Katibu Mkuu Mstaafu Bw. Vincent Mrisho akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ofisi za Tume leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Jospeh Warioba na kushoto ni Mjumbe wa Tume Prof. Mwesiga Baregu.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Dkt. Khalid Mohamed akiongea katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Katibu Mkuu huyo aliwasilisha maoni ya watumishi wa ofisi yake kuhusu Katiba Mpya.
Mkurugenzi wa Uratibu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Bw. Ahmad Kassim Haji akiongea katika mkutano na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Ofisi hiyo ya ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar iliwasilisha maoni ya watumishi wake kuhusu Katiba Mpya. kwa Tume.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Awadh Said akiongea katika mkutano kati ya Wajumbe wa Tume na ujumbe wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar uliowasilisha maoni ya watumishi wa ofisi hiyo kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...