Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Tabora waliofika kwenye Stesheni ya treni ya mkoa huo kuupokea ujumbe wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye wakiwaaga Wanachama wa CCM maeneno ya Stesheni ya Seranda,wilaya ya Manyoni mkoani Singida.wakati ujumbe wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM ulipopita eneo hilo mchana wa leo.
Vijana wa Chipukizi Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana wakati alipofika kwenye Kituo cha Treni cha Saranda mkoani humo na kuzungumza na WanaCCM wa Manyoni.Mh. Kinana na Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wako safarini kuelekea Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM.
"Bai Baii.........!! "hivi ndivyo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye walivyokuwa wakiwaaga wanaCCM wa mji wa Saranda,Wilayani Manyoni.
Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na WanaCCM wa Manyoni.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wanaCCM wa Manyoni,Mkoani Singida wakati waliposiama katika kituo cha Saranda.
Mbunge wa Jimbo Manyoni,Mh. John Chiligati akizungumza.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.
Endeleeni na jitihada hizo viongozi wa ccm, 2015 tunataka ushindi wa kishindo na kusambaratisha upinzani wa chama fulani.
ReplyDeleteHivi CCM hilo treni wamekodi au treni hilo linafanya safari hii kama safari nyingine? Namaanisha safari za kawaida. Naomba ufafanuzi.Picha ninayopata mpaka sasa ni kama vile mtu aliyekodi teksi.
ReplyDeleteHivi ukiwa kwenye train hauruhusiwi kuoga?Maana ndugu zangu wakuu nawaona na nguo zile zile wala hawajabadilisha.
ReplyDeleteWe ndau hapo juu mbona majungu jamani! Zungumza mambo ya kuleta maendeleo mtu akioga au asipooga inakuhusu nini? Angalia hilo treni, angalia wanayoyafanya, angalia hali ya nchi kwa sasa! Kisha tafakari, toa maoni!
ReplyDeleteMdau wa Tatu (3) hapo juu Sun Jan 27, 03:55:00 pm 2013
ReplyDelete...wanaruhusiwa kukoga kwenye Treni?
Kama uliliona hilo kwa nini wewe usingeandaa ndoo za maji,ndara, mataulo na sabuni ili viongozi waoge wakiwa safarini?