Kaka Michuzi,
Pole na kazi,
Ninaomba kama kuna anayefahamu anifahamishe nini cha kufanya kuhusiana na DAWASCO kinondoni.
Mimi ni mteja wao Account 00505204, na ninaishi kwenye nyumba ya kawaida yenye idadi ya watu 7 na niliwekewa mita ya maji kama ilivyo wateja wengine.
Tangu
mita ya maji ilipowekwa imekuwa inaleta matatizo kwa mwezi inaonyesha
tunapaswa kulipa kati ya TZS 97,000 - 214,511, tumehangaika kuripoti
ofisi za Dawasco kinondoni (ofisi iliyoko nyuma ya Airtel HQ) kwa muda
mrefu sana na 2010 alikuwepo meneja mwanamke(sikumbuki jina) akaahidi
kwa maandishi kwamba tungefungiwa test meter lakini haikufanyika na
tulipozidi kufuatilia tukaambiwa amehama na sasa akawepo meneja (Bw.
Mtowela) ikabidi tuanze upya story yetu ikachukuwa tena muda mrefu
lakini test meter ikafungwa na wakagundua kwamba ni kweli mita ina
matatizo hivyo wakatwambia wataweka mita mpya hapo ilikuwa 2012.
Tukapewa maagizo kwamba wakati suala letu linashughulikiwa tuwe tunalipa angalau TZS 50,000 (elf 50).
Tulianza
kulipahiyo elf 50 lakini bado walikuwa wakifika kukata maji wakisema
tunadaiwa mamilioni ya pesa na wakishakata inabidi twende tena kwa
meneja kujieleza ndipo turudishiwe maji.
25 October, 2012 tulifuatilia Meneja akasema mita
ziliwaishia lakini zimeshawasili hivyo Jumatatu 29 October, 2012
watakuja kutubadilishia mita na tutakapopata ankara ya mwezi Novemba
2012 itaonyesha ni kiasi gani tunapaswa kulipa. Ankara ikaendelea
kuletwa ikionyesha bado tunadaiwa mamilioni ya pesa (3,789,225.80).
Leo 25 January, 2013 tatizo bado linaendelea na baada
ya kuona tumekatiwa maji kwa sababu tunadaiwa 3,789,225.80 (bill ya
December 2012) tumefika Dawasco kinondoni na tumeambiwa kwamba MENEJA AMEBADILISHWA na hayupo hivyo tufike kesho TUKAANZE TENA STORY UPYAAA!!!.
Na aliyetupa jibu hilo billing officer nae ni mgeni anasema katika kazi alizokabidhiwa hii ya kwetu haipo.
Na aliyetupa jibu hilo billing officer nae ni mgeni anasema katika kazi alizokabidhiwa hii ya kwetu haipo.
Kama mteja kwa kweli nimechoka na sielewi nifanye nini maana nimeshakwenda sana kwenye hiyo ofisi lakini hakuna kinachofanyika.
Naomba
kufahamishwa nifanye nini?? kwa sababu mpaka sasa sijui haswa napaswa
kulipa kiasi gani ?? na pia wanapokuja kukata maji wananisumbua kwa
sababu tatizo sio kulipa bali kama mteja nina haki ya kujua matumizi
yangu halisi ni kiasi gani (najua haifikii hiyo elf 50)
Asante
Mdau Kinondoni
Pole mteja wa DAWASCO. Mimi pia nilikuwa mteja wao wa maeneo ya Kijitonyama nami yalinikuta hayo hayo pale DAWASCO Kawe. Mita ilikuwa ikisoma nadaiwa mpaka mamilioni wakati maji yenyewe hayatoki. Ukienda kujieleza wanakupa fundi wao na mpaka umempata huyo fundi basi ujue lazima zitakutoka siyo chini ya laki mbili amazaidi. Mafundi wataupa gharama na wakishafunga maji yatatoka wiki tatu na kama una bahati basi mwezi mmoja baada ya hapo yanakatika tena.
ReplyDeleteKama nyumba unayoishi ni ya kwako basi suluhiso la kero yako ni kuchimba kisima. Mimi nimechimba kisma kwa kuwatumia wataalam wa mambo ya visima. Wao kwa kutumia wajiologia wao watakufayia survey na kujua wachimbe umbali gani kupata mwamba ambao hauna chumvi. Japokuwa gharama si ndogo lakini ni suluhisho la kudumu. Kwa sasa sionani na tena na nimepumzika na kero zao.
KAWASHITAKI, ILI WAKIJA NA MISPANA YAO KUKATA MAJI UNAWAONESHA NA KUWAPA NAKALA YAO!!!
ReplyDeletePOLE SANA, INAUDHI NA KUKUPOTEZEA MUDA.
Nakushauri uchimbe kisima, kuepukana na hiyo adhabu. Maana kila wakati mameneja wanahamishwa, na wakihamishwa unatakiwa uanze upya! utaishi hivyo mpaka lini?
ReplyDeleteChimba kisima ndugu yangu matatizo yatakwisha.
Kinachotakiwa kufanya ni kuonana na EWURA, hawa jamaa huwa hawana mchezo na mambo ya kijinga kama hayo. Huo ni uzembe na swala lako linaitajika kufanyiwa marekebisho ya haraka.
ReplyDeletePole na hayo maswaibu.
Mdau Mpenda haki
kaka pole sana.huu ni mwendelezo uleule wa utendaji mbaya kwenye mashirika ya umma.mimi nakushauri wapeleke tu mahakamani kwa sababu wao watakiwa wamekiuka haki zako za kukupatia huduma.na hapo lazima utapata haki yako pamoja na fidia ya kipindi chote cha usumbufu wa kukatiwa maji kulipa bili kubwa na kusumbuliwa kwa mda mrefu.kwanza kitendo cha kukukatia maji wakati unahakika umelipia ni kukudhalilisha na kukuchafulia jina.
ReplyDeletewazo langu tu mdau.
Nadhani kuna chombo cha kulinda haki ya wateja labda huko EWURA au mwenye kujua naomba atutaharifu. DAWASCO hawjali wateja wao na wanategemea kulipwa bill. Na mimi na experience ya huduma mbaya yao na tatizo sio kulipa bill ila ni huduma kama mifano ilivyoonyeshwa hapo juu. Mahakama naona itachukua muda ila nalo ni wazo zuri, labda huku EWURA kun suluhisho au kumwona top wa DAWASCO kabisa maana wafanyakazi wake wamemwangusha.Mwakyembe aliona wizara inamwangusha akaingia mwenyewe mtaani na huyu bosi wa DAWASCO inabidi ashie spana maana kazi yao ni huduma ya maji ya mteja kama mimi na wewe na sio kukaa kwenye ofisi ya AC.
ReplyDeleteHii ndio sababu ya watu kuiba maji, DAWASCO waangalie tatizo kuu na sio matokeo ya tatizo kuu. Tatizo la DAWASCO ni DAWASCO wenyewe.
Pole mdau. Mimi niko Tegeta na nilikatiwa maji toka mwaka 2008 Juni. Cha kushangaza ni kwamba napata bill kwa njia ya sms. Hadi wiki iliyopita bill yangu ni shs. 1,503,000/= Mara nyingi natumiwa hizo sms kwa vitisho vingi. Mara tunakuja kukata maji; mara tutang'oa bomba; mara huduma itasitishwa ndani ya siku kadhaa n.k. Je hawana kumbukumbu ya zinazoonyesha wateja wenye na wasio na huduma? it seems they do not update their records accordingly. Utendaji mbovu kabisa. Na hao EWURA kazi yake ni nini hasa kama wanashindwa kusimamia utendaji wa sekta hii. Wamejikita zaidi kwenye petrol stations tu. Tunawahitaji pia katika sekta ya maji. Maji ni uhai
ReplyDeletePamoja na shauri nzuri hapo juu, uwashitaki mahakamani na kudai fidia ya usumbufu huo waliokupatia wa muda mrefu, utendaji wa serikali yetu baadhi ya maeneo ni wakishenzi sana, inasikitisha
ReplyDeleteNenda EWURA haraka iwezekanavyo utahudumiwa na tatizo lako litakuwa historia. EWURA ni kama mahakama
ReplyDeleteMdau
ReplyDeleteNenda kawaripoti ukiwa na documentation zako zote kwa EWURA Consumers Consultative Council wapo
Gorofa ya pili, jengo la INFOTECH Place,lipo pale 'keepleft' cha Kawe mara baada ya kupita Clouds na makao makuu ya JKT.
Contact zao hizo hapo:
TEL: (+255-22) 2780236
Email: info@ewuraccc.go.tz
http://ewuraccc.go.tz/
Kuchimba kisima si kutatua tatizo maana kuna watu hawana uwezo na wengine wanaishi nyumba za kupanga!Kwahiyo ushauri wangu kawashtaki na upate haki yako na waweze kujirekebisha tabia yao mbaya ya kuwanyanyasa wateja!
ReplyDeletePole sana mdau.
ReplyDeleteHakuna ofisi ya DAWASCO isiyo na kero. Hata mimi bado nahangaika na swala kama lako katika ofisi ya DAWASCO iliyoko BUNJU. Baadhi ya majibu yao ni "ukisha lipia itabidi usubiri kati ya mwezi mmoja au mitatu ndio swala lako lishughulikiwe'' au ''tunasubiri vifaa kutoka makao makuu'' au ''ma surveyor wamesha toka njoo kesho saa mbili asubuhi'' ili mradi unanyanyasika kwa kitu ambacho ni haki yako.
Chimba kisima ndugu yangu. Mimi nimeshaonana na wataalamu wa visima. Wamesha kagua eneo langu na wako tayari kunikabidhi kisima kwa muda wa siku tatu.
DAWASCO ni wa kuachana nao na urasimu na rushwa zao.
Angalia hata kwenye mtandao wao. Taarifa zao haziko ''up to date''.
They did the same faking responsibility to me in 2012 at kibaha branch.At last I came to realise that most of dawasco staff specifically have very low qualifications towards their profession.let the top management or government make a scrutiny of dawasco staff by certifying their qualification requirements.or make court fire
ReplyDeletekuchimba kisima ni swala zuri kabisa, lakini matatizo haya yataendelea, kula nao sahani moja, watanzania tumezoea kuwa wavivu wa kufuatilia mambo mpaka mwisho wake!!!
ReplyDeleteNionavyo mimi hii yote ni sababu ya shida ya maji hapa mjini na ukosefu wa suluhisho la kudumu kuikabili hali hii ikichangiwa na udhaifu wa wahusika wa masuala ya maji jijini.
ReplyDeleteSULUHISHO: kwakua maji ni uhai na kilio cha maji kwa wakazi wa jiji kinagusa wote yaani wa masaki mpaka uwanja wa fisi, basi ningeshauri tuwe na subira kwakua kunamtu ataturetea maji si mda mrefu kupitia bomba moja kuubwa maalum kwa wakazi wa Darisalaama. Na hapo ndio shida ya maji itabaki kua historia.
nenda EWURA , ndugu yangu, kikubwa tu, uwe na barua zako zote ulizowaandikia, na walizokujibu, na ueleze jinsi walivyokusumbua, hawa EWURA huwa hawana mchezo kama ulivyosema hapo, juu , kwani wao wanakuwa mahakama, na wanaendesha kesi vizuri na haraka sana, ili mradi uwe tu na vielelezo vya kutosha, unawashinda na wanakurudishia maji na hata faidia wanaweza kukulipa.
ReplyDeleteEWURA ofisizao zipo mataa wa samora, jengo la jmall ghorofa ya sita, idara ya malalmiko
mdau
ReplyDeleteOUTDATED, OVERCAPACITATED, RAG TAG, MONEY GRABBING, OLD TIMBER ORGANIZATION.
Jambo ambalo NAWASIFIA ni wepesi, ufanisi, ukarimu, ukunjufu, uharaka wa KUKUPA ILE MICKEY MOUSE FOMU INAYOGHARIMU SHILINGI 20,000 ambayo unaambatanisha na eti picha yako.
Baada ya hapo? Kama unaumwa hedex meza kichwa.
kitu ambacho siwaelewi hawa jamaa ni kwamba hata mteja akienda na pesa pungufu wanazikataa eti mpaka meneja akubali na asipokuwepo ndo basi mteja anaondoka na pesa yake khaaa! Hawa wanafanyaje biashara??
ReplyDeleteAcheni ulalamishi ninyi sie huku bonyokwa hatujui hata hiyo dawasko, na maisha yanaendelea kama kawaida, kuweni wabunifu. Heri yenu maji yanatoka au mnafikiri sie hatuna haki sawa ya kuwepo hapa Dar.
ReplyDelete