Na mwandishi wetu, Addis Ababa
Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.

Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.

Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.

Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Vijana msikate tamaa.Tucheze mechi nyingi na hasa za ugenini

    ADEN RAGE-Juzi nilikusikia ukidanganya watanzania kwenye kipindi cha michezo kwenye redio moja maarufu Tanzania kwamba mchezo huu hautambuliwi na FIFA(wakati ukitetea wachezaji wa simba kujiunga na timu ya Taifa) angalia hii link-http://www.fifa.com/worldfootball/index.html HAUNA UZALENDO NA NCHI.ACHA SIASA KWENYE MICHEZO UNAJISHUSHIA HADHI

    David V

    ReplyDelete
  2. Stars mmebadilika sana na soka limekuwa ,hii ikimaanisha kocha ni mzuri na wachezaji waliopo sasa ni vipaji vizuri.Hongera sana kwa soka la kusisimua na hii ikumbukwe kuwa wachezaji wa yanga wote wamekosekana ktk first eleven ,hivyo nadhani wangekuwepo matokeo yangekuwa mengine.Stars oyee ,kazeni mwendo ,tutafika!!Big up mdau wa Ughaibuni!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...