Kundi la Odissey na ngoma yao ya 'Going back to my Roots' lilitesa sana enzi zetu
Home
Unlabelled
ngoma azipendazo ankal - enzi hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
ankal hii nyimbo imekuwa kigungua kinywa changu,kazi kwa kwenda mbele
ReplyDeleteEnzi hizo tuliimba:..... kama una noti zililete leo zishindane na maua *3 then we sang: sisi makaburu tunavaa tinabul yee.....
ReplyDeleteBlackmpingo
Enhhee?
ReplyDeleteHivi inafikia mimi mtu mzima na 'bandawe' langu kichwani nalia?
Ni huu wimbo ''Going back to my roots'' unanifanya nilie nikikumbuka miaka yangu nikiwa handsome boy na sina bandawe 'upara wa uhalaza' kichwani nikicheza na kuzidiwa na Muziki enzi hizo nilikuwa nashika utosi wa kichwa changu kikiwa na nywele zake laini nzuri na nyeusi!,,, lakini sasa huku nikilia machozi nikishika utosini mwa kichwa changu kwa masikitiko na kumbukumbu ya zamani nafuta jasho juu ya kipara!
Ohhh hivi sasa kichwani kwangu nashika Uwanja wa ndege au Zege linalomwagwa la Mabasi yaendayo KASI JIJINI DAR!
Ahhh mimi Mzee Mzima wa za zile za zamani Enzi zile niacheni niendelee kulia kila siku Michuzi akitundika kete zetu za enzi hizo!!!
Uwiiiiiiii !
ReplyDeleteUwiiiiiiii !
Uwiiiiiiii !
...watoto wa Kizazi Kipya msinicheke mtu mzima wa Zile za Kale nikilia mtapata laana.
Ankali achilia Mdau wa tatu Babu mwenye Kipara cha uhalaza Anony wa Thu Jan 10, 12:04:00 PM 2013, Hivi sasa nina nywele zimekakamaa kama magugu za kizee hata mafuta haziyakubali, mimi nulikuwa na Afro langu kichwani kama huyo Brazameni anayeimba hapo!
Ahhh, katika haya maisha yetu vitu viwili vinakumbusha sana yaliyopita navyo ni Picha za zamani tulivyokuwa na pia Muziki wa Kipindi hicho kama huu !
Kizazi Kipya mtake msitake sisi za Za Kale tumewafunika kila Idara, angalieni kitu hichi 'Going Back to my Roots' !!!
ReplyDeleteSi mtatutaka ?
Ama kweli maisha yanatudanganya sana!
ReplyDeleteTulitegemea enzi miziki hii inapigwa tutakaa tukiwa vijana wabichi kumbe wala sivyo!
....Matokeo yake sasa maisha yamesogea, umri umesogea na sasa tumebakia tunafuta majasho ya vipara!!!
Unanikumbusha mbali Mzee Michuzi mpaka Machozi yananitoka kwa furaha. Japokuwa sasa nina KIPARA, SINA MENO, MAGOTI MABOVU, KIUNO NA MGONGO NDIO BALAA. Nyie vijana atakayenicheka ataota ndundu.
ReplyDeleteDah hili debe nakumbuka sometimes lilikua linapigwa Empire cinema befor movie la Jack chan halijaanza....we acha tu halafu kinu kilikua kinakita kama uko disco vile....
ReplyDeleteHawa dot.com hawajui hata Empire cinema ilikua wapi.