Na Atley Kuni.
Zoezi la Chanjo limefanyika kimkoa katika Wilaya ya Sengerema kwenye Tarafa ya Sengerema kijiji cha Sima na Kata ya Sima Mkoani Mwanza.
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evaristi Ndikilo amesema zoezi hilo kimkoa ni lazima lifanikiwe kwa mujibu wa malengo walio jiwekea ya 95% kwa kila wilaya kinyume chake wale wote watakaoshindwa kufikia lengo itabidi wajieleze na sababu zilizofanya washindwe kuvuka malengo katika Mkoa wake.
Ndikilo amesema yeye kama mtendaji Mkuu katika Mkoa wa wa Mwanza hayupo tayari kuona Mkoa huo unakuwa wa mwisho katika zoezi hilo.
Amewahimiza wazazi kujitokeza kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo hiyo kwani kuacha kuwachanja watoto, si hatari kwa mototo tu, bali pia watoto wenzake wanao mzunguka hivyo ni vema kila mzazi akaona umuhimu wakumpeleka watoto katika chanjo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewahakikishia wananchi wa Sengerema na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla wake kuwa, chanjo hiyo ni salama kwakuwa imefanyiwa utafiti wakutosha na wataalam wa afya wa Ulimwenguni na Wizara ya afya hapa nchini.
Akihututubia mamia ya wananchi wa kijiji hicho cha Sima, Amesema watoto wa chini ya miaka 5 wanachangamoto nyingi, hasa kwenye nchi zetu hizi zinazo endelea , kwani kwingineko kwa nchi zilizo endelea watoto wanao zaliwa hukua kwa takriba ni 99% tofauti na hapa kwetu.
Amesema ugonjwa wa kichomi huua watoto kwa 14% ukitanguliwa na Malaria ambao huuwa kwa asilimia 15% huku ugonjwa wa kuharisha ukishika nafasi ya tatu kwa kuuwa watoto wengi kwa asilimia 12% kwani nchini Tanzania kila mwaka watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wapatao takriba ni 198,443 huugua ugonjwa wa kuharisha na kati yao 13,397 hufariki dunia.
Ujumbe mahususi wa siku hiyo ni Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye afya, ameongeza kuwa Chanjo hiyo ni sehemu ya Ilani, hivyo kufika 2015 jamii ya kitanzania iwe ni jamii iliyo na ustawi.

Magonjwa ambayo hadi hivi sasa yana chanjo ni donda koo, kichomi, kuharisha, pepopunda, kifua kikuu, surua, homa ya uti wa mgongo, kifaduro, homa ya ini, na polio, haya ndio magonjwa yaliopo katika mpango wa Taifa wa chanjo alisema na kuongweza.
Amehiza viongozi wa kila ngazi kuzindua kampeni hiyo, na watoto walengwa ambao ni kuanzia wiki 6 hadi wiki 32 wapatiwe chanjo hiyo bila kukosa.
Jumla ya watoto 149,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hiyo na amesema zoezi hilo ni endelevu hadi tarehe 31. DEC. 2013.
Kaulimbiu ya katika maadhimisho hayo ni kuwa “Mtoto asiye chanjwa ni hatari kwake na kwawenzake, mpeleke mototo wako akachanjwe”.
Ofisi ya Mkoa ya Mwanza itoe Ufafanuzi,Mchanganuo(breakdown by sources),hizi Takwimu za Pato la Wastani kwa Mwaka kwa mkazi wa Mwanza (Regional Pa Capita Income),kwamba,limepanda kutoka shs.400,000/=(approxy) hadi shs.800,000/=(approxy)kati ya mwaka 2005 hadi 2012,wamezipata wapi?nani aliyezikokotoa?je,ofisi ya takwimu mkoa wa mwanza inao uwezo huo kitaalamu na nyenzo cha kuifanya kazi hiyo ya kukadiria Pato la Mkoa? sisi wakazi wa mkoa wa mwanza,tunaujua vyema mkoa wetu na hali halisi ya uchumi wake.Dishing out sensational statistics that do not reflect the realities on the ground does not "eliminate poverty",not at all! mwanza sio mbumbumbu!watu wamesoma!kwa hilo la chanjo,nawapa hongera kwa jitihada hizo!kilimo kimesahaulika kabisa,tembea vijijini uone;samaki ziwa victoria wamekwisha,tuseme wame adimika mno tokana na uvuvi usio na tija;madini,kawaulize GGM,vipi watu bado wanakunywa maji ya tope na dhahabu imejaa tele!Statistics do not hide facts on the ground!no matter how you cook them!zero willa always remain zero!kuna msomi mmoja alipata kuniambia,days back,kwamba,"the only constant in change(the process of change),is change itself".Sasa hebu nyie wanasiasa wetu jaribuni kuilazimisha "change iwe constant",tuone,mtaweza?badilikeni jamani,people can never be fooled again!
ReplyDelete