Salaam Ankal Michuzi na Wadau wote,
Nimeona mara kadhaa anapotangulia mtu yeyote mbele za haki alimradi ni mtu mashuhuri basi mwili wake hubebwa na GARI LA WAGONJWA. 

Sasa kinachonisumbua ni kwanini magari ya kubebea wagonjwa yana bebea maiti. 
Je kukitokea mgonjwa atasubiri mpaka hili gari limalize shughuli za msiba ndiyo likamhudumie mgonjwa? 
Sikuhizi kuna magari maalum ya kukubebea miili ya waliotutangulia kwenye haki kwanini yasitumiwe hayo. Sijajua hili wazo limetoka wapi ninauliza maana inawezekana kunasababu ya kufanya hivyo, kama kuna sababu naomba tuambiane ili na sisi wengine turekebisha akiba zetu kichwani.

Mdau wa Globu ya Jamii, Uswazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ooh mdau wa swali la kizushi
    Ni kwamba hayo magari uyaonayo yanabeba miili ya waliotutangulia ni maalumu kwa kazi hiyo sio kwamba ni ya kuwabebea wagonjwa hapana hizo gali ni za kazi yake hiyo ila nyingi zinzfanana sana ndio maana waona hivyo na yote inategemea na muundo wa gari lenyewe pia = mdau wa michuizi

    ReplyDelete
  2. Hill gari unaloliona wewe ni ambulance limenunuliwa rasmi kwa ajili ya kubebea waliotangulia mbele ya haki na watu hukodi kwa shughuli hiyo tu. Si kama wagonjwa wanaathirika la hasha. Magari ya aina hii yako namna mbalimbali duniani kutegemea na mahali ulipo. Tembea ujionee. Mwenyezi mungu awalaze pema peponi waliotutangulia na kuwapunguzia adhabu za kaburi - amen

    ReplyDelete
  3. Mi sijakuelewa

    ReplyDelete
  4. Kaka unamaanisha kwamba watu wanatumia gari la kubeba wagonjwa kwenda nalo mazikoni(makaburini)au kubebwa huku unakokusema ni kwamba imetokea ajari labda tuseme ya gari, likaja gari la kubeba wagonjwa likabeba maiti na kuipeleka hospitali??Katika uchunguzi wako kuna uthibitisho wowote ya kwamba hayo magari ni ya serikali maana siku hizi kwa huko nyumbani kuna embulance za kukodi pia ambapo yawezekana pia ikabeba maiti badala ya mgonjwa???Iwapo kuna uthibitisho wa kutumika magari ya serikali ktk hilo basi itakua si sahihi kwakua yawezekana ikatokea dharura ya mgonjwa kama unavyosema lakini kama ni gari la kukodi sidhani kama imekaa vibaya.

    ReplyDelete
  5. Mdau usijisikie vibaya kuuliza. Huwezi kupata majibu kabla hujauliza maswali. Labda tu hukufafanua kubeba maiti kutoka wapi kwenda wapi. Ambulance zinabeba maiti kutoka crime scene kwenda hospitali kwaajili ya autopsy au utaratibu mwingine wa kitabibu na kisheria. Baada ya kuwa mwili uekabidhiwa kwa funral homes, hapo ndipo gari maalum la kubeba maiti linapotumika kwa maombezi, mazishi au kuchomwa mototo. Tofauti kati yetu na wenzetu, ni kuwa there several fire houses to dispatch ambulances to multiple 911 calls. Labda na sisi tukifika miaka 300 ya uhuru kama wenzetu tutakuwa na ambulance nyingi. Kwa uthibitisho zaidi nenda google.

    ReplyDelete
  6. Usifikirie sana kwani utapatwa na pressure maana hapa Tanzania kila kitu kinakwenda kinyume na maadili. Usishangae mgonjwa kupanda bajaji au teksi ila kwa aliyeenda mbele ya haki akapata ambulance na huduma zote ambazo mgonjwa ndiye anahitaji. Yaani hiii nchi we acha tu, sijuwi viongozi wetu wana nini kichwani?

    ReplyDelete
  7. kwani hilo gari lipo mmoja tuu??

    ReplyDelete
  8. GARI LA KUBEBEA WAGONJWA NI GARI MAALUM NA ENDAPO IMEPIGWA SIMU KWENDA KWENYE TUKIO LA KUMCHUKUA MGONJWA NA IKAKUTA MGONJWA AMESHAFARIKI HAPO KUNA GARI NYENGINE MAALUM YA KUBEBEA MWILI AMBAYO INAKUWA KAMA HIYO YA KAWAIDA ILA TU INAKUWA HAINA VIOO PEMBENI VIOO NI KWA DEREVA TU,KAMA HIYO YA KAWAIDA NA FULL A/C, NA GARI YA KWENDA KWENYE MAZIKO PIA IPO TOFAUTI KABISA NA HIZO GARI 2 ZA MWANZO,KWA WENZETU KUNA GARI ZA DHARULA AINA 3 TUFAUTI,MAREHEMU HARUHUSIWI KUBEBWA KATIKA GARI LA KAWAIDA LA WAGONJWA.

    ReplyDelete
  9. Wewe utakuwa ni msukuma au Mjaluo, yale sio magari ya wagonjwa ni magari maalumu ya kubebea MAITI ndugu!

    ReplyDelete
  10. Mnyalu Mdau wa TISA Sat Jan 12, 08:00:00 AM 2013

    Ohhh !

    Unayo nafasi kuwatania Watani wako wa Jadi Wasukuma na Wajaluo, lakini zingatia hapa tunazungumzia Maafa, Majanga, Vifo na Misiba!

    ReplyDelete
  11. Wadau pana tofauti kati ya aina mbili za Magari kutokana na aina ya Huduma.

    1.Ambulance (huwa na rangi Nyeupe pia zinamilikiwa na Mahospitali na Mamlaka)hizi ni kwa ajili ya wagonjwa, au wagonjwa walio ktk hali ya dharula ambao huweza kutokea wakafia ndani ya chombo wakiwa njiani kuelekea Hospitalini, hapo hakuna jinsi itabidi gari iwe imebeba maiti.

    2.Hearse ({Gari za maiti}, hizi huwa na Rangi nyeusi na humilikiwa na Makampuni Binafsi sio ya Umma ya Mazishi ambayo nchini kwa sasa ni huduma binafsi zenye kulipiwa), hivyo haiwezi kutokea mgonjwa akabebwa na gari la Maiti, isippokuwa inawezekana mgonjwa akapandishwa akiwa hai lakini akafia ndani ya Ambulance akiwa njiani kupelekwa Hospitalini.

    Hizi ndio tofauti mbili kati ya gari la Mgonjwa na Gari la Maiti!


    ReplyDelete
  12. WAPENDWA MIMI NAWAKATALIA KABISAAA,HIZI GARI ZA AINA HII KAZI YAKE NIKUBEBA NDIZI KUTOKA MARANGU KWENDA DARE ES SALAAM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...