Mtoto Hanifa Salum Hassan mwenye umri wa miaka mitano anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu (Leukemia) ambao umemfanya ashindwe kusimama na kutembea, anasumbuliwa na maumivu ya kichwa wakati wote, wakati mwingine hushindwa kupumua hivyo kulazimika kupumua kwa kutumia mashine pia hawezi kula analishwa kwa kutumia mirija na pia kila baada ya muda inabidi abadilishiwe damu.

MATIBABU

Matibabu ya mtoto Hanifa ni ya gharama kubwa sana. Ugonjwa wake haukujulikana alipopelekwa Hospitali ya taifa Muhimbili lakini alipopelekwa nchini India gharama za uchunguzi pekee zilikuwa dola 7,600 ambapo mtoto Hanifa aligundulika kuwa na ugonjwa wa Acute lymphoblastic Leukemia.

Matibabu yake yalipangwa yawe kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya matibabu iligharimu dola 10,000. Mwisho wa awamu ya kwanza zilihitajika dola 10,000 zingine ili aingie kwenye awamu ya pili ya matibabu lakini uwezo wa ndugu na jamaa ulikuwa ndio umeishia hapo hivyo matibabu ya mtoto Hanifa yalilazimika kukatishwa na Hanifa kurudishwa Tanzania.

Ripoti za madaktari India zilipelekwa Muhimbili ambapo matibabu ya mtoto Hanifa yalipangwa kugharimu Tsh. milioni 2 kwa mwezi.


Hakuna pesa za kumwezesha mtoto kuanza matibabu Muhimbili hivyo mtoto Hanifa amebaki nyumbani jijini Dar es Salaam akiwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi mbalimbali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yake.


Hadi sasa ndugu na jamaa wanahaha kutafuta pesa za kumwezesha mtoto Hanifa kumalizia awamu mbili za matibabu yake nchini India kama ikiwezekana au ikishindikana basi aweze kuanza matibabu Muhimbili.

MICHANGO

Kwa watakaopenda kujitolea kuokoa maisha ya Mtoto Hanifa wanaombwa watoe michango yao kupitia akaunti hizi

Kwa walio Tanzania

Jokha Khamis Issa
Akaunti Namba: 041212000428
People Bank of Zanzibar
Kwa mawasiliano namba ya simu ni: +255 777 462587

Kwa walio nje ya Tanzania wanaweza kutuma michango yao kwa akaunti hii

Suleiman Maadini
Account Number: 15092968
Sort Code: 30-67-99
Bank: Lloyds TSB
Country: United Kingdom
Kwa mawasiliano na Bwana Maadini: +44 78 18674305

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Loh.Mungu amsaidie sana huyu mtoto apone haraka.Kuna kundi jingine kama mimi,tupo nje lakini tuna akaunti katika benki za Tanzania. Mara nyingi tunatumia Internet Banking System kufanya transactions.Wahusika kama mna akaunti NBC au NMB,CRDB ziongezeni hapo.Ni mtu mmoja tu anaitwa MAGGID MJENGWA aliwahi kunielewa wakati anachangisha michango ya familia ya Mwangosi(RIP),wengine wanachukulia kama utani wa kwenye Blog.Kuna sehemu za utani kwenye blog na kuna sehemu zisizo na utani kama suala hili.

    David V

    ReplyDelete
  2. David V upo sawa, na hiyo njia ya internet banking hata baadhi ya wafanyakazi wa ma bank husika hawajui ni nini!! ni huduma nzuri na rahisi na haina transaction fee yeyote kama unahamisha bank za aina moja, wahusika kama mna account za NBC, NMB, na au CRDB ziongezeni tutajitahidi kwa uwezo wetu kuongeza japo chochote!!!!!!

    ReplyDelete
  3. David V

    naomba unifundishe jinsi ya kufanya online banking(internet Banking) na NBC au CRDB sijawahi kusikia hyo huduma kabisaa tafadhali utakua umetusaidia wengi kweli tuliopo nje ambao tunashindwa hata kujua salio mpaka kwenda ATM fanya mpango basi hapa hapa

    ReplyDelete
  4. Anonymous namba 3 CRDB wanayo internet banking wewe nenda tu watakuelekeza.

    ReplyDelete
  5. inakuwa vingumu sana kufanya internet banking ya crdb kama uko nje ya nchi kwa mara kwanza, kwa sababu unabidi uregister na password unachukua kwenye branch yako ya crdb ndio baada ya hapo unaweza kubadilisha na kuweka password yako na wewe unaweza kutumia internet banking popote pale, ila kwa nmb na nbc sina uhakika wao wanafanyaje?

    ReplyDelete
  6. Please Tupeni Akaunti namba za CRDB, NBC, NMB, Au MPESA,TigoPEsa, Airtel Money! Mimi hapa nina Mpesa na kuna hela Nipo Tayri kabisa mchangia huyu mtoto, Nimesoma hii habari nimejisikia Uchungu sana, I have Baby Gal ana 5 years pia,Yani naona jinsi wazazi wa huyu mtoto mnavyokuwa na machungu. Please Wekeni MPESA,Tigopesa,Airtel money, Easypesa etc. Akaunti ziwe NMB,CRDB,NBC tutachanga tu.Poleni sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...