Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula (kulia) akimkabidhi funguo ya nyumba, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid baada ya kununua nyumba ya shirika hilo iliyopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid. 
Mkurugenzi  wa Mipango Uwekezaji na Miradi wa  Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Yacoub Kidula akiangali akikagua nyumba ya shirika hilo kabla ya kuikabidhi kwa mnunuzi wa nyumba hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Hamid Mahmoud Hamid. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid.
Baadhi ya nyumba za Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilizopo katika eneo la mradi wa nyumba za bei nafuu huko Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KUONA ZAIDI NYUMBA HIZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hawa wakubwa wanazo nyumba hawatosheki uzieni watu wa chini si kujilimbikizia mali ndio maana umasikini hauishi

    ReplyDelete
  2. Inaonekana ni nyumba nzuri lakini finishing bado ni tatizo ukiangalia edge ya hizo kitchen countertops hazipo smooth!Sasa kama kwenye picha hiko hivi sijui kwa karibu kabisa zinaonekanaje!Taratibu tutafika!

    ReplyDelete
  3. Sasa Wandugu mmeshindwa hata ku-maintain mazingira ya nje? Kwani ina cost kiasi gani kupata wafanyakazi wa kusafisha hapo nje kuondoa magugu na kukata majani kupafanya pavutie kidogo? Mbona kila kitu mnachofanya ni sub-standard? Kwani kwakuwa ni nyumba za bei nafuu ndo ina maana hazisafishwi? Mdau, CA, USA

    ReplyDelete
  4. Hawajamaa bwana kila siku wanapoweka hizi taarifa zao za nyumba za bei nafuu kwanini wasiweke na bei kabisa tukauona huo unafuu, maana kila wanapotoa taarifa zao ukisoma haioneshi gharama za hizo nyumba zao.

    ReplyDelete
  5. wanaouziwa ni wanachama au ni yeyote mwenye fedha, kama si wanachama kuna juhudi gani za kuhakikisha wanachama wanafaidi kwanza matunda ya michango/uanachama wao?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...