Familia ya marehemu Dr. Enock Ndoganije Sayi wa Mbezi beach Dar es Salaam tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wote walioshiriki tangu katika kuugua hadi mazishi ya mpendwa wetu Dr. Enock Ndoganije Sayi.

Tunatambua ukarimu, upendo, faraja na misaada yenu mbalimbali mliyoitoa kwetu katika kipindi hicho kigumu kwetu.

Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja, bali tunatambua ushirikiano wenu mulio tupatia .

Shukrani za pekee ziwaendee uongozi na wafanyakazi wote wa Wizara ya Afya, MUHAS, MOI, MNH, Chama cha madaktari wanawake Tanzania, uongozi na wafanyakazi wa Hospitali ya Agakhan, TAFES, wachungaji na washirika wa kanisa la KKKT Mbezi beach, majirani ndugu na marafiki wote waliokuwa nasi katika kipindi hicho kigumu kwetu.

Familia imeandaa sadaka ya shukrani itakayofanyika jumapili tarehe 13/01/2013 katika kanisa la KKKT Mbezi beach kuanzia saa nne asubuhi, tunawakaribisha ndugu, jamaa na marafiki wote kuungana nasi.

Daima tutamkumbuka. Mungu aiweke roho yake mahali pema, Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...