Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na jopo la APRM kuhusu Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Mhe. Rais alitoa ufafanuzi huo mbele ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mhe. Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda nao walihudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU ambapo Tanzania iliwasilisha ripoti yake kuhusu Demokrasia na Utawala Bora.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania. Wengine katika picha ni Waziri Bernard K. Membe (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwemo pia wajumbe na Wabunge waliofuatana na Mhe. Rais Kikwete kuhudhuria Mkutano huo.
Mhe. Rais Kikwete (kushoto) akibadilishana mawazo na Mhe. Salum Barwany, Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini nje ya ukumbi wa mkutano nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana nao nchini Ethiopia ambao unajumuisha Mawaziri, Wabunge na Timu ya APRM, Tanzania.
Picha na Ally Kondo, Addis Ababa
Picha na Ally Kondo, Addis Ababa
Jee tujiulize Wazanzibari ni wangapi katika hilo kundi alilofuatana nalo mheshimiwa Rais. Tunajuwa kwamba maoni kama haya Bwana michuzi kwa ukereketwa wake mara nyingi tunapoyaweka anayapigilia mwenyewe tuu na anashindwa kuyaweka hadharani na wadau wengine wakapata kuyaona.any way tunafahamu kwamba tunapoongelea muungano inakuuma sana Bwana michuzi lakini tutafanyajeee na ndio hali halisi inabidi ukubali matokeo tuu ndugu yangu.
ReplyDeleteShibuda ni mzanzibari
ReplyDeleteKatika hili, tutezame uwiano wa idadi ya watu Zanzibar na Tanyanyika. Isiwe kwamba tunajitizama kama Nchi Mbili hivyo kila litendekalo kuwe na uwiano wa watu au mgawo. Hilo halikubaliki.
ReplyDeleteLa! Ningetegemea uwepo wa wanawake 51% katika hili jopo na si linavyo onekana sasa.
Tuweke vigezo mahsusi katika madai yetu
swala sio wazanzibari wangapi..hao waliokwenda wanatuwakilishaje? anyway kwenye hii picha nilioweza kuwatambua ni Mh. Ramadhan Shaaban (next to Mh Shibuba), Mh. Rajab Baraka (wa tatu kulia mstari wa mbele) na Nd. Said (wa tatu kulia mst wa nyuma)
ReplyDeleteNi mara ngapi Rais wa Zanzibar anakwenda nje na troupe yake je ni wa-bara wangapi huwa anawachukua? sio unaropoka ropoka tu angalia na upande unaoulizia pia.
ReplyDeleteWewe Mtoa Maoni wa kwanza anony Sun Jan 27, 08:42:00 pm 2013
ReplyDelete..Ninyi huko Zanzibari idadi yenu ji wawili (2) na sisi huku bara tuko Laki moja (100,000) sasa kwa akili yako unataka uwakilishi wetu uwe 50 kwa 50 ?
Kama itakuwa hivyo wanatakiwa watu 100 kutuwakilisha Bara(50) na Zanzibar(50) sawa kwa sawa sisi tutatosheleza watu 50 kutoka idadi yetu ya watu 100,000 wakabaki watu 99,050 je wewe watu wengine (48) utawatoa wapi?, uta kunya wapi watu wengine 48?, wakati nchi nzima mpo wawili(2) tu?
Au ninyi Zanzibar mtaongeza kuwakilishwa na watu wengine (-48)?
Yaani 2-50=-48 ?
Elimu na Akili Zanzibar ni tatizo!
Sun Jan 27, 08:42:00 pm 2013
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Nini Zanzibar wengi wenu akili zenu finyu kama wewe!
Wapo Wazanzibar ambao akili zao ni nzuri mfano watu hawa:
1.Mhe.Maali Seif Hamad
2.Mhe.Dr.Gharib Bilal
3.Mhe.Aboud
4.Mhe.Dr.Shein
5.Mhe.Naibu Waziri wa Fedha (Muungano)
MADAI YAKO KUHUSU IDADI YA WALIOFUATANA NA MHE. RAISI KWENYE SAFARI NI FINYU, WALA HAYANA TIJA WALA MSHIKO, KAMA KUNGEKUWA NA HITILAFU WATU HAO WATANO (5) WA ZANZIBAR WENYE AKILI SAAANA KULIKO WEWE WANGELIONA HILO NA KUSAHIHISHA NA SIO WEWE MJINGA!
acheni blaa blaaa jamani, znz ni 2.2% ya bara so uwiano gani hapo? utajikuta km wanaenda watu 15 na raisi znz inatakiwa aende robo mtu, so unamfuta tuu. Wananwake iwe 51% ili iweje? tuache matatizo haya ya balance balance acheni nature ichukue mkondo wake tafadhali
ReplyDeleteWache mambo ya ubaguzi, Raisi alikwenda kama Raisi wa tanzania na anawakilisha tanzania/ sasa mambo ya kuwa waznz wangapi na watanganyika wangapi mambo ya kijinga na akili finyu mwisho utasema walikwenda waislamu wangapi au wakiristu wangapi ? na pia mtaendelaa kusema wapenba wangapi au wahaya wangapi wamekwenda safari..tufikiriane kujenga tanzania na maendeleo yaje kwa namna gani wakati ulaya wanaendelea kuungana sio tutaka kujitenga kwa mambo ya sio na msingi je jiuulize viongozi walioteuliwa znz kwa hajue wajibu wao ...
ReplyDeletena hao wanawake 51% na wazanzibari whatever % mnaowazungumzia, wanaqualify kwenda ktk kutuwakilisha ktk mada husika? Kama mada ipo popular miongoni mwa wahindi tu, then usishangae uwakilishi ukawa ni watanzania wenye asili ya kihindi tu, usiulize why mweusi hakwenda, jibu ni kwamba, mweusi hayupo competent na mada husika..thats just a simple example kwako mzanzibari mwenzangu hapo juu
ReplyDeleteKwanza nashukuru sana Bwana Michuzi kwa kuweka maoni yangu hadharani na wadau kuweza kuyasoma.Moja kwanza napenda kuwajuilisha hawa wadau ambao wengine wameweza kuniita mjinga na mengineyo kwa kuuliza ni Wazanzibari wangapi ambao wamefuatana na mheshimiwa Rais.Any way ningepeda kama kunauwezekano ningeweza kwanza nikakutana nao hawa watu ili nikaweza kuwapatia kolifikeshen zangu na wao wakanionesha za kwao tukaweza kukompea nani mjinga.Ninapozungumza kolifikehsen sio za mlimani tunazungumza LONDON UNIVASITI,na univasiti nyenginezo ulimwenguni.Pili tunapozungumzia nchi tukumbuke kwamba haimati wala haihusiani Wazanzibari ni wangapi wala nchi yao inaukubwa gani.Tunazungumzia nchi mbili zenye mamlaka sawa sawa na kama hawa watu watakuwa wamesoma kidogo tuu basi pia wangekumbuka kwamba Baba wa Taifa la Tanganyika ndie aliekuja na kumtaka Baba wa Taifa la Zanzibar Mh.ABEID.AMANI.KARUME.kumtaka waunde muungano.Halafu wanaozungumza ukubwa na udogo wa nchi mimi naona watu akili zao ni ndogo .Nitatoa mfano mimi binafsi Bwana MICHUZI nimewahi kufanya kazi katika nchi moja hivi karibuni ambayo inaitwa MALTA,hii nchi ni ndogo kuliko ZANZIBAR lakini imo kwenye EUROPEAN UNION na inaheshimika kama nchi nyengine yeyote ya Europe kwa hiyo hawa watu wanaozungumza ukubwa na udogo wa nchi Waengereza kwa lugha ya rahisi husema they just talking CRAP. Na kunawengine wametaja watu wenye akili kama vile mheshimiwa Gharib Bilai na wengineo, mimi nahisi ningekuomba Bwana Michuzi hawa watu ungewaekea kidogo maoni ya katiba mpya ambayo yametolewa na Mh.Amani.Karume. Mh.Seif.Shariff. Mh.Mzee.Moyo.Mh.Bora.Afya. na wengine wengineo ,Jeehawakuzungumzia suala la uwiyano kati ya Zanzibar na Tanganyika,Jee na wao pia hawana akili kama mimi ,kuna mpuuzi mmoja nae pia amezungumza jee Risi wa Zanzibar anapokwenda nje ya nchi anafuatana na Watanganyika wangapi,jibu la mjinga kama huyu ni rahisi tuu kwa sababu inaonekana wazi hakusoma,jee mmesahau kwamba anapigiwa kura na Wazanzibari na sio Watanzania,na anawakilisha Zanzibar na sio Tanzania nyinyi Utanganyika mliukataa na ndio maana CHADEMA wanadai serikali yao ya TANGANYIKA irejeshwa.Any way nina points nyingi tu za kuwaandikia nikawasaidia elimu kidogo lakini mda mdogo nakutakieni kila la kheri.
ReplyDeleteMzanzibari anonymous wa 11 Pointi zako ni pumba hata Kiingereza chenyewe hujui pamoja na kudai kuwa umesomea Uingereza!
ReplyDelete..kolifikehsen=QUALIFICATION...
Kwa nini usiandike kwa Kiingereza kama hapo kwenye CAPITAL LETTERS?
Mtoa Maoni wa 11 wa Zanzibar anon wa Tue Jan 29, 01:08:00 am 2013
ReplyDeleteLeo ndio nimeshuhudia ya kuwa
1.Unaweza ukadai kuwa umesoma lakini usielimike!
2.Kiingereza sio kugezo cha kuelimika!
3.Wengi wanaojiita wamesoma pia Kiingereza chao ni kibovu kama wewe!
Pamoja na kikaa kwako Uingereza bado Kiingereza chako kibovu nina wasiwasi hata huko UK unabeba Maboksi ama Unalea wazee na Mataahira!
Hata kama unadai umesoma labda Umehitimu kutoka Vyuo vya Elimu ya Kiwango cha chini vya Wahindi wa UK.
Au inawezekana Shahada zako umenunua pale London kwa Wasanii wa Ki-Nigeria!
Mdau unaedai huyo mtu hakusoma kwa sababu hakuandika kolifikeshen kama unavyotaka wewe kwa lugha ya kiigereza ni mpuuzi nahisi kama wewe nndio hukusoma kwa sababu kumbuka lugha inayozungumzwa hapo ni KISWAHILI na sio ENGLISH alivyandika mdau sawa sawa wewe ndio unamatatizo ya akili.
ReplyDelete"You have the right to criticize, but do you have the heart to help" ...Abe Lincoln
ReplyDelete...poor souls, hivi hamuwezi kutoa hoja bila kuumbuana?!
Mie ni Mtanzania toka bara, lakini namuunga mkono jamaa Anonymous wa kwanza. Kwanza ni haki yake kutoa mawazo yake. Kwa sababu asiposema hatuwezi kujua kuwa hawa Wanzazibari au popote pale watu wana mawazo yapi au kitu fulani kibadilike au hapana. Pili, mtu yoyote yule ambaye anaekimbilia matusi au kumdharau mtu mwingine anaonyesha ameshindwa hoja au ni wale vibaraka, kazi yao ni kubisha kila kitu maana kuna faida fulani wanapata kuwakandamiza wenzao. Tatu, jamaa wote wanaosema eti hajaandika kiingereza sahihi, sidhani hapa, Michuzi, ni sehemu ya kupima elimu lugha ya mtu, kwani wote tunaandika bila kurudia kusoma tuliyoandika. Watanzania naomba tuwe na hekima, siyo kila kitu tunapinga kwa matusi. kwa mtindo huu tutafika lakini taratibu sana.
ReplyDelete