Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini humo.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Begum Taj na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Marcel Escure
wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, tayari kuanza ziara ya yake ya kiserikali ya siku tatu.
Mama Salma Kikwete akionega na mke wa Rais wa Mali,Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
PICHA NA IKULU
Mama Mali na Tz jee communication inakwenda hapo?
ReplyDeleteAnglais and Francais!
Wakoloni weupe wamechanganyikiwa sana hawa siku hizi njaa imewazidi katika nchi zao kwa hiyo ni lazima tuwaangalie sana na kwa umakini Wafaransa wameanza wenyewe kuingilia mambo ya MALI na walifikiria watapata sapoti kutoka kwa wazungu wenzao kama vile Mwengerezalakini ubaya zaidi mwengereza kamuambia nimechoka na vita visivyo na mpango kama unahitaji msaada basi nitakusaidia ndege mbili za mizigo basi sasa kaona aanze kuelekea AFRICA nchi kama vile Tanzania anaweza kupata msaada wa majeshi japo alfu moja ili aweze kujastifai uharamia wake na njaa yake ndio iliomtuma hivyo kwa sababu MALI kuna gesi na Mafuta hizo ndio tamaa zao za kijinga kwa hiyo mimi nasema huu Mualiko wa Rais ni lazima tuwe becarefull hawana heri hawa mutakuja kuniambia siku moja maneno yako ni kweli.
ReplyDelete