Kundi la Odissey na ngoma yao ya 'Going back to my Roots' lilitesa sana enzi zetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. ankal hii nyimbo imekuwa kigungua kinywa changu,kazi kwa kwenda mbele

    ReplyDelete
  2. Enzi hizo tuliimba:..... kama una noti zililete leo zishindane na maua *3 then we sang: sisi makaburu tunavaa tinabul yee.....
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  3. Enhhee?

    Hivi inafikia mimi mtu mzima na 'bandawe' langu kichwani nalia?

    Ni huu wimbo ''Going back to my roots'' unanifanya nilie nikikumbuka miaka yangu nikiwa handsome boy na sina bandawe 'upara wa uhalaza' kichwani nikicheza na kuzidiwa na Muziki enzi hizo nilikuwa nashika utosi wa kichwa changu kikiwa na nywele zake laini nzuri na nyeusi!,,, lakini sasa huku nikilia machozi nikishika utosini mwa kichwa changu kwa masikitiko na kumbukumbu ya zamani nafuta jasho juu ya kipara!

    Ohhh hivi sasa kichwani kwangu nashika Uwanja wa ndege au Zege linalomwagwa la Mabasi yaendayo KASI JIJINI DAR!

    Ahhh mimi Mzee Mzima wa za zile za zamani Enzi zile niacheni niendelee kulia kila siku Michuzi akitundika kete zetu za enzi hizo!!!

    ReplyDelete
  4. Uwiiiiiiii !
    Uwiiiiiiii !
    Uwiiiiiiii !

    ...watoto wa Kizazi Kipya msinicheke mtu mzima wa Zile za Kale nikilia mtapata laana.

    Ankali achilia Mdau wa tatu Babu mwenye Kipara cha uhalaza Anony wa Thu Jan 10, 12:04:00 PM 2013, Hivi sasa nina nywele zimekakamaa kama magugu za kizee hata mafuta haziyakubali, mimi nulikuwa na Afro langu kichwani kama huyo Brazameni anayeimba hapo!

    Ahhh, katika haya maisha yetu vitu viwili vinakumbusha sana yaliyopita navyo ni Picha za zamani tulivyokuwa na pia Muziki wa Kipindi hicho kama huu !

    ReplyDelete
  5. Kizazi Kipya mtake msitake sisi za Za Kale tumewafunika kila Idara, angalieni kitu hichi 'Going Back to my Roots' !!!

    Si mtatutaka ?

    ReplyDelete
  6. Ama kweli maisha yanatudanganya sana!

    Tulitegemea enzi miziki hii inapigwa tutakaa tukiwa vijana wabichi kumbe wala sivyo!

    ....Matokeo yake sasa maisha yamesogea, umri umesogea na sasa tumebakia tunafuta majasho ya vipara!!!

    ReplyDelete
  7. Unanikumbusha mbali Mzee Michuzi mpaka Machozi yananitoka kwa furaha. Japokuwa sasa nina KIPARA, SINA MENO, MAGOTI MABOVU, KIUNO NA MGONGO NDIO BALAA. Nyie vijana atakayenicheka ataota ndundu.

    ReplyDelete
  8. Dah hili debe nakumbuka sometimes lilikua linapigwa Empire cinema befor movie la Jack chan halijaanza....we acha tu halafu kinu kilikua kinakita kama uko disco vile....

    Hawa dot.com hawajui hata Empire cinema ilikua wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...