Kutoka Kushoto - Mh. Balozi Tuvako Manongi, Dr. Aleck Che-Mponda, Mh. Balozi Ramadhani M. Mwinyi
Kutoka Kushoto - Mh. Noel Kaganda, Mh. Balozi Tuvako Manongi, Dr. Aleck Che-Mponda, Mh. Balozi Ramadhani M. Mwinyi, na shemeji yangu Stanley Harris.
Dr. Aleck Che-Mponda alikutana na Balozi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mh. Tuvako N. Manongi na Naibu Mwakilishi wa kudumu, Mh. Ramadhani M. Mwinyi, jana, Alhamisi, January 24, 2013 mjini New York.
Dr. Che-Mponda alifanya utafiti muhimu kuhusu mgogoro katika ya Malawi na Tanzania kuhusu Ziwa Nyasa mwaka 1971 kwa ajili ya Ph.D yake kutoka Chuo Kikuu cha Howard (Howard University). Dissertation inaitwa, ''The Malawi-Tanzania Border and Territorial Disputes, 1968: A case study of Boundary and Territorial Imperatives in the new Africa". Dr. Che-Mponda alimkabidhi Mh. Balozi Manongi, nakala la andiko (dissertation) lake. Kwa wasiofahamu, Dr. Che-Mponda ni baba yangu mzazi.
Utafiti aliyofanya zaidi ya miaka 40 uliyopita umekuwa muhimu sana sasa kutokana na Rais wa Malawi, Mh. Joyce Banda kuruhusu makampuni kuchimba mafuta (oil exploration) katika Ziwa Nyasa, akidai kuwa Ziwa yote ni mali/ardhi ya Malawi.
Well done Dr. Aleck Che-Mponda and your daughter Chemi Che-Mponda!
ReplyDeleteSijawahi kusoma Makala ktk blog nikasisimkwa na vinyweleo ktk ngozi yangu kwa ghadhabu kubwa dhidi ya Malawi na Raisi wao Mama Joyce Banda kama leo!
Kumbe ukweli upo namna hii tunapata tabu bureee, kumbe Mkoloni wetu Mwingereza sisi Tanzania na Malawi alishatoa msimamo wa Mpaka tokea mwaka 1924 sasa huyu mama anataka kutueleza nini leo hii?
Kwanza kama ni hivyo Tanzania tunastahili kumfungulia Kesi huko huko ICC (Mahakama ya Dunia) kwa kuingilia Mpaka wa nchi yetu akaruhusu Makampuni ya Uingereza kutafiti Mafuta na Gesi ndani ya eneo letu.
Sioni sababu ya kuomba nipewe Bunduki, Magwanda na Ramani hiyo kama ghadhabu ilivyonishika kabla sijaisoma hii taarifa vizuri, NI WAZI BORA TWENDE MAHAKAMANI NA USHAHIDI WA DR. CHE MPONDA UKIWEPO IKIWEZEKANA NA YEYE AWEPO KATIKA MSAFARA WA WAWAKILISHI WA TANZANIA !
Mhe. Raisi Kikwete unamchelewesha huyu mama Joyce Banda ametuvamia katika sehemu ya nchi yetu!
ReplyDeleteNipi Bunduki na Sare za Jeshi niende mastari wa mbele kumpiga adui Malawi!
Nafirikiri hata kama Kesi tukishinda ni mihimu tukatuma Majeshi ama madege tukaipiga Malawi kwa adhabu dhidi ya uvamizi wao ndani ya eneo halali la nchi yetu!
ReplyDeleteSikujua kama Dr. Che Mponda ni baba ya Michuzi ( kidding, I think the author of this article did not put his/her name)
ReplyDeleteWewe Mama Joyce Banda Raisi wa Malawi, unautafuta Uraisi kwa njia mbaya huko kwenu!
ReplyDeleteUnafanya uvamizi kwenye nchi ingine, kwani huoni wanamama wenzio wanaofanya harakati za Uongozi na Uraisi nchini Tanzania wakipanda Treni?
Kwa nini usipande Ngalawa kwenye Ziwa Nyasa ili kuonyehsa wananchi wako kuwa upo kwa ajili yao?
Badala yake unafanya uvamizi kwenye Ziwa kwa kuruhusu Watafiti wa mafuta na gesi wa Makampuni ya Uingereza?
Heeeee Mama Joyce Banda Raisi wa Malawi ame BREACH INTERNATIONAL LAWS ON NATIONAL BOUNDARIES !!!
ReplyDeleteNI HIVYO ALIVYORUHUSU UTAFITI WA MAFUTA KWA MAKAMPUNI YA UINGEREZA, NA KUINGIA HADI ENEO LA MAJI YA TANZANIA KTK ZIWA NYASA WAKATI ZIWA LIPO KWENYE DISPUTE!
KWA NINI ASIPELEKWE KUSHITAKIWA UMOJA WA MATAIFA KWA UVAMIZI?
Tafadhali,
ReplyDeleteKatika Kesi hiyo ya Tanzania na Malawi kuhusu mgogoro wa Ziwa Nyasa tunaomba Mhe.Aleck Che-Mponda na Mhe.Balozi Tuvako Manongi wawepo kama Wawakilishi ama Wajumbe upande wa Tanzania!!!
kwa hiyo.....
ReplyDeleteDula A Dula