![](http://api.ning.com:80/files/u-xZvHIxjSJmufxBOCgm-jIxPlYJ-vBs4WMUqUk2VxuuEkU6MnjFCZxloIu4CLPwgj5ijQjr4OxMICY5NpGcwfe0ugw3Zia8/SHINDANOAH4.jpg?width=650)
--
MSHINDI wa Bahati Nasibu ya 'Timiza Ndoto Yako, Jishindie Toyota Noah' ambayo ilikuwa inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Ramadhan Salum Pazi, mkazi wa Buguruni-Rozana jijini Dar es Salaam, leo amekabidhiwa gari lake aina ya Toyota Noah.
Makabidhiano hayo yamefanywa na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan nje ya ofisi za Global Publishers.
Bahati Nasibu hiyo iliyokuwa inaendeshwa kupitia magazeti ya Global ambayo ni Uwazi, Risasi, Championi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda ilifika mwisho Desemba 20 mwaka jana ambapo bwana Ramadhani Pazi aliibuka kidedea.
HIYO BAHATI NASIBU YA KWELI AU YA KUPANGA MATOKEO MBONA ALIYESHINDA HANA FURAHA KABISA WALA SURA YAKE HAIONYESHI KUSHINDA KAMA VILE ANALAZIMISHWA KUSEMA YEYE NDIO MSHINDI MAANA BAHATI NASIBU ZA MJINI WASHINDI HUWA WANAJULIKAMA MAPEMA HUENDA YEYE NI RUBBER STAMP TU HAPO BINAFSI NINA WASIWASI NA USHINDI WAKE TUTAMUONA NALO MJINI KAMA KWELI KASHINDA!!
ReplyDeletemtu unapata zawadi unashindwa hata kuonyesha jino moja, umenunaaaaaaaaa au mshindi wewe ulikuwa unataka vogue sport? ha ha haaaa.. wenzako wanashindi bajaji unaona meno yote hamsini mdomoni.
ReplyDeleteOpossum (Didelphis Virginiana)aka The North America Opossu, wa MEXICO wanamuita Tlacuache, ndiye mnyama pekee mwenye meno HAMSINI, sisi binadamu tuna meno 32 tu, kama hujan`goa hata moja, au hujapoteza meno kilabuni!
ReplyDelete