Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohammed Mansour akimkabidhi Katibu wa Taasisi ya Zanzibar Free Drug Badru Nassir Ali sehemu ya msaada wa vyakula na bidhaa nyengine za nyumbani kutoka Vodacom Foundation kusaidia nyumba kumi na moja za kusaidia waathirika wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo Kisiwani Unguja.Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(Katikati) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Hafla hiyo ilifanyika Mjini Zanzibar hivi karibuni. Msaada huo ni sehemu ya program ya Pamoja an Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi msaada ya vyakula na bidhaa nyengine za matumizi ya nyumbani uliotolewa na Vodacom Foundation kwa vituo kumi na moja vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo. Kutoka kulia kwake ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim,xxxx, Meneja wa Vodacom Zanzibar Moh'd Mansour, Katibu Msaidizi wa Mtandao wa Free Drug Zanzibar Fatma Sukwa na Katibu wa Mtandao huo Badru Nassir Ali. Msaada huo ni sehemu ya Programu ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akimkabidhi Katibu Msaidizi wa Mtandao wa Free Drug Zanzibar Fatma Sukwa sehemu ya msaada wa vyakula na bidhaa nyengine za nyumbani kutoka Vodacom Foundation kusaidia nyumba kumi na moja za kusaidia watumaiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo Kisiwani Unguja.Wa pili kuhsoto ni Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohamed Mansour na Meneja Mahusiano ya Nje wa kampuni hiyo Salum Mwalim. Msaada huo ni sehemu ya program ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka.
Baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya waliopo kituoni hapo kwa ajili ya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na waanzilishi wa vituo na watumiaji wa dawa za kulevya mara baada ya kutoa msaada ya vyakula na bidhaa nyengine za matumizi ya nyumbani uliotolewa na Vodacom Foundation kwa vituo kumi na moja vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mateja yanapenda matunda na juice.

    ReplyDelete
  2. MASIKINI NGUZU KAZI YA TAIFA HIYOOO NA MIJIFISADI INANUFAIKA TU NA KUATHIRIKA KWA KIZAZI CHA TAIFA. IKO SIKU YENU!

    ReplyDelete
  3. Kwa nini tusiweke mikakati ya kuwasaidia kabla hawajaathirika? Watu wengine wanajitangaza kusaidia vituo hivyo lakini hela wanayonunulia hiyo misaada imetokana na biashara ya madawa ya kulevya. Tungekuwa wakweli na kutolindana kwa kuwa hizi biashara ni za watu wakubwa sana katika nchi tungefanikiwa. Vodacom foundation tafuteni mbinu ya kuelimisha watu kuwaweka hadharani wauzaji badala ya kuwasaidia waathirika!

    ReplyDelete
  4. Ohhhooo,

    Unga ni matatizo makubwa tupigane dhidi ya hili tatizo.

    Angalieni masista duu wazuriii nywele lainiii lakini Miteja!

    ReplyDelete
  5. Hehehehehe!

    Teja kula yake chakula cha kawaida ni ya tabu sanaaa, akijitahidi amekula Juisi Biskuti na Keki, kwa nini msiweke pia Juisi na Keki ktk Msaada huo?

    Uteja na chakula kama Ugali kwa Nyama, Ubwabwa na Maharage wapi na wapi?

    ReplyDelete
  6. Mama Grace umependeza!

    ReplyDelete
  7. Kuna jambo moja linalo nitatiza siku nyingi!Haya yote ya Uteja na Biashara ya Madawa ya Kulevya ni "matokeo tu" ya matatizo sugu ya kiuchumi,mfano,kukithiri kwa ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana,kupanda mno kwa gharama ya maisha,vipato au mishahara duni isiyo tosheleza mahitaji ya msingi,uwezo mdogo wa nchi kiuchumi(teknolojia duni,elimu tasa,nk),na sababu nyinginezo nyiiiiingi!Swali langu ni kwamba:Hivi kweli,katika mazingira au taswira hii ya Kitanzania,ya Utanzania,"ni haki kweli,ni busara kweli,ni halali kweli,je,inaleta mantiki yoyote?",kuitarajia Zanzibar,yenye watu wanaopata milioni moja na ushee hivi(hao tu,ambao ni sawa na idadi ya watu wa wilaya moja ya Tanzania Bara),serikali ya Zanzibar "itegemee itawatoza kodi wazanzibari wachache hivyo" ili ipate Fedha za Kuendeshea shughuli zote za serikali?(Miradi ya Maendeleo pamoja na Matumizi ya Kawaida)!Mbali na fursa ilizo nazo Zanzibar,tokana na rasilimali bahari;vivutio vya utalii;kilimo cha viungo(spices)mbalimbali,nk.,LAKINI,JE,HAIJAWAINGIA AKILINI VIONGOZI WETU,kwamba,Tanzania Bara,kutokana na ukubwa wake na rasilimali nyingi zilizopo Bara,kwamba,"tunalazimika kunyofoa japo kidogo(hata asilimia 10% ya Pato la Taifa toka upande wa Bara)" ili kuwapa "Booster" kichocheo,wenzetu wa Visiwani,wapate "pazuri pa kuanzia,nguvu ya ziada" katika kukabiliana na matatizo hayo ya kiuchumi,ambayo,matokeo yake ndiyo huko,kujikuta Vijana wengi wamekata tamaa na kupoteza kabisa matumaini ya kuishi,nakujiingiza katika vitendo hivyo hatarishi katika maisha yao,na hatimaye,kulitia Taifa umaskini mkubwa zaidi,kwa kupoteza Nguvukazi hiyo adhimu? hebu kila mmoja wetu atafakari kwa kina,aje na mawazo yake mmbadala kuhusu hoja hii muhimu!Kwasababu,hata Zanzibar wakisema wakope toka Nje,bado tatizo litakuwepo,watakopa kiasi gani,kitakacho weza kubebwa na nguvu yao kuichumi kwa sasa!Ya huko mbeleni,hatuyajui,ni hapo yatakapo tokea,iwapo,yatapatikana mafuta au gesi au chochote kile!Lakini,hata hivyo vyote vikipatikana,kuna kikwazo gani,surplus kidogo ya Bara ikamegwa ili iwape nguvu ya ziada ya kuanzia,wenzetu wa Zanzibar?Kwa wale wenye mawazo potofu,"mtu hata azikiri kutwa kucha na kilemba chake kichwani",huwezi kuihamisha Zanzibar kuipeleka Madagascar au Comoro!Bado itabakia papo hapo karibu sana na ndugu zao wa Bagamoyo na Pangani!au nasema Uongo? Kazi kwenu,watunga sera!Mpaka aje Mjerumani atufundishe hata katika hili,jamani?Tubadilike.

    ReplyDelete
  8. Wazanzibari Ulevi ni nje ya Misingi mizuri ya Dini tupigane kuachana nayo ili tupate Rehma!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...