Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
 Gari iliyomchukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikiondoka Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi aliloandaliwa kwa heshima yake mjini Paris Ufaransa leo Januari 21, 2013 ikiashiria kuanza rasmi kwa ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akiwa katika maongezi rasmi na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa na ujumbe wake  katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakiongea na wanahabari baada ya mazungumzo yao rasmi katika Ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Champs L'Elyesee (hutamkwa chanz elezee) jijini Paris leo Januari 21, 2013.PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wanatumia Lugha gani hawa kuwasiliana?(Wengi mtakimbilia Kiingereza,lakini je ni sahihi?)Wafaransa huwa hawataki kusikia lugha nyingine masikioni mwao zaidi ya Kifaransa.Nadhani kuna haja ya Rais wetu kuwa anatumia KISWAHILI(Lugha inayozungumzwa na wengi Tanzania) anapokuwa sehemu ambako Kiswahili hakitumiki,watafutwe wakalimani.Ndivyo wanavyofanya Wachina,Warusi,n.k.Tutangaze lugha yetu.

    Kwa wanaofuatilia AFCON2013 kule Afrika ya kusini,niwape Clip hii..Rais wa Cape Verde amemwagiza kocha wa Timu ya mpira wa miguu inayoshiriki michuano hii kutumia lugha ya nchi yake(Kireno) kila anapohojiwa na Media.Sababu-Raia wa Cape Verde wanahitaji kufahamu anachozungumza kocha wao,mataifa mengine yasiyofahamu Kireno ndiyo yapate tabu ya kufahamu anachoongea,siyo tena raia wa Cape Verde waanze kuhangaika kufahamu kocha wao alichozungumza kama atatumia lugha tofauti na Kireno(Lugha inayozungumzwa na wengi nchini humo).

    David V

    ReplyDelete
  2. nachokupendea raisi wangu unapiga suti za uhakika.. piga panga JK

    ReplyDelete
  3. David V
    Kwa taarifa tu, huku nje kiswahili kinajulikana ni lugha iliyoanzia Kenya! hawajui kama kuna nchi inayoitwa Tanzania inaongea kiswahili. Naomba tu nikufahamishe hili kama unataka lugha yetu itangazike tunatakiwa pia tukijue sana kiingereza ili tuweze kuitangaza....huwezi kutangaza kiswahili wakati english hujui au english yetu ina overdose ya kiswahili, lazima ujue kiingereza zaidi kuweza kutangaza kiswahili kwani hata kufanya application ya kazi ya kutafsiri kiswahili inahitaji ujuzi katika kujua lugha ya kiingereza...hapo ndipo tuliposhindwa na wakenya! Nina uhakika na ninachosema kwa sababu mimi ni mwalimu huku midwest na hayo ndiyo nayoshuhudia kila siku katika maisha yangu ya kazi. LAZIMA WATANZANIA WAJUE KIINGEREZA SANA ILI TUWEZE KUTANGAZA KISWAHILI VIZURI, zaidi ya hapo tutaendelea kujidanganya tu, pia kiingereza bado ni option nzuri sana kwani kazi zote zinahitajika english as first language...hukuliona hilo Bw. David V au bado una imani na hao viongozi wanaotuambia kuwa hadi chuo kikuu mjifunze kiswahili lakini watoto wao wana access ya kwenda shule za nje au internship, au hata home schooling za english. Tafakari hilo.

    ReplyDelete
  4. Che GuevaraJanuary 22, 2013

    Wazungu wakitaka kitu kwako WATAMSIFIA HADI MAMA YAKO MZAZI JAPO HAWAMFAHAMU!

    ReplyDelete
  5. We anony wa 02:28:00 umetoa ukweli na hali halisi. Wengi tunadhani kukitangaza kiswahili ni kukiongea tu popote hata pasipowezekana lakini hilo si kweli. Tunahitaji kujua lugha nyingi za kigeni,Kiingereza hatujui, kiswahili chenyewe wengi wetu hatukijui vema tunaongeaongea tu alimradi.

    Kuhusu hilo agizo la rais wa Cape VErde bado mie naona kuna tatizo kwani Kireno ni lugha ya asili ya waCape Verde? Hawana lugha yao?

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Tue Jan 22, 02:28:00 am 2013 Unajua maana ya 'English as a first language''?

    Maana yake ni lugha ya Mama sasa mtanzania aliyezaliwa na kukulia Tanzania hata aisome Ki-Ingereza kiwango cha PhD (English language and literature) baado hawezi kumfikia mtu wa 'English as a first' language atakuwa ni 'gwiji' wa lugha ya Kiingereza tu.

    Hivyo lugha ya kigeni yaani Kiingereza tuisome kama kama somo na kuielewa vizuri itusaidie ktk masuala mbalimbali lakini 'lugha yetu mama' tuliyozaliwa nayo pia tuimudu kama 'Kiswahili as a first languge'

    Mdau
    Gwiji wa lugha ya kigeni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...