MAREHEMU MWL. RUTH MOLLEL BIDUGA 

Familia ya Bwana Hilary J. Biduga waMikocheni , Dar es Salaam , inapenda kuwakumbusha ndugu, jamaa na marafiki kufika kwenye arobaini ya Marehemu Mwl. Ruth Mollel Biduga itakayo fanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 19 Januari, 2013 kuanzia saa tano asubuhi nyumbani kwa marehemu Tabata , Maduka manne karibu na chuo cha Ualimu cha St. Mary.

Vilevile ,tunapenda kuwakumbushia kuwa misa ya shukrani itafanyikaTabata, kanisa la KKKT usharika wa Tabata Matumbi siku ya Jumapili ya tarehe 20 Januari, 2013 kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Tunawashukuru watu wote kwa ushirikiano mwema na upendo waliotuonyesha kipindi chote cha msiba wa Mama yetu mpendwa. Tunaomba Mungu awabariki sana.

Marehemu Ruth Mollel Biduga alikuwa mama mwenye upendo,ukarimu kwa kila mtu na hii itakuwa shughuli ya wapenzi wake kumtakia safari njema na mapumziko mema. Mungu ni mwenye Heri na mwenye Huruma tele.

- Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Familia ya Biduga poleni sana na binafsi nimeguswa sana na kifo cha Mwl.Ruth Biduga alikuwa mwalimu wangu pale Azania Secondary School, ni kweli alikuwa mwalimu mama kwani alikuwa mpole sana na mwenye kuona wanafunzi wote kama wanae poleni sana.

    ReplyDelete
  2. POLENI SANA FAMILIA YA MOLLEL NA BIDUGA.MUNGU AWAPE NGUVU.MWL BIDUGA NI YULE ALIKUWA MWALIMU JANGWANI?NILIMFAHAMU MWL BIDUGA AKIWA MWALIMU WANGU MWANZA.RIP MAMA BIDUGA.

    ReplyDelete
  3. Rest in Peace Mwl Biduga, ulikua mwalimu na mama yetu pale Azania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...