Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013. Kiongozi huyo amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Matarumbeta ya Mzee Hozza ndani
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kimya kingi chaleta Mshindo!

    Mhe.Raisi Joseph Kabila, ameona atupitie Tanzania ndugu zake wa siku nyingi ingawa huko kwao anasemwa sana kuhusiana na ukaribu na udugu wake kwetu!

    Wakongomani hamkumbuki ya kuwa tumekuwa naye hapa nchini kipindi cha nyuma?

    Wakongomani hamkumbuki ya kuwa tumekaa na wengi wakiwemo akina Thabo Mbeki na Walter Sisulu(AFRIKA KUSINI),Dos Santos (ANGOLA) na Augustinho Netto, Museveni,Obote(UGANDA),Mengistu Haile Mariam (ETHIOPIA),Samora Machel na Eduado Mondlane na Joaquiim Chissano (MSUMBIJI), Sam Nujoma na Hikipfunye Pohamba(NAMIBIA)

    ReplyDelete
  2. Kaka, Kaka, Kaka, Kaka!

    Karibu sana Mhe.Raisi Kabila!

    ReplyDelete
  3. Karibu sana Mhe. Raisi Brother Joseph Kabila !

    Du za kitambo?

    Vipi jamaa kule Msituni umemalizana nao?

    Karibu sana tupo tayari kukusimamia kwa lolote ndugu yetu!

    ReplyDelete
  4. nampenda sana huyu rais blazamen kabila anapiga pamba vizuri na anajuwa kutumia madaraka vyema

    nimependa sana usafiri wake wa maana na sio tudege twetu tudogo tudogo na bado wananchi wamelalamika sana

    karibu sana mwanajeshi wetu kabila sio mbaya ukitembelea jeshi letu ambalo ulisoma hapo siku za nyuma na ile shule uliyesoma

    kabila ni mwenzetu na hapa ni nyumbani kwao karibu sana kaka

    ReplyDelete
  5. Sasa hao M23 umeshamalizana nao au? Sasa wale wanawake wanaobakwa ovyo itakuwaje? Ublazamen sio dili bro dili ni amani

    ReplyDelete
  6. Hiyo ndege aliinunua marehemu Mobutu, mzee wa luxury, akakimbia nayo Morroco lakini serikali ikairudisha DRC kwa nguvu. Kabila na baba yake waliirithi na Joseph akiondoka mwingine atairithi. Mobutu alifanya mambo mengine ya maana.

    ReplyDelete
  7. Mtoa Maoni wa kwanza, alikwepo Mwanaharakati mwingine Hayati Walter Rodney wa (GUYANA) naye aliishi Dar Es Salaam-Tanzania miaka hiyo ya harakati akiwa na wenzake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...