SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA


TAARIFA KWA WANANCHI KUHUSU KUFUNGWA KWA MAUZO YA NYUMBA ZA MAKAZI ZA kIGAMBONI HOUSING ESTATE ZILIZOKO KIGAMBONI DAR ES SALAAM

Shirika la Nyumba la Taifa lililizindua mchakato wa mauzo ya nyumba za Makazi za Kigamboni (Kigamboni Housing Estate) tarehe 20 Desemba 2012, ili kuwapatia Watanzania walioko ndani na nje ya nchi kupata muda wa kujiandaa kwa ajili ya tarehe rasmi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuanza kupokea rasmi pesa. Fursa hiyo ililenga kuwapa nafasi pia watu walioko nje ya nchi, waliosafiri kipindi cha sikukuu na vile vile ilizingatia maoni ya wateja wetu ambao wamekuwa wakipendekeza kupata taarifa ya kuanza mauzo kuanzia wiki moja na zaidi ili waweze kijipanga.

Kuanzia tarehe 2 Januari 2013, maombi yalianza kupokelewa na mwitikio umekuwa mkubwa sana. Tumepokea maombi zaidi ya asilimia 120 ya idadi ya nyumba 182 zinazouzwa. Tunawapongeza sana wananchi kwa kuitikia wito wa kununua nyumba za makazi za Kigamboni Housing Estate.
 Kama utaratibu wa mauzo unavyotaka, tukishapokea maombi zaidi ya asilimia 120 lazima tutangaze kufungwa kwa mauzo ya nyumba husika. Mnamo tarehe 3 Januari 2013 tulifunga rasmi mauzo ya nyumba hizo baada ya kufikia lengo hilo kwa mradi huu wa Kigamboni kwa sasa.

Tunapenda kusisitiza kuwa tumefunga zoezi la kupokea pesa kutoka kwa wanunuzi wa nyumba za mradi huu wa Kigamboni. Hata hivyo, kumalizika kwa mauzo ya nyumba hizi za Kigamboni, ni mwanzo wa kuanza mauzo ya nyumba za miradi mingine mingi ya nyumba za gharama nafuu ambayo zinazondelea kujengwa na Shirika hapa Dar Es Salaam na maeneo mengine  nchini. Miradi mingine ya nyumba za gharama nafuu  inayotekelezwa kwa sasa sambamba na mradi huu wa Kigamboni ni pamoja na Mwongozo Housing Estates (Dar Es Salaam) na miradi mingine inayoendelea katika Mikoa 14 nchini.

Mikoa na Wilaya zenye miradi ya nyumba za gharama nafuu kwa sasa ni pamoja na Mvomero (Morogoro), Kongwa (Dodoma), Ilembo (Katavi), Geita, Mkinga (Tanga), Babati (Manyara), Monduli na Longido (Arusha), Mkuzo (Songea) na Unyankumi (Singida).

Hivyo, tunawashauri wananchi waendelee kujiandaa zaidi kwa kuweka akiba ya fedha na vile vile kuendelea kufanya mawasiliano na benki ambazo zinaushirikiano na Shirika la Nyumba la Taifa ili waweze kufanyiwa tathmini ya mikopo yao ya nyumba, ili mara tu taarifa za mauzo ya nyumba katika Miradi zitakapotoka waweze kununua nyumba hizo. Benki ambazo tunashirikiana nazo ni pamoja na Commercial Bank of Africa (CBA), NBC, NMB, AZANIA BANK, BANK OF AFRICA(BOA) na Banc ABC. Benki zingine ni EXIM BANK, KCB na Stanbic Bank.

Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono ili kulijenga Taifa letu..

Pamoja Tunaweza

   Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii.
Shirika la Nyumba la Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hope zoezi hili lilienda kwa haki bila undugunaizesheni.

    ReplyDelete
  2. UTAPELI MTUPU, SISI WATU WA HALI YA CHINI AMBAO NDIYO TULIPASWA KUWA WALENGWA TUESHINDWA KUOMBA KUNUNUA NYUMBA HIZO TOKANA NA GHARAMA KUBWA AMBAZO HATUZIMUDU ZA KUNUNUA NYUMBA, HAYA MATAJIRI KAZI KWENU MAANA NDIO NAONA MNALENGWA ZAIDI, MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!!!

    ReplyDelete
  3. HONGERENI SANA NHC KWA MAONO HAYA. HEBU JAMANI IKUMBUKENI MTWARA BASI. FANYENI KAMA DHARURA MAAANA KUNA SHIDA YA NYUMBA ZA BEI RAHISI NA HII NI PESA NJE NJE. JARIBUNI (IKIWEZEKANA) UNGANENI NA WADAU WA NJE (ISRAEL WAPO WENYE INTEREST NA NI WAZOEFU WA NYUMBA NAFUU KWA UJENZI WA HARAKA ZAIDI). TUTAKWENDA KWA HARAKA NA FAIDA ZAIDI. CHEERS NHC!

    ReplyDelete
  4. Hivi jamani Mtanzania aliye maliza chuo kikuu mshahara wake ni kiasi gani kwenye ajira serikalini? hivi hawa ni Watanzania wakipato gani? kwa kulinganisha na mauzo haya ya nyumba za watu wa kipato cha chini?Tuwemakini mlundikano wa madeni kwa wananchi kuna madhara makubwa kwa taifa kwa ujumla. Mimi biafsi nafanya utafiti wa harama halisi wa hizi nyumba kisha nitaweka wazi kwenu wadau wenzangu muone nani anafaidika na hili zoezi. Changa la macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...