SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) litaanza tena safari zake kati ya Dar es Salaam na Mtwara, kuanzia  Ijumaa tarehe 8 February 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam  jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro alisema kuwa shirika lake litatumia ndege aina ya Dash 8-300 ambayo inauwezo wa kubeba abiria 50.

“Sasa tumejipanga upya kurejesha safari zetu kati ya  Dar es Salaam na Mtwara ambazo zinatarajiwa kuanza Ijumaa, tarehe 8 mwezi huu wa Februari 2013. Urejeshwaji wa safari za kwenda Mtwara, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuongeza safari za kuenda mikoa mbali mbali ambayo tulikuwa hatuendi kwa sasa,” alisema.

Kapteni Lazaro alibainisha kuwa ratiba inaonyesha kuwa ATCL itaruka kwenda Mtwara katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili na kuongeza kuwa marekebisho ya ratiba yataendelea kufanywa kulingana na mahitaji ya wateja.

Alisema kuwa shirika lake litatoza nauli kuanzia shilingi 199,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi.  “Abiria katika njia hii watahitajika kulipia kuanzia shilingi laki moja na tisini na tisa elfu kwa tiketi ya kwenda na kurudi. Abiria wanaweza kupiga simu namba 0782737730 ili wapate nafasi za usafiri. Vile vile abiria anaweza kupiga simu kwa mawakala walio karibu yao,” alisema. 

Urejeshwaji wa safari za Mtwara unakuja mwezi mmoja baada ya shirika hilo kurejesha safari za Kigoma baada ya kumalizika kwa ukarabati wa uwanja wa Kigoma. 

“Napenda niwahakikishie abiria wetu  kuwa tutaendelea kutoa huduma bora kuliko zote kwa bei nafuu” alisema. Aidha, Kapteni Lazaro alisema kuwa shirika la ATCL lina mpango wa kuongeza ndege zaidi kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, na kubainisha kwamba wanategemea kuchukua ndege ambazo ni kubwa zaidi na za kisasa zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. TABORA????

    ReplyDelete

  2. KEPTENI HIYO AIRBUS ITOE HAPO FOR NOW.
    WEKA YA DASH 8 Q300.

    ReplyDelete
  3. Uchumi unakuwa kwa kasi ya 7.1% kwa mujibu wa World Bank report, huku huduma za muhimu kama Usafiri wa anga zikienda mwendo wa Ali jojo, kama tunavyoona British Airways inafunga virago mwezi ujao, huku Basi letu la Toyota DCM likiwa halijaimarika kutoa huduma.

    Je, tutaubeba vipi uchumi huu unaokua kwa kasi ya ajabu bila huduma za usafiri zinazoimarika?

    WASTANI WA KASI YA KUKUA KIUCHUMI DUNIANI NI 5% (Average annual GDP growth worldwide), huku sisi Tanznaia tukiwa na kasi ya kiasi cha 7.1% zaidi ya wastani wa dunia!!!

    Ni swali la kujiuliza, hao Investors kwenye Sekta za Gesi, Mafuta, Madini, Fedha na Mawasiliano wanahitaji vitu hivi muhimu ikiwemo usafiri wa kuaminika, wenye ushindani na wenye bei nafuu.

    HAPA NDIO INAPOFIKIA PALE UNAISHI NYUMBA YA KUPANGA KTK CHUMBA KIMOJA, HUKU WANAO WENYE JINSIA TOFAUTI WAKIKUA KWA HARAKA NA KUHITAJI UWE NA VYUMBA VYA ZIADA KUWALAZA!

    ReplyDelete
  4. mdau wa 3 juu anony Thu Feb 07, 09:25:00 am 2013

    ...(Air Toyota DCM) /ATCL ndio kwanza basi lipo gereji huko miferejini, dereva amewaachia mafundi gari na funguo yeye amekwenda kunywa Gongo wakimaliza wata lijaribu halafu watampigia simu aje!

    ReplyDelete
  5. hahahahaha!!!

    Mdau wa nne mara zote Magereji yanakaa sehemu ambazo karibu yake kuna mpango mzima yaani mabanda ya Gongo!

    Mafundi na vijana wao wa spana wanachepuka mara kwa mara wakienda piga glasi zao na 'pepsi zao', maana kazi na dawa.

    yeye Dereva wa Toyota DCM hatakuwa na kuhitaji kupigiwa simu, yeye akisikia resi zinapigwa za majaribio anamalizia glasi zake kwa 'kugudua' anarudi gereji anajua mambo waa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...