Familia ya Marehemu Siraju Juma Kaboyonga (pichani) inatoa shukurani zake za dhati kwa wote walioshiriki kwenye msiba na mazishi ya mpendwa wao Siraju Juma Kaboyonga aliyefariki tarehe 18/12/2012 na kuzikwa tarehe 20/12/1012 katika Makaburi ya Kisutu Dar es salaam.

Tunatoa shukurani za dhati Kwa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete - Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais mheshimiwa Gharib bilal ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………kwa taasisi, makampuni, ndugu, jamaa na marafiki kutoka Tabora, Mwanza Dodoma na kwingineko ambayo kwa aina ya pekee walijitolea kwa hali na mali kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu.

Ni vigumu kutaja kila mtu ILA Kwa uchache tunapenda kutoa shukurani za pekee Kwa NSSF, PPF, PSPF, TEA, SSRA, Ofisi ya Makamu WA Rais, Mfuko WA pembejeo, mheshimiwa Malima na Sheikh Yusufu wa Masjid Kuba.

Tunamwomba mwenyezimungu awaongezee pale mlipotoa na awajalie upendo wenu uzidi daima dumu. Yote yaliyotokea ni mapenzi ya Mwenyezimungu mwingi wa Rehema mwenye Kurehemu.

Tunamwomba mwenyezimungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Arobaini ya marehemu itasomwa nyumbani kwake Sinza Mori tarehe 26/01/2013 saa saba mchana.
Wote mnakaribishwa kwenye shughuli ya arobaini Inshallah.

INNA LILAH WAINA ILAH RAJIGHUUN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. goon to soon we will forever miss you... may ua soul rest in peace.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...