Baba Mtakatifu Benedikti XVI  tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku. 

Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.

Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot.com.

Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)
                                                    Umati Mkubwa wa Waumini
                 Moja la jukwaa kubwa la wapiga picha wa kimataifa
     Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome alikuwepo kuiwakilisha Tanzania.
                Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma walikuwepo pia.
                       Baba Mtakatifu akiingia kwenye St. Peter's Square
                 Picha ya Baba Mtakatifu alipotupitia Karibu huku akitubariki
Bendera ya Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mkatoloki Tanzania nashukuru kwa uwakilishi huu. Kwa sababu yeyote ile; Papa Benedikti amefanya jambo la kishujaa ktk kujitadhmini na kuachia madaraka. Hongera Sana

    ReplyDelete
  2. Mimi Mkatoloki wa Tanzania nashukuru kwa uwakilishi huu. Kwa sababu yeyote ile; Papa Benedikti amefanya jambo la kishujaa ktk kujitadhmini na kuachia madaraka. Hongera Sana

    ReplyDelete
  3. Mfano nikiuliza sasa hapo bendera ya nini itakuwa ni kosa?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa 3 juu NI KUWA BENDERA HAPO INAWAKILISHA NCHI YA TANZANIA PIA KUNA BALOZI (PADRE KUTOKA TANZANIA HAPO VATICAN) NA WAO VATICAN WANAE BALOZI HAPA TANZANIA!!!

    WAKATI TANZANIA INA WATU WA DINI NA MADHEHEBU MENGI TU, PIA HUKU WENGINE HATA DINI WAKIWA HAWANA KABISA!

    Haki haijatendeka kwa hili!

    ReplyDelete
  5. Mwanawane Mdau wa tatu Hiyo Bendera ya Tanzania pana Balozi(ambaye ni Padri au Askofu/Mtanzania) anaiwakilisha Tanzania huko Vatican, na pia pana Balozi(Padri au Askofu/Mzungu) wa Vatican anaiwakilisha hapa Tanzania!!!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa tatu 3 juu Suala la uwepo wa Bendera ya Tanzania hapo lina siri kubwa sana.

    Mambo kama haya yanatakiwa yajadiliwe kwenye Katiba mpya!

    ReplyDelete
  7. Bendera ya Tanzania kuwepo VATICAN hiyo ni sawa!!!

    Lakini Tanzania kuingia Uanachama wa OIC hiyo hapana?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...