Wachezaji wa timu ya Simba wapo nchini Oman kwa kambi maalum ya kujifua wakati wakijiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo jioni ya leo wanakipiga na timu ya taifa ya wanajeshi wa Oman ambayo nayo inajiandaa kucheza Kombe la Dunia la wanajeshi. 

wakiwa nchini Oman walialikwa katika hafla fupi iliyoandaliwa na mdhamini wao wa safari ya Oman,Mama Rahma Al Kharoos iliyofanyika nyumbani kwake eneo la Al Kheri jijini Muscat, Oman jana usiku kwa ajili ya chakula cha usiku.

Walikula pamoja na baadaye bendi maalum kutoka Tanzania iliwapigia muziki na wakaserebuka pamoja huku Rahma akimwaga noti kwa kuwatunza wachezaji wa Simba waliokuwa wakiyarudi magoma nyumbani hapo

Katika hafla hiyo, Rahma alikabidhiwa jezi ya Simba na Musleh Rawah ambaye ni mmoja wa wadau wa Msimbazi na jezi ya timu ya taifa ya Oman na kocha wa makipa wa timu hiyo, Haroun Amur.
Mmoja wa wadau wa Timu ya Simba,Musleh Rawah (mwenye kanzu) akimkabidhi Mama Rahma Al Kharoos Jezi ya timu ya Simba ikiwa ni Kama Shukran kwa Mwaliko wa Timu hiyo nchini Oman.
Kocha wa Makipa wa Timu ya Taifa ya Wanajeshi wa Oman, Haroun Amur akikabidhi Jezi ya Timu yake kwa Mama Rahma Al Kharoos.
Wachezaji wa Simba wakijisevia Msosi.
 Wachezaji wa Timu ya Simba wakiyarudi Magoma huku Mama Rahma Al Kharoos akiwatunza manoti.Picha zote na Saleh Ally.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wachezaji hawatakiwi kula misosi mingi mpaka wakajisahau na kuanza kutoka vitambi.

    Kumbukeni nyinyi ni wanamichezo.

    ReplyDelete
  2. hakika unapokuwa na nafasi kubwa ni busara sana kuwa na wasaidizi wengi! safi sanaaa!

    ReplyDelete
  3. KWA MSOSI HUO NA KUIBA TAARABU .Lazima mpigwe 7-0 mwaka huu na chama kubwa ( YANGA).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...