Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Sio kila kitu wananchi wanasikilizwa. Mfano wananchi hawakusikilizwa walipokataa vyama vingi. UK haikusikiliza wanachi wao kuhusu kujitoa EU. Kuna baadhi ya maamuzi inabidi yafanywa kwa manufaa ya nchi kwa sababu za hali ya kidunia inavyoendelea kwa wakati huo.

    ReplyDelete
  2. hivi serikali yetu kwanini sio sikivu? au wanataka mtwara iwe kama niger delta? wananchi wa mtwara wanayo haki ya kupigania rasilimali ya gesi itumike kujenga gridi mpya ya taifa ianzie mtwara. wamakonde endelezeni mapambano na wala msitishwe na ubabe wa dola katika kupigania haki yenu. na kama noma na iwe maana tumechoka kuonewa na kufanywa watu wa kusini wapumbavu. aluta continua chingas.

    ReplyDelete
  3. Thank you Zitto. U r right on!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. Hii gesi hii itakuja kuleta mambo.

    David V

    ReplyDelete
  5. Haya wenye macho wasikie na wenye masikio waone.Wakati hili vuguvugu linaanza nakumbuka nilishawahi pia kutoa maoni yangu kua mbona naona kama serikali ndio yenye mtazamo wa kutugawa na si wananchi wa kusini?lakini kwa bahati mbaya yale maoni hayakutolewa ktk safu hii ili kufikisha ujumbe kwa umma jinsi ya suala hili lilivyo.Taarifa tunazozisikia kila wakati toka serikalini ni kwamba wananchi wa Mtwara hawataki gesi iende Dar na unapowasikia wananchi wenyewe wa Mtwara wao wanasema Tanzania ni moja na gesi lazima isambazwe kote hapa Tanzania ila mitambo tu ndio ijengwe hapa ili kukuza uchumi wa mkoa. Tuhuma zinazosambazwa za kusema watu wa Mtwara hawataki gesi isafiri si za kweli, na kama walinukuliwa vibaya na hao wanaosema hivyo basi nadhani muda bado upo wa kuweza kusawazisha hizi taarifa ili pale palipoleta utata wa kuelewa hoja za watu wa Mtwara paeleweke na kuepusha migusano isiyo na tija, nasema hivyo kwakua lengo ni moja kuwaendeleza watanzania wote kwa kupitia njia zenye maridhiko ya wote.

    ReplyDelete


  6. Zitto kama umechoka shika jembe kalime hebu usigawe nchi kwa kuchochea ujinga

    ReplyDelete
  7. ZITO NA WAASI WENZAKE NI HATARI KWA USTAWI WA TAIFA INABIDI UFIKIRIE NI HASARA KIASI GANI SERIKALI ITAPATA KWA KUKATISHA MPANGO WAKE.KWA NINI UMESUBIRI MPAKA MCHAKATO UFIKE HAPO NDO UANZE UCHOCHEZI.NAJUA ASILI YAKO NI WABISHI MNO.KWANI DAR SI TANZANIA?WAMTWARA HAWAJAZUILIWA KUJA DAR KUFANYA KAZI.MBONA ULAYA GAS INASAFIRISWA TOKA URUSI HADI UK KUPATA SOKO NA WARUSI HAWAJAANDAMANA.ACHA UCHOCHEZI

    ReplyDelete
  8. ringa na uhuru wa kikwete angekuwa Nyerere angeshakuhifadhi kizuizini

    ReplyDelete
  9. Dirty politics that's what it is. Ana hasara gani kwao kigoma basi sangara waliwe huko huko wasiletwe dar kwa bei kubwa sana. Mbona haulizi kwa nini dagaaa ambalo katika miaka ya sabini ndio kilikuwa mboga kubwa ya wananchi, sasa hata huko inakotoka kwao kigoma wananchi hawawezi kuafford. Very stupid. sasa mtashika dola au federation of states, maana arusha ikijitenga, mtwara na Zanzibar ikifuata, Mwanza nayo itataka kujitenga, after all wasukuma wanaongoza kwa population kubwa, ya why not. Mchele nao mbeya usije dar. Halafu na wenyewe wabaki hukohuko wasije si wanajiatosheleza. Ajabu ni kwamba hata walioenda shule wanapandia hili bandwagon. AIBU AIBU AIBU. GESI INALIWA TANGU LINI. BADO TUKO PORINI KIAKILI NA KIFIKRA.

    ReplyDelete
  10. Sio kila kitu lazima uwasikilize wananchi mh.zitto unakosea...ukiwa kiongozi kila kitu ufanye kwa msukumo wa wananchi mwisho wa siku watakugeuka pia hukutumia akili na mamlaka uliyopewa. kila kitu kiko wazi ni kwamba tuko kwenye emegency crisis ya tatizo la umeme kwa wakati huu na viwanda vilivyomo pamoja na miundombinu iliyoko inahitaji kwanza umeme wa haraka na vyote hivyo viko dar na sio wote unaotumika ni 14% ugomvi uko wapi hapo? mbona wanasiasa mnatuzingua????

    ReplyDelete
  11. Gezi ya Mtwara ikizalisha umeme huko Mtwara badala ya kule Dar es Salaam na njia mpya ya umeme ikajengwa kuusafirisha hadi Dar es Salaam, maeneo yote ya vijijini na mijini kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam yatakuwa yamefaidi kwani yote yatakuwa yamewezeshwa kuwa kivutio kwa uwekezaji hasa kwenye fani ya kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa kisasa maeneo ya vijijini. Umuhimu wa power grid badala ya gas grid umeelezewa zaidi kwenye link hii: http://db.tt/S6eMcAr3.
    Kikwazo kikubwa kwenye ujenzi wa hili bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni kwamba bado hatujajua ni maeneo yapi yenye gesi na ni yapi hayana kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam hadi Tanga hadi mpaka wetu na Kenya kwa hiyo inawezekana kabisa tukawa tunajenga bomba kwa gharama kubwa ili kusafirisha gesi kutoka pointi moja yenye kidogo sana kwenda pointi nyingine yenye gesi yake nyingi zaidi, inayotosheleza na kubaki.
    Ujenzi wa mabomba kwa ajili ya usafirishaji wa gesi nyingi umbali mkubwa ndani ya nchi yetu ni muhimu ukawa na udhibitisho kwamba hatutoi pointi hii kupeleka pointi ile yenye gesi yake nyingi inayotosheleza na kubaki. Lakini hili halitakuwa tatizo iwapo gridi ya umeme badala ya gridi ya gesi itajengwa kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
    Gridi ya umeme utokanao na gesi asilia ikiwepo kati ya Mtwara na Dar es Salaam itakuwa kianzio kipya na itakuwa ni boresho la uhakika wa sekta ya umeme ya taifa na kwa vile inaanzia karibu sana na machimbo makubwa ya gesi huko Msumbiji basi itakuwa rahisi kuunganisha grid ya Msumbiji na ya Tanzania itakapobidi hapo baadaye.
    Mikoa ya kusini ndiyo iliyobaki bila kuunganishwa na grid ya taifa kwa muda mrefu kutokana na kutokuwa na kianzio cha umeme kinachofaa lakini kwa vile kianzio kizuri cha gesi asilia sasa kimmepatikana basi umeme wa gesi uzalishwe huko Mtwara na grid ya umeme ijengwe kutoka Mtwara hadi Dar ili kuwezesha pia mikoa ya kusini kuunganishwa na gridi ya taifa. Ni vizuri ikazingatiwa kuwa umeme utokanao na gesi asilia unakuwa wa faida zaidi unapozalishwa na kutumika karibu zaidi na machimbo ya gesi.
    Gharama ya ujenzi wa gridi ya umeme ni karibu mara mbili ya gharama ya ujenzi wa bomba la gesi lakini ni kidogo sana ukilinganisha na uwingi na ukubwa wa faida zitakazotokana na kuwepo gridi ya umeme kati ya Mtwara na Dar es Salaam ambazo ni zaidi ya zitakazopatikana kutokana na kuwepo bomba la gesi kati ya Mtwara na Dar es Salaam kwa kipindi chote cha uhai wa mradi. Ukweli ni kwamba hata kama bomba lingekuwa tayari liko ardhini, bado ingekuwa faida kubwa zaidi kuliacha huko ardhini na umeme na bidhaa nyingine kutokana na gesi asilia ya Mtwara zikazalishwa huko Mtwara na grid mpya ya umeme ikajengwa kusafirisha hadi Dar es Salaam. Mabonde makubwa na mazuri mno kwa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kama bonde la mto Ruvu na bonde la mto Rufiji bado hayaendelezwi hasa kutokana na kukosekana kwa umeme wa uhakika.
    Kwa hiyo nakubaliana na Mh Zitto kwa hili na ni muhimu wanasiasa wakawa pamoja kwenye hili, wakakaa pembeni na kuwaachia wataalamu husika wakanya upembuzi yakinifu kuhusu manufaa ya umeme utokanao na gesi ya Mtwara ukazalishwa huko huko Mtwara badala ya Dar es Salaam na kusafirishwa kwa gridi mpya ya umeme hadi Dar eslaam.

    ReplyDelete
  12. ni kweli kbsaaa thats point zitto wawe wanaweka muda wakuwasikiliza wananchi na kujua matatizo yao.



    meggie impostra.

    ReplyDelete
  13. Simbachamwene anasema ili gesi isafirishwe nje inabidi bomba lijengwe kupeleka gesi Dar. Kwani hiyo gesi haiwezi kusafirishwa kutoka Mtwara ambapo napo kuna bandari? Kipi kitakuwa ni rahisi kwa nchi, gesi kusafiriswha kutoka Dar au Mtwara? Ni kwa nini viwanda visijengwe Mtwara? Tunajua mshajipangia percentage zenu ndio maana mnakazania kujenga hilo bomba, lakini hii sio miaka ya 90.

    ReplyDelete
  14. nilimsikia Naibu Waziri mmoja leo asubuhi anadai kwamba kiuchumi,ni gharama zaidi kusafirisha umeme wa gesi kutoka Mtwara hadi Dsm kwa njia ya nyaya(umeme ukifuliwa au kuzalishwa palepale Mtwara),kuliko kusafirisha gesighafi kwa mabomba kisha ikafuliwe Dsm!nilibaki mdomo wazi,nikajiuliza,"Hizi ni Economics za wapi za huyu ndugu yetu?"au ndio zilezile za "Online!".Hivi,nani atakaye kuwa analinda hilo bomba la gesi umbali wote huo toka Mtwara hadi Dsm?Na gharama ya ulinzi huo,ammbao utachukua zaidi ya miaka 50,utagharimu shilingi ngapi?je,waziri,hesabu hiyo keshaipiga?Na ,vipi, mikopo iliyotajwa na Mh.Zitto,ikopwe na serikali kimya kimya "bila ya kibali na ridhaa ya Bunge let?".Wamewaona wenzao wa Marekani,pamoja na Ukubwa wote na Utajiri wote na Manguvu yote walionayo,"bado serikali lazima iombe kibali cha Bunge/Congress ili iweze kukopa zaidi,iwapo imeshavuka "Debt Ceiling","Ukomo wa Kukopa ulioidhinishwa NA Bunge"!Hapa kwetu vipi? Viongozi wamejisahau,wanadhani,wanaendesha Makampuni Binafsi?.Soma East African la leo(wiki hii).Kabla,serikali haijafikiria kwenda kukopa IMF au World Bank,wanatakiwa kuomba idhini na kibali cha Bunge letu!Idhini hiyo haitolewi na Benki ya Dunia wala IMF! Tanzania sio Koloni la IMF na Benki ya Dunia.Labda tuambiwe sasa na serikali tutambue!Otherwise,this is messing around with our economy!Viongozi wapo miaka mitano Kumi,wameondoka!Nani atakayelipa mikopo hiyo,ikichukuliwa kiholela?Hatukatai kukopa,lakini,kwanini zitumike "njia za panya?".Kimyakimya bila ridhaa ya Bunge?No,tunahitaji maelezo!

    ReplyDelete
  15. KWA WANAHARAKATI WA GESI:

    Mdau Anony wa Sun Jan 20, 09:59:00 pm 2013

    MUWE MNATOA MAONI NA KUZINGATIA SABABU ZA KIUCHUMI NA KIUEDNESHAJI.

    NINA WASIWASI KWA JINSI YA UTOAJI WENU MAONI NA MISIMAMO YANU NI WAZI HAMNA UELEWA WA KIUCHUMI BALI MNA MSUKUMO WA KISIASA NA KUWA HAMPO KISAYANSI BALI MPO KISIASA!

    1.GAS INATOKA KATIKA FACTORS OF PRODUCTION AMBAYO NI LAND (ARDHI) AU MIAMBA MABAYO IPO KWENYE ARDHI.

    2.GAS HAIPO NJE YA ARDHI NA KUOKOTWA KAMA KITU CHA KUOKOTA, GAS INATAFUTWA ,WAKATI UTAFUTAJI WAKE UNAGHARIMU MABILIONI YA DOLA ZA MAREKANI (US $$$ BILLIONS)FEDHA AMBAZO SERIKALI IMETUMIA KUITAFUTA GAS HADI INAPATIKANA HAZIKUTOKA MKOA WA MTWARA PEKE YAKE ZIMETOKA KATIKA MAPATO YA RASILIMALI ZINGINE AMBAZO ZIPO MIKOA MINGINE KAMA KAHAWA, ALMASI,DHAHABU,MALI ASILI,TANZANITE,NA MALI ZINGINE NYINGI KUTOKA MIKOA MINGINE.

    3.KATIKA SUALA LA RESOURCE (RASILIMALI) KAMA ILIVYO GAS, ITIFAKI ZA KIUCHUMI NI LAZIMA ZIZINGATIWE KWA KUWA PANA VITU VITATU (i)Exploration,(ii)Production (iii)Trading, HIVYO ILI MPANGO UWE NA TIJA NI LAZIMA KANUNI ZA KIBIASHARA NA KIUCHUMI ZIZINGATIWE, KAMA MALI IMEPATIKANA NI LAZIMA IUZWE AU IENDEHSWE KWA TIJA KAMA TUNAVYOONA YA KUWA INAANZIA (1)EXPLORATION ,HALAFU (2)PRODUCTION NA (3) TRADING.

    KAMA WANANCHI WA MTWARA MNATAKA KUNUFAIKA NA GAS MTAHITAJIKA KUYAFIKIA MASOKO YA HISA DAR ES SALAAM (DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE-DSE) AMBAKO HISA ZITATOLEWA KARIBUNI ILI WANANCHI WAWEKEZE.

    4.MNATAKIWA MZINGATIE SABABU ZA KIUCHUMI ZA GAS KULETWA DAR ES SALAAMA KWANZA KABLA MITAMBO YA KUICHAMBUA NA KUZALISHA BIDHAA NA AJIRA HAIJAKAMILIKA HUKO MTWARA, HIVYO GAS INAKUJA DAR ES SALAAM KWA SABABU ZA KIUCHUMI KWA KUWA KWA SASA MTAWARA HAKUNA VIWANDA VYA KUTOSHA AMBAVYO BIASHARA ITALIPA VITAKAVYOTUMIA GAS NA PIA, SERIKALI KAIJAJENGA VIWANDA VYA KU PROCESS GAS NA KUZALISHA BIDHAA TOFAUTI HUKU IKIZALISHA AJIRA...HIVYO KWA SASA HAKUNA JINSI GAS ILI IWE NA TIJA NI LAZIMA ILETWE DAR ES SALAAM...ZINGATIENI BIASHARA NA UCHUMI KWANZA KULIKO SIASA.

    5.MHE. WAZIRI PROF. SOSPETER MUHONGO ALITOA TAARIFA KWA UMMA /PRESS RELEASE AMBAYO IMEFAFANUA VIZURI SANA YA KUWA ASILIMIA 14.3% YA GAS NDIO IPO MKOANI MTWARA, HUKU 7.1% IKIWA LINDI NA INGINE 3.7% IKIWA MAENEO MENGINE NCHINI HUKU KIASI KIKUBWA ZAIDI 74.9% IPO BAHARINI AMBAKO KWA MIPAKA YA TAWALA ZA MIKOA SIO SEHEMU YA MTWARA LAKINI NI SEHEMU YA TANZANIA.

    MKUMBUKE YA KUWA TUNA ENEO LA ZIADA LA BAHARI AMBALO UMOJA WA MATAIFA (UN) IMETUPATIA EEZ (EXTRA ECONOMIC ZONE) YAANI KILOMETA ZA ZIADA KUELEKEA BAHARINI AMBALO SIO SEHEMU YA MKOA WOWOTE ULE ILHALI LIKIWA KATIKA SHERIA ZA KIMATAIFA LINATAMBULIKA KAMA SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA...NDIYO SEHEMU YENYE KIASI KIKUBWA CHA GAS CHA 74.9% HIVYO MTWARA WANALETA SIASA KUDAI GAS HIYO (YOTE) PEKE YAO WAKATI IKIWA NI MALI YA WATU WA MIKOA YOTE YA TANZANIA YAANI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IKIJUMUISHA NA VISIWANI.

    HIVYO WANAHARAKATI WA GAS KUNUFAISHA MKOA WA MTWARA PEKE YAKE MZINGATIE HOJA HIZO 5 HAPO JUU.

    ReplyDelete
  16. Sasa nimepata majibu kwanini hawa "Vigogo!"hawataki kuhamia Dodoma!Dsm ni kila kitu brother!Wajinga Ndio Waliawao!au sio Kaka?Ipo siku.....kachumbari itageuka kuwa mboga!The super powers,The Pioneers of Democracy and Liberty,Our Own Colonisers,the UK,the USA,Japan,Italy,Germany,etc etc,"Ikiwa wao Vyama Vikuu vya Siasa Vinabadilishana Madaraka ya Kutawala au Kuongoza Nchi kupitia Chaguzi Kuu mbalimbali!",kila wapiga kura wao wanapo ona ipo haja na lazima kufanya mabadiliko ya Uongozi ili kuleta Tija na Ufanisi katika uendeshaji wa serikali,ili kuboresha maisha yao,ITAKUWA SISI TANZANIA?who are we to defy and resist Global Wave of CHANGE? msijidanganye ndugu zangu ,bila kuchapa kazi,kuacha ufisadi,kutokomeza rushwa,hamna chenu,wakati unasema ukweli!2015 sio mbali.Dawa ni kubadilika tu,tena kubadilika haraka sana!

    ReplyDelete
  17. Huyu Zito ingawa ni mwanaharakati lakini tuwe waangalifu anavyotumia jukwaa la kisiasa. Nimesikiliza vizuri interview ya naibu waziri wa nishati kwenye TV. Ni kwamba Zito Kwabwe alikuwepo wakati maamuzi muhimu ya huu mradi yakiwa yanafanywa (a) kwenye bunge na (b) kwenye kamati ambazo yeye anahusika.

    Sasa kama yeye ana nia njema ni kwa nini hakutoa hizi hoja siku nyingi hapo awali? Ni kwanini asubiri wananchi wa Mtwara (ambao inabidi waelimishwe) waanze maandamano halafu na yeye ajiunge kwenye kutetea hii hoja? Ni kwa nini asubiri mradi unapoanza ndio alalamike? Kwa hili ninashuku DHAMIRA ya Zito Kabwe. Narudia nashuku DHAMIRA yake na si HOJA zake ambazo zinaweza kuwa na nguvu....

    ReplyDelete
  18. Hakuna kitakachoharibika hapa Tanzania!

    Sisi sio Kenya, watu wana busara hatuwezi kukalia kuti kavu kama jirani zetu.

    ReplyDelete
  19. Zitto Kabwe wakati taratibu za awali za Mradi huu zikipangwa yeye alikuwa katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

    Hivyo asilete za kuleta akaanza Siasa za Ukigeu geu wake, awe na msimamo na sio kuwa na msimamo wa Siasa wa 'Karata tatu'

    Yeye isitoshe ni Mwanauchumi mzuri na katika uchumu pana masuala ya 1.Available resources, 2.Unlimited needs, 3.Priority choices regarding 1 and 2 above.

    Hivyo maamuzi sahihi kama Gas kusafirishwa Dar ama kubakia Mtwara yatazingatia kanuni za kiuchumi kama hapo juu No.1,No.2 na No.3 zinavyoainishwa.

    ReplyDelete
  20. kusuka au kunyoa!mkataba uko wapi?siri ya nani?

    ReplyDelete
  21. buree chitaki!kunchika bomba,chumuni!kuchika nchanga,chilingi!samaki nchanga mpe Palanchinchi!mi chiwezi kumung'unya wala chitemi!chimama apoapo njomba,nichikupige nchale wa chingo!we,kamata bomba tu njomba,utamu wake utanchikia tu,chipige kelele!(with love from mtwara)!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...