Na Abdulaziz,Lindi

WATU wanne wakiwemo watumishi wa basi ndogo aina ya Hiace,wakazi wa mkoa wa Mtwara,wanashikiliwa na Polisi mkoani Lindi,kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kuwatelekeza abiria njiani kwa ajili ya kwenda kupakia na kubeba pombe haramu ya moshi (gongo).

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani hapa,George Mwakajinga,alieleza kuwa watuhumiwa hao wote wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mwakajinga amewataja wanaowashikilia kuwa ni pamoja na dereva na kondakta wa Hiace, Shaibu Daudi (30),John Mbena Saidi (25),Mariamu Yassini Mautila (36) wakazi wa Ligula,na Habiba Maulidi Sijaona (28) wafanyabiashara ya Pombe ya moshi (Gongo) mkazi wa mtaa wa majengo,Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na kitendo kilichofanywa na wafanyakazi wa gari hiyo kuwashusha na kuwatelekeza njiani abiria waliokuwa wamewabeba kuelekea mkoani Mtwara,na kwenda kijiji cha Ruhokwe kilichopo wilaya ya Lindi,kubeba pombe haramu ya moshi (gongo).

Mwakajinga akasema Hiace hiyo,ambayo mlango mkubwa wa nyuma umeandikwa neno lisemalo,Simba wa Yuda,yenye namba za usajili T 436 BJV,inamilikiwa na mfanyabiashara aitwae D.D. Chigumila wa mjini Mtwara,ilikuwa imebeba zaidi ya abiria 20,wakitoka mjini Lindi kwenda mkoani Mtwara.

“Siku hiyo hii ilikuwa ikirejea mkoani Mtwara, ambapo iliwabeba abiria na walipofika eneo la kijiji cha Mnolela, Lindi vijijini,dereva na kondakta wake huyo,waliwatelemsha njiani abiria waliokuwa wamewabeba bila ya kuwapa msaada mwingine na kuondoka zao”Alisema Mwakajinga.

Kamanda huyo wa Polisi mkoa akasema kutokana na kitendo walichofanyiwa abiria hao,walichukuwa uwamuzi wa kupiga simu kwa askari wa kata ya Mingoyo,wilaya ya Lindi,ambapo waliwafuatilia na kufanikiwa kuikuta gari hiyo kijiji cha Ruhokwe,ikiwa imebeba madumu (15) ya pombe ya gongo yenye ujazo wa Lita 300.

Wakizungumza na gazeti hili,baadhi ya abiria hao,akiwemo mke wa mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoani Lindi (LPC),Mrs Abdull -aziz,Devota Ng’itu,Lucy Aizaki,Madadi na Fatuma Mkaumba, wameiomba Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kumnyang’anya leseni ya kuendesha gari kwa dereva huyo.

“Tulikuwa tukitoka mjini Lindi kwenda mkoani Mtwara, na tulipofika eneo la kijiji cha Mnolela dereva alisimamisha gari na kutueleza gari ni mbovu hivyo tutelemke watatuombea msaada gari nyingine,jambo ambalo halikuwa la kweli”Alisema Fatu Mkaumba.

Abiria hao walisema mara baada ya kutelemka chini ili kutekeleza ombi la wafanya kazi, waliondoa gari na kuondoka zao,huku bila ya hata kuwarejeshea fedha walizozichukuwa za nauli walizolipa.

”Kwa kusema kweli ndugu yetu mwandishi wa habari,wafanyakazi hao wa Hiace wametufanyia kitendo cha kinyama ambacho hakiwezi kuvumiliwa,ikizingatiwa muda waliotutelemsha njiani ni wa jioni ya saa 12:45”Alisema Mrs Abdull-azizi.

Mwakilishi wa Sumatra mkoani Lindi,Duncan Somi,ameliambia gazeti hili kwamba kuwa kitendo kilichofanywa na wafanyakazi hao wa Hiace,kukatisha au kuwatelemsha na kuwatelekeza abiria njiani ni kosa chini ya kifungu cha (17) kifungu kidogo cha (1) {C} ambapo faini yake sio chini ya Sh,250,000/-

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. USA inajulikana kama ni MOONSHINE.

    ReplyDelete
  2. Watafanyeje sasa na maisha ndo mumewakaangisha namna hiyo?

    ReplyDelete
  3. WAACHENI MKAMAMATE MAJAMBAZI NA MAFISADI. WATOTO WAO WAKALE WAPI? KUNA ANAYELAZIMISHWA KUNYWA POMBE?

    ReplyDelete
  4. KONYAGI MNAONA SASA?

    Tulitoa Maoni mfikirie uwezekano wa hii Konyagi-B aka Gongo kama itaingia ktk Gridi ya Taifa Sambamba na Konyagi halisi ili uzalishaji ukue Kitaifa na pia kuwakomboa kwa kipato watu kama hao akina mama hapo!

    ReplyDelete
  5. Amaaaaaaaaa somo kwani ilipo hayo hiyo kitu ya nkorosho nini.

    ReplyDelete
  6. hiyo inayo semekana ni gongo,je, kuna "mtaalamu yoyote" aliyetambua kwamba ina kiwango gani cha ulevi (alcohol content)? kuna pombe kali zinauzwa madukani(groceries,pubs,bars,etc)zenye kilevi(alcohol content)hadi asilimia 60% hata 75%!,msije mkawanyanyasa hao kina mama,wanahangaikia elimu ya watoto zao,au hata kujikimu kimaisha tokana na hali duni ya kiuchumi,bureee,kumbe pombe yenyewe inayoitwa gongo,ni kilevi cha kilevi kinacho kubalika kabisa na kuuzwa hata katika ma baa mitaani! natoa tu hiyo tahadhari,maana,ndugu zetu wa vijijini mara nyingi huchukuliwa kama "washamba,wasiojua kitu!",lakini sio kweli nyakati zote,"they surely know what they are doing!".Sasa,kwamfano,mikoa ya kusini,Lindi na Mtwara,ambako,zao la Korosho ndilo zao lao kuu la biashara,na zao hilo lina byproducts nyingi zenye thamani kubwa kibiashara,miongoni mwake ni pombekali itokanayo na Mabibo ya Mikorosho!jina lake nimelisahau,sijui ni "Uraka" au vinginevyo!Tusikimbilie kuwanyanyasa hao ndugu zetu wa vijijini waliopigika vibaya na hali duni ya maisha,tuwe msaada kwao,wakikosea waelimishwe,kwamfano,kama hilo gongo lina kilevi(alcohol content)hatarishi,waelimishwe,vipi wataweza kupunguza kilevi hicho,ili na wao,waweze kusukuma mbele maisha yao na ya familia zao!nafikiri nime eleweka.Tusifikiri kwamba,mara zote,watu kama hao,wana nia ya kuvunja sheria,NO!wanajihangaisha na kile kilichopo karibu ya uwezo wao(mazao,mizizi,madini,nk)ili kujikimu kimaisha!Kitendo cha Dereva wa Basi hilo kuwaacha abiria,au kuwanyanyasa hao kina mama wenye pombe hiyo,siyo kitendo cha kistaarabu!Tujifunze na Tubadilike!Mabadiliko hayataletwa na Watu kutoka Nje,ni sisi wenyewe kwa kushirikiana na kuwa na Uzalendo!Ione shida ya mwenzako "ya kwako wewe!",tutakwenda!

    ReplyDelete
  7. Poland= "Bimber", aka "Bimberek".

    ReplyDelete
  8. Pamoja na ujanja wote, but America was build by Moonshiners and Bootleggers!!! Tunaweza iga pia :)

    $D

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...