Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na ujumbe wa watu wa Misri ulioongozwa na Waziri wa Maji wa nchi hiyo Dk.Mohamed Saad (kushoto) walipofika ofisini kwake kwaajili ya mazungumzo mbalimbali kuhusu sekta ya maji na umwagiliaji hassa suala la maji ya mto Nile ambayo chanzo chake ni ziwa Victoria. Magembe aliwataka kuimarisha Ushirikiano wa nchi hizo kwenye mambo yote wanayokubaliana na kwayale wasiokubaliana kuendelea na majadiliano.
Waziri wa Maji wa Misri  Mohamed Saad (katikati) akizungumza na watendaji wa Wizara ya Maji nchini kulia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof.Jumanne Maghembe kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Bilinith Mahenge.
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania wakinukuu mambo mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na ujumbe wa Wizara ya maji ya nchini Misri jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Misri nchini Tanzania,Hossam Moharam (kushoto) akiwa sambamba ujumbe wa nchi yake uliofika nchini kwa majadiliano ya mambo mbalimbali ya sekta ya maji.
Ujumbe wa Wizara ya Maji ya nchini Misri ukifuatilia majadiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...