Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.

Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. 

Tembelea Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog kwa picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Usalama kwanza au madai kwanza?Nawapongeza waendesha kivuko cha Kigamboni kwa kutoruhusu kuendesha kivuko kilichobeba abiria kupita kiasi!jambo hili si la kulifumbia macho hata kidogo hawa vijana lazima waelewe kuwa ingewafaidia nini kama wangeondoka then kivuko kikazama!je ni kwamba kanuni na taratibu za usafiri za vyombo vyetu hawazijui!! Duu walimu kazi mnayo kuwaelimisha vijana hawa kuelewa umuhimu wa maisha yao!

    ReplyDelete
  2. Tunatumia kodi zetu kusomesha majambazi ona sasa!
    Hivi mpaka vurugu ndio watu wafanye kazi???

    ReplyDelete
  3. Inatisha! Hii ndiyo nguvu ya umma. Polisi wanazembea na maisha ya watu. Mpaka wanafunzi wanaamua kwa umoja wao kuandamana. Hapo walipo bila kufikiria ya kuwa hata pantoni haitaweza kuwavusha wote, lakini wako radhi kuingia wote ili madai yao yapate kusikilizwa. Inaonyesha jinsi gani mfumo mbaya wa utendaji kazi wa serikali na vyombo vya dola unavyoathiri maisha ya kila siku ya mtanzania wa kawaida.

    Tumewasikia! Mwenye macho haambiwi tazama!

    ReplyDelete
  4. Wasomi pamoja na pole kwa kadhia ya vitendo viovu vya majambazi, Je hamuogopi kufa kwa mamia jinsi mlivyojazana kupita kiasi katika kivuko na uwezekano wa kufanya ferry izame mkakosa usafiri kwa miezi kibao?
    Mdau
    Ferry Kigamboni

    ReplyDelete
  5. Sasa jamani, wizi halafu kulawitiwa kunaingilianaje? Hawa ni wezi wa laptop au wa nyota za hawa wanafunzi?

    Halafu hawa wanafunzi ndio viongozi/wafanyabiashara wa baadae, sasa kama jeshi la Polisi haliwezi kuwahakikishia usalama wa maisha yao sasa hivi, je wakiingia madarakani/biashara watawaheshimu polisi kweli?

    ReplyDelete
  6. Wanafunzi walichoshwa na uvamizi huu wa vibaka kwa kweli ,lakini elimu yao haikuwasaidia pale ambapo walifanya maandamano yasio halali niki maanisha hayakuwa na kibali.

    ReplyDelete
  7. Maguvu ya Polisi yanatakiwa yaelekezwe kwa Hao Wabakaji na Walawiti huko Kigamboni badala ya kuwagandamiza Wanafunzi wasio na Hatia!

    Kama POLISI mna NGUVU na uwezo mkubwa namna hii kwa nini msifanye Operesheni za Mara kwa mara dhidi ya hao WAHALIFU KIGAMBONI (Wezi, Wabakaji na Walawiti) badala ya kulaumiwa kwa kutumia nguvu dhidi ya Wadai ambao ni Wanafunzi wa IFM?

    Hivi Tanzania tunakwenda wapi?
    Polisi inakwenda wapi sasa?

    ReplyDelete
  8. Kamanda Kova,

    Hapakuwa na sababu ya kufanya msafara kwenda Kigamboni au kuendesha Mikutano, la muhimu ilikuwa ni matekelezo ya MAAMUZI KAZI kama hivi:

    Kwa kuwa ulitoa tamko kulishughulikia suala la muhimu ingekuwa:

    1.KAMA POLISI INASISITIZA ULINZI SHIRIKISHI KWA RAIA NA MALI ZAO, HUKU WAKIELEKEZA KUTII SHERIA ZA KIRAIA PANGEWEKA USIMAMIZI WA ULINZI SHIRIKISHI WAKIJUMUISHWA WANAFUNZI, WANANCHI NA POLISI HUKO KIGAMBONI.

    2.KUNGEFANYIKA DORIA YA MARA KWA MARA ZA OPERESHENI ZA KIPOLISI ILI KUKABILIANA NA WAHALIFU, KWA SABABHU HAWA WAHALIFU NI SEHEMU YA JAMII YETA NA ULE UWEZO WA KUFANYA UASI WAO (MODUS OPERANDI) WANAUPATA KUTOKANA NA KUISOMA NA KUIJUA JAMII WALIYOPO VILIVYO.

    Hivyo matekelezo ya uamuzi yangefaa zaidi kuliko misafara na mikutano mingi ambayo imepelekea mambo kufikia kulaumiana na watu kupata maafa yasiyo na sababu zozote.

    Hapa ilitakiwa kukabiliana na suala zima la Uhalifu moja kwa moja bila kupoteza muda wala ajizi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...