Wanachama wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini  katika mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.
 Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
 Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
 Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Pichani kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
 Pichani ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo. 
 Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.Picha zaidi bofya Jiachie Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mungu wa Yanga huyu! iko siku atawaliza tu kama sio likle jengo lenu la mtaa wa Twiga sijui! Chezea mwindi wewe? Ah!

    ReplyDelete
  2. Ni kituko cha aina yake na aibu yam waka kwa Klabu kubwa za Mpira kufanyia Mikutano yao kwenye Bwalo la Maafisa wa Usalama na Polisi!

    Ni kuwa Mashabiki wamekosa busara kwa fujo na vurugu!

    Hivi hamuoni ni fedheha sana hivyo, badala yake angalieni si mngafaidi kama mngefanyia kwenye Hoteli za Kitalii?

    ReplyDelete
  3. Police Officer's Mess:

    Nilitaka nione kama mtu Shabiki angefanya fyokoooo, weee!

    Wana wa Makunjas Askari wa Miamvuli wangeshuka kama mwewe Ukumbini!!!

    ReplyDelete
  4. Hehehe!,

    Masela wa Yanga SC, vipi 'uvutaji' uliwezekana hapo 'Ndani ya Ngome' ?

    Je mliweza kujaribu kuwasha Viberiti hapo ndani ama pembeni ama vyooni?

    Subutuuuu, hapo ilibidi ,mvute Sportsman,SM na mtu akizidi anavuta sigara Nyota ama sigara Safari za Kiwandani !!!

    ***hapo Sigara Nyota na Sigara Safari ndio zilikuwa Ganja za muda***

    Huyo ambaye angefanya angejaribu hivyo hapo Ukumbi wa Polisi nadhani angekuwa amekusudia yeye mwenyewe kuwekwa ndani!

    ReplyDelete
  5. Kweli Polisi inaweza!

    Fujo zote Yanga SC mkiwa Klabuni kwenu, lakini ndani ya Ukuta wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay,,mlisalimu amri kimyaaaaa!

    ReplyDelete
  6. Ehhh Mashabiki wa Yanga!

    Inafahamika ya kuwa mnatokea maeneo ya Jangwani, na mkiwa kule kwenu mnakuwa Matajiri sana na mkiwa huru!!

    Je, mlipata ujasiri, mlijaribu au mliweza kumuenzi Hayati Bob Marley hapo ndani ya Ukumbi wa Maafisa wa Polisi Oysterbay?

    ReplyDelete
  7. Huyo Shabiki wa Yanga ambaye angejaribu kuwasha kiberiti na 'kuvuta' ohhh!

    Wana Usalama kila kona ndani ya Ukumbi wa Maafisa wa Polisi hadi vichochoro vya kwenda Msalani!

    Ile kiberiti kikiwashwa kwaaa!, WAKULU wanachukua tahadhari wanasikilizia moshi unaotoka kama wachukue hatua gani kulingana nao?

    Ikionekana moshi sio Mhusika anakula kofi la mgongoni puuuu huku moshi ukiwa mdomoni na kooni anapaliwa!, anameza kipisi kilicho mdomoni (ili kuficha ushahidi, lakini moshi uliozagaa bado unamponza) na wakati mwingine anaachia upepo (anaj...mba) fuuuuu !!!

    Mkutano wa Yanga unaendelea Mhalifu anawahishwa Kituoni!

    ReplyDelete
  8. POLISI NI DUME!

    Enheee Mashabiki wa Yanga SC ama kweli Kikao chenu Jumapili kilikuwa kinafanyika huko KIUMENI!

    Mmeona katika picha ile Mkukatano umemalizika kila mmoja kimya mikono nyuma kwa amani anawahi mlangoni anaondoka!

    'Kiumeni' Police Offer's Mess Oyesterbay mchezo?

    ReplyDelete
  9. Ndani ya Bwalo la Maafisa wa Polisi!

    Ni uamauzi wa Busara sana kwa waliyeasisi utaratibu wa Klabu korofi za Mpira kama Simba SC na Yanga SC kufanyia mikusanyiko yao hapo Bwaloni 'Ngome Kongwe' mjengoni.

    Hapo Mashabiki mngeleta mchezo mngeona Maafande Maafisa waliokuwa wanapata moja mbili zao baridi huku ninyi mkiwa Kikaoni wangeshuka kutoka kwenye Stuli zao kwenye Kaunta wakavua Mikanda yao viunoni moto ukawaka Ukumbini na baada ya muda mfupi watu wamefungwa mashati wanakokotwa kwenda Kituoni!!!

    Chezea Polisi?

    ReplyDelete
  10. Sheikh wa Yanga picha ya 6 kutoka juu:

    Assalam Alaykum,
    Inasemekana siku ya mahesabu kwa Mwenyezi Pepo ya Daraja la juu itakuwa na Rangi ya Kijani!

    Je, wana Simba SC mnasemaje?, mpo tayari kwa kuvaa Kanzu za Kijani?, je mtakuwa na chenu hapo?

    Hivyo Sheikh wa Yanga ameona afanye maandalizi na mapema kwa kuiwahi tiketi hiyo kwa kushona kanzu ya rangi ya Kijani!

    ReplyDelete
  11. Polisi Jogoo la MBEGU!

    Yanga mmetoka mikono nyuma kimya kabisa licha ya usela na fujo zenu mkiwa Klabuni kwenu.

    Penye wengi na wakorofi unaweza kukuta pana mtu amekuja na msokoto wake kibindoni lakini kulingana na msimamo mkali ulio ngunguri wa wana usalama hapo Bwalo la Maafisa O'Bay, Msela wa Yanga anajikuta anakosa nafasi ya sio kupuliza, ile kuuchomoa kutoka kibindoni anajikuta anarudi nao Jangwani!!!

    Si mchezo, hata kuwasha sigara mlikuwa mnaogopa!, mnajistukia msije kufikiriwa mnavuta bangi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...