Hii ndio hali ilivyo katika barabara kuu iendayo Lindi na Mtwara
kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo hayo.Abiria wa Mikoa hiyo wamekuwa
katika wakati mgumu kutokana na magari mengi kunasa kwenye tope lililotoea kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo,baada ya kukaa kwa muda mrefu,msaada wa kampuni ya Kharafy and
sons -mkandarasi wa barabara hiyo ya km 60 alifika eneo la tukuo na kusaidia kuvutwa magari yaliyonasa.Picha na Mdau Abdulaziz Video,lindi.
Home
Unlabelled
Mvua zakwamisha Abiria waendao Lindi na Mtwara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HALI KAMA HII NDIO INAYOCHOCHEA MAANDAMANO YA KUPINGA GESI KUSAFIRISHWA KWENDA DAR, HIVI NI KWELI MIAKA 51 BAADA YA UHURU BADO HAKUNA BARABARA YA UHAKIKA KWENDA KUSINI, JAMANI TUKIDAI TUNAAMBIWA TUNATUMIWA KISIASA WAKATI MAZINGIRA YA KUTUMIWA KISIASA SERIKALI INAYATAYARISHA YENYEWE, CHONDE CHONDE BABA JAKAYA KTK HIZO KM 11,000 ZILIZOSEMWA NA WAZIRI MAGUFULI BASI WALAAU 400 ZIWE ZA BARABARA YA KUSINI DAR-LINDI- MTWARA
ReplyDeleteMkiambiwa mikoa hiyo iko nyuma na inataka maendeleo mnapinga. Ukweli huu unawaumbua wenyewe. Rasilimali zitbumike kuendeleza mikoa hii.
ReplyDeleteSasa wauze gesi ili wapate misaada. Huku Dar hakuna atakaewasaidia. watajiju.
ReplyDeletePicha zinaonekana vizuri kwelikweli kiasi cha kuielewa vizuri mno taarifa hii ya mvua zinazoendelea kusini.(ujumbe umefika).
ReplyDeleteNi wazi ya kuwa tuachane na CENTRALIZED DEVELOPNETS na CENTRALIZED ADMINISTRATION, Ndio maana Muasisi baba wa Taifa Kambarage Nyerere alianzisha Suala la Madaraka Mikoani ili kusambaza Uwezo wa Utawala kuwafikia Wananchi katika maeneo yao na pia ili Maendeleo nayo yaweze kuwafikia huko walipo.
ReplyDeleteIngawa pana sababu nzito za Kibiashara na Kiuchumi kwa Gesi kuletwa Dar, lakini tuangalie pia kwa mtazamo huo wa KUEPEKA KUELEKEZA MAENDELEO KWENYE SEHEMU MOJA TU YA NCHI YAANI DAR ES SALAAM.
Hivyo kwa upande mwingine wananchi wa Mtwara wana haki ya kudai rasilimali ziendelezwe katika eneo lao ili matatizo ya Uhamiaji mijini kama Umachinga vipate Suluhisho la kudumu.