Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (katikati).
Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akipata maelezo kuhusu Kitengo cha Utafiti cha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bw. Mohammed Hamad leo mara baada ya kutoa maoni yake kuhusu katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao leo kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Prof. Mwesiga Baregu.
Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela akitoka nje ya ukumbi wa mikutano wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo mara baada ya kutoa maoni yake kuhusu katiba Mpya. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na kulia ni Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. toeni maoni baba zangu lakini mkae mkijua wazanzibari wameshaanka katika ule usingizi wa pono wa kufaa sasa wako hai wanachotaka ni nchi yao yenye mamlala kamili koti lina wabana na hawako tayari kufanya mazoezi wakonde ili walitumiye tena koti wameshachoka na koti hili na koti la viraka huwa wanao vyaa ni machizi si watu wenye akili timamu so wanataka koti jipya ndo wanachotaka longa longa zenu kaeni nazo wenyewe wameshaamka jamaa hawa jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...