Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza katika mshindano hayo Nahodha Fundi Abuubakar kutoka Bumbwini.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.
 Ngarawa mbili za mbele zikichuana vikali katika mashindano yalio fanyika huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 
 Naibu Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Haji Mwadini Makame akipuliza filimbi kuonyesha ishara ya kuanza kwa mashindano hayo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Wananchi wakishangiria jinsi mpambano ulivyokuwa mkali huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Ngarawa zikianza mashindano mara tu ilipopulizwa firimbi ya kuanza mashindano hayo huko forodha mchanga ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mwandishi unapotosha kiswahili, bora uache kazi. Sio 'ngarawa" ni "ngalawa" na sio "firimbi" ni "filimbi"..........umetoka musoma nini?

    ReplyDelete
  2. ZFA na TFF Mashirikisho ya a Soka Bara na Visiwani, nadhani tusizidi kupoteza muda kwa Mpira wa miguu ni vile hatuna chetu.

    Kwa nini tusibadili mwelekeo wetu na kuhamia kwenye hizi Resi na mbio za ngalawa?

    ReplyDelete
  3. HOPE is coming back in Zanzibar,GodBless!

    ReplyDelete
  4. mdau wa kwanza toka hapa kiswahili gani unacholeta hapa? Ngarawa na firimbi ndio lugha sahihi kiswahili chako cha kibara kaa nacho huko huko

    ReplyDelete
  5. Ni Ngarawa, na ni firimbi ndio asili yake maneno.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa Kwanza unatokea Burundi nini? aliyeandika Ngarawa na Firimbi hajakosea hata kidogo kwani ndio kiswahili fasaha,na wala sio Ngalawa na Filimbi rudi shule kajifunze lugha ya Kiswahili.
    mdau wa Pwani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...