Kapteni
Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa
mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8
Q300 . Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22.Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.
Marubani wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo asubuhi.
Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam.
Safi sana ATCL.Tulipojikwaa tumejikwaa,tusirudie kujikwaa......
ReplyDeleteDavid V
Kwa kweli wanajitahidi kadri ya uwezo wao.Kuna umuhimu wa kuangalia namna mpya ya kuliendesha shirika hilo kongwe
ReplyDeleteNimesikitishwa sana na kauli ya Waziri kwa kusema kwamba wanaiadabisha ATCL kwa kuleta shirika la ndege lenye kutoa huduma kwa bei nafuu.Ukweli ATCL imekufa kutokana na maamuzi mabovu ya serikali na udhibiti hafifu.Ma Auditor internal na external wanafanya kazi gani ? Usalama wa taifa wanafanya kazi gani ? Mi nadhani usalama wa taifa unajumuisha kuthibiti hata mambo yanayopelekea kufilisi mashirika ya serikali ?MSIFE MOYO ATCL MANAKE NAONA WAZIRI KESHAWATUPA.MPIGANE MUWE AUTONOMOUS ILI MPANGE MIPANGO YENU NA KUIFANYIA KAZI BILA KUINGILIWA NA WANASIASA
ReplyDeleteTunaiombea mafanikio mema.
ReplyDeleteDaima mbele. Tuna Imani na juhudi za kuifufua upya ATCL. Tunawaunga mkono.
ReplyDeletekioo kilichotoka marekani tayari kimefungwa? ok sawa tuendelee na safari zetu tutafika tu waagenda lwaviga a.k.a sukuma twende.
ReplyDelete