Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Bwana George R.W Nyatega akitoa muongozo mbele ya wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo, (hawapo pichani) namna ya kujadili na kutoa maoni juu ya katiba mpya.

Wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), wameshiriki kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya.

Awali akifungua majadiliano hayo kuhusu katiba mpya ndani ya ukumbi wa vikao Regency Park Hotel, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. George Nyatega aliwasihi wafanyakazi hao kutoa maoni yao kwa uhuru kwani suala la katiba mpya ni la kitaifa na kwa hiyo maoni yote yataheshimiwa.
Mkurugenzi Msaidizi wa masuala ya Sheria Bw.Firmat Tarimo, akisoma majumuisho ya maoni kuhusu katiba mpya, maoni yaliyotolewa na wafanyakazi wa Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Sehemu ya wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu wakiwa na shauku ya kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya katika ukumbi mikutano Regency Park Hotel
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa akitoa maoni kuhusu katiba mpya.
Majadiliano muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha wafanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kuhusu kutoa maoni ya katiba mpya. Kutoka kushoto mwenye miwani ni Cuthbert Simalenga Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA, katikati ni Bw. Abdallah Hatibu Meneja wa Bodi ya Mikopo kanda ya Zanzibar, kulia ni Bw. Firmat Tarimo Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Sheria.
Afisa mikopo Bi.Octavia Selemani akichangia juu ya katiba mpya ndani ya ukumbi wa Regency Park Hotel Mikocheni Jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ndugu wesi! kwa nini mnawatesa watoto wasio na hatia? Mnajua kuna kufa? mtajibu nini kwa Muumba? nawauliza nyie ndugu wesi? Mnawadhulumu hadi MAYATIMA? Ndugu wesi moto wa GESI unawasubiri naapia!Mwe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...