Mwenge nchini.
Mratibu wa Mbio za Mwenge mkoa wa Iringa Bw. Atilio Mganwa akitoa mchango wake kuhusu uboreshaji wa shughuli za mbio za Mwenge nchini ambapo mkoa wa Iringa utakuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa Mwaka 2013.
Washiriki wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea mjini Zanzbar. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...