Home
Unlabelled
UFAFANUZI KUHUSU MIRADI YA UTAFUTAJI NA UVUNAJI WA GESI ASILIA NCHINI KATIKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nahisi watu wa Mtwara na Lindi wanachoitaji ni ajira.Sasa hii gesi ikiwa inapita juu kwa juu kutakuwa hakuna manufaa kwao.Bora ingekuwa inasambazwa kutoka mikoa hiyo na wao wakapata kazi.
ReplyDeletenafikiri kuna mambo mengi ambayo serikali imechemsha , ina rushwa imejaa , viongozi hujinufaisha wenyewe kwa kujipangia mambo mazuri mazuri na kuwasahau wananchi ambao ndio waliowapa mamlaka ya kuwatawala , lakini ukiangalia kwa undani hakuna hata mmoja ktk nchi yetu hii na dunia kwa ujumla anayemtakia mtu mwengine heri au faida , angalia hata ndugu kwa ndugu au rafiki kwa rafiki huhasimiana kwenye masuala ya maslahi, si CHADEMA wala CUF wala CCM wala chama chochote kile kinataka kumpatia maslahi mwananchi kila mmoja anaangalia tumbo lake na familia yake huo ndio ukweli. Lakini haya maneno yaliandikwa ktk barua hii yanapaswa kuungwa mkono, kwa hapa serikali imesema sawasawa.
ReplyDeleteProfeza,
ReplyDeleteHaya maneno ni mazuri lakini nayo yamejaa blah blah blah. Umejitahidi sana kuleta historia; ila nazo ni full blah blah bla. Miaka milioni blah blah nani anataka kujua? Nautical miles blah blah mimi mvuvi wa Msimbati najua hicho ni nini? Mbona hizo Nautical miles haziko Mara? Unajua ama umeanza kuwa mwanasiasa au umeandika hili tangazo au niseme karipio kwa jazba; kwa kuwa umeainisha mazao meeengi ya biashara halafu kwa makusudi ukasahau korosho, hizo ni blah blah blah Profeza. Anyways, Nafikiri sina shida na mipango ya serikali ila nachelea utimilifu wake ndiyo inaweza kuwa shida. Pia kwenye hizi blah blah kuna kitu hujagusia kwa mfano wapinzani wamekuwa wakifanya blah blah blah juu ya uwezekano wa ugunduzi wa gesi hapa Dar Es Salaam, hili likoje? Mbona umelichunia? Au unataka kutuambia hizi ni blah blah
Ila asante mwaego kwa taarifa; ila hili mnalo maana wapinzani wamepatia pa kushika. Mweee.
Kamnunile Kungoma-Blah blah
Wananchi wa Mtwara na Lindi hawajakataa gesi kusafirishwa kwenda maeneo mengine ya nchi. Wanachotaka wananchi wa Mtwara na Lindi na ambacho Serikali inapotosha makusudi ni kuwa mtambo wa kuzalisha gesi ujengwe eneo husika na gesi isafirishwe na kwenda kuunganishwa kwenye gridi ya Taifa. Kwa nini halijajengwa bomba la maji toka Mtera kija Dar ili umeme uzalishwe hapo.Ukijengwa mtambo wa kuzalisha umeme vijana wa Mtwara ambao wengi wao ni Machinga wa hapo mtaa wa Kongo watarudi kwa kuwa ajira itakuwepo huko, na ieleweke kuwa vijana hao hawaji hapa mjini kwa kupenda bali mazingira ya huko huwalazimisha hivyo.Watu wa Mtwra na Lindi wamejifunza kutokana na matokeo ya seheme nyingine ambako serikali imewafanyia kama ambavyo wanatka kufanya huko.
ReplyDeletebinafsi sielewi kwa nini kila kitu kiwe Dar. jenga hivyo viwanda kwingine, jenga hizo gridi kwingine. yaani jiji la Dar limekwishakuwa kero. unatoka nyumbani saa 12 asubuhi unafika ofisini saa 3. jamani hamuoni umuhimu wa kujenga kwingine.
ReplyDeletekwani umeme ukifiliwa Mtwara au Lindi hauwezi kuingizwa kwenye gridi? kila kitu Dar kila ktu Dar. inaudhi.
naunga mkono kauli ya profesa kuangalia umoja wa kitaifa zaidi. Kuhusu ajira hao wamachinga wanaweza kuajiriwa popote katika ardhi hii ya tanzania , no matter where kiwannda kitakuwepo. Hivi unadhani unaweza kuajiriwa kwa kiwanda kuwa kwako la hasha, ni vigezo, ujuzi na ufundi (skill, experience and knowledge). Jamaa wa blah blaa hapo, nadhani unazungumza blah blah, hii nchi imeundwa kwa msingi ya umoja, na tusifikie mahali tukagawanyika kirahisi. Inazekana walikuwa wanasababu ya kuandamana ila mabango yao yaliashiria ubaguzi wa dhahiri, nalo si jambo sahihi. Jamani akili za kuazimwa changanya na zako, lakini si katika swala la kuagawa nchi hii then ukasupport kwamba ni jambo sahihi.
ReplyDeleteUncle gesi hii ni ya ntwara na lindi sasa kwenda kuendeleza darisalama mi naona si sawa. Kwani huku hatuwezi kuwa kama darisalama! Ba ndugu zangu nisaidieni sisi huku mpaka tupate maendeleo na si kuwa daraja la haoo wengine
ReplyDeleteSospeter! Umeona tofauti yaa siasa ana kazi ulokuwa unafanya mwanzo? Unalazimishwa kusema bla bla? Mazao yote uloyasemwa hayo yanalimwa na serikali? Hivi mimi nijipinde shambani halafu mtu mwingine aje adai kufaidika na shamba langu? Hivi yale amji ya mtera wa mtera hawafaidiki nayo? ule umeme unaofuliwa mtera wa mtera hawaupati? Kwanini gesi bomba hiloooo lipite kwenda dar wa mtwara hawataki gesi? halafu kutoka dar ndo manufaa ya gesi yarudishwe mtwara?
ReplyDeleteMtwara wamefungua njia subirini na wa mikoa mingine waamke.
ISSUE HAPA NI MAENDELEO KUWEPO BAADHI YA MIKOA TU, KAMA SERIKALI NI ADILIFU MBONA MIKOA MINGINE IMEENDELEA KWA PESA ZA WOTE NA MTWARA IKASAHAULIKA NDIO MAANA WANA MTWARA WANATAKA SASA WAENDELEE KWA KUTUMIA RASILIMALI ZAO TATIZO LIKO WAPI, HAPA TUNAANDAA VITA, NANI ATASIKILIZA WIMBO MZURI HUKU ANA NJAA, SERIKALI INATAKIWA IFANYE UADILIFU NA SIO KULETA TAKWIMU ZA UJANJA UJANJA, MIE NASEMA KILA JAMBO LINA WAKATI WAKE, HATA HII KUFANYA BAADHI YA WATANZANIA MAZUZU LITAKWISHA.
ReplyDeleteTaarifa ya Wizara ni nzuri,kama ni kutoa ushauri zaidi basi wananchi watoe kwa kuzingatia umuhimu na maslahi ya Taifa letu kwa ujumla. Hebu tuache kubeza taarifa kisa tu tunaongozwa na hisia za mapenzi na vyama fulani fulani. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
ReplyDeleteTatizo la Siasa ni Uongo. Hata pale dhamira ya mtu inamsuta kutokana na imani yake ya Kiroho; bado analazimika kumtumikia shetani. Hiki ndicho ninacho kiona kwa Prof. Muwongo.
ReplyDeleteHapa Dar pamejaa. Maji hayatutoshi; Nyumba za kulala hazitoshi hata vyoo havitoshi kwa jinsi (kajisemea yule jamaa tumezaliana) tulivyojurundika hapa.
Kwa vipi hatuioni hii fursa ya kutaapisha huu utitiri urudi Mtwara na Lindi. Kama mtu anaweza ajiriwa popote, kwenda Mtwara kuna hitaji Passport au Work permit kwa Mtanzania? Tuache kurubuniwa hadi fikra. Tumuogope Mungu.
Wamachinga tulio wakimbizi Dar, tunadai maendeleo yetu. Na Rasilimali ndiyo hii
Je na wewe umetoa "assumption" kwa mrengo wa Chama unakokula? Makazi makuu ya Mamlaka za Pamba, Korosho, Kahawa, Katani zilivyojengwa DSM, ilitufikisha wapi? Kwa nini hatujifunzi kutokana na makosa yetu? Kwa nini utumwa wa fikra hau tuishi?
ReplyDeleteHili la Mtwara ndilo tulilo azimia katika Decentralization by Devolution? Kwa nini tu wabinafsi kiasi hiki?
Hapa rasilimali ni yetu wote Watanzania. Ila itakuwa processed Mtwara kwa ushirikiano wa Watanzania wote. Utofauti wa maendeleo Kimkoa unadhihirisha umuhimu wa kufanya haya wananchi wanayodai.
Ubishi wa viongozi wetu kuona na kuheshimu ukweli ni Janga
Hapa inategemea anayeongea yuko upande gani, lakini ukweli wa nchi hauoneshi kama rasilimali za Nchi ni za Watanzania, ila labda ni za watawala. Ndio maana gap ya kimapato ni kbwa sana kati ya watawala na watawaliwa. Nchi nyingine gapa kama hii hutokana na juhudi za kila mtu kibiashara, lakini hapa kwetu Gap kubwa inatokana na uhusiana wako na watawala, ndio maana watu wengi wanatumia nguvu za ajabu kuhakikisha wanakuwa watawala! Tumeona wafanya biashara wanapanda na kushuka kutokana na ni nina yuko madarakani. Sasa hii inapoteza uhusiano asilia wa nguvu za kijasiliamali na kurundika railimali nyingi kwa wachache wenye "coccections". Na hao wachache wanahama kabisa kwenye jamii au maeneo ya wenzao ambayo bado hawajashiba!!
ReplyDeleteNdio maana kuna taswira kwamba rasilimali sio za wa-TZ wote!
Mimi kwa upande wangu bado nasimamia kwa wananchi wa Mtwara wasikilizwe hoja zao ni za msingi. Pamoja na kwamba Utalii uko zaidi ukanda wa kaskazini na watanzania wote wanafaidika lakini bado wale walioko mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wanafidika zaidi sababu kuna kuwa na mzunguko mkubwa wa hela na wafanyabisha za utalii wanajikita katika maeneo hayo hivyo kutoa ajira kwa walio wengi. Wizara inatamka kwamba mikoa inayozalisha mahindi inalisha watanzania wote ni sawa lakini mbona sasa hivi Serikali imejikita katika kuimarisha miundo mbinu ya Kanda ya Mikoa inayozalisha mazao hayo kwa nini na Mtwara isifikiriwe kama Mikoa mingine. Serikali sasa kupitia Wizara ya Utalii inafanya bidii kutangaza hifadhi za kusini kwa kutafuta wawekezaji na kuimarisha miundo mbinu kutokana na rasilimali ya Hidahfi ya Ruaha, kwa nini Mtwara nao wasiimarishiwe miundo mbinu ikiwapo kujengewa mtambo wa gesi ambao utawavutia wawekezaji na kukuza uchumi katika Mkoa huo na iliyopo karibu? Bado naona kuna sababu ya Wanamtwara kudai haki yao.
ReplyDeleteKama wakuu wa mikoa wangekuwa wanachaguliwa kutokana wa wabunge na madiwani kutoka huo mkoa or na wananchi wa huo mkuo wakati wa uchaguzi mkuu wa nafikiri hii ingesuluhisha mambo mengi. Kwani wakuu hawa wangechaguliwa kutokana na uzito wa sela zao kutokana na kulinda pamoja na kutetea maendeleo ya huo mkuo kufuatana na katiba ya muungano. Mfano mgombea wa mkuu wa mkoa wa Arusha aliyekuwa mchimba madini kati ya sera zake jamaa atatetea haki na mazingira bora ya wachimbaji, bei bora ya madini, partnerships na foreign investors, local market ya tanzanite na uwekezaji na uboreshaji wa process industry za tanzanite nchini ili kuset price na ku take advantage of that. Maybe mgombea mwingine from Arusha hapo hapo ni environmentalist ambae anao utunzaji wa mazingira na ajira kwa wote na tourism ni bora zaidi and so on. Ikienda mikoa mingine hivyo hivyo mfano kigoma wawe na kiwanda cha kupack na kusindika samaki, kusaidia wavuvi ujenzi wa barabara na madaraja and so on. My point is, kama mkuu wa mkoa hatoki ndani ya mkoa huo basi yeye haoni umuhimu wa fight for them, ndio maana kuna wakuu WENGINE wako dedicated to their job lakini wakija kuja kuhamishwa yule anakuja akija na agenda nyingine anasahau zile ptoject nyingine. Hii ndio imeua vyama ushirika na vitu vingine . Jana Mjengwablog anasema alivuka daraja kwa kuogelea mwaka 1983 huko Mbeya , mpaka leo daraja halijajengwa. Ndio maendeleo yaende kote lakini Mbeya ni one of biggest food producer in Tanzania lakini hatuwezi kuwareward wakulima wake kwa daraja litakalo cost chini ya 20 mil? Kama wakuu wa mikoa wanatoka kwenye mikoa hiyo sio Kabila la mkuo huo but from there, nafikiri watakuwa wana fight for maslahi ya mkoa zaidi ya matumbo yao
ReplyDeleteMdau Ohio
Tanzania ndiyo nchi pekee inayongoza duniani kuwa na viongozi waliokwenda shule. Wooooooooooote ni madaktari (PhD) holders. Kwanini tusijifunze kwa majirani zetu, kama Kenya na Rwanda, wanaoongozwa na viongozi wasio madaktari? Hakuna nchi hata moja ya G8 yenye raisi daktari lakini wao matajiri, sisi malofa. Kama viongozi hawa wasingekuwa na elimu kwa viwango vya udaktari, Tanzania ingekuwa wapi? Kwahiyo inawezekana tanzania tunajifunza ujinga kupitia elimu yetu, ama tuluzaliwa wajinga.
ReplyDeleteI was so disappointed with the remarks made by Sospeter!kweli,kusoma sana sio kila kitu katika maisha!Watanzania wa Mtwara ujumbe wenu umefika,subirini mabadiliko,change is coming!we are used to puppeteering and sloganeering!talk is cheap!
ReplyDelete