Baba Mtakatifu Benedikti XVI tarehe 27 Februari amekutana na waumini kwa mara ya mwisho kabla ya kung'atuka kwenye nafasi yake ya kuliongoza kanisa katoliki hapo kesho kwenye mida ya saa mbili za usiku.
Umati mkubwa wa watu ulijumuika nje ya kanisa la Mtakatifu Petro kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kuliongoza kanisa katoliki kwa kipindi cha miaka 8 tokea kuchaguliwa kwake.Itakumbukwa kuwa Baba Mtakatifu Benedikti XVI alichaguliwa kuliongoza kanisa katoliki baada ya kifo cha Baba Mtakatifu John Paul II. Mwenyezi mungu amuongoze Baba mtakatifu kwenye maisha yake yote nje ya uongozi wa Kanisa katoliki.
Jumuiya ya Watanzania Roma ikiongozwa na Katibu wake ilikuwepo kuiwakilisha Tanzania kwenye siku hii ya Kihistoria duniani. kwa picha zaidi mnaweza kutembelea hapa www.watanzania-roma.blogspot. com.
Picha zote zimeletwa kwenu na Andrew Chole Mhella (Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma)
Bendera ya Tanzania
Mkatoloki Tanzania nashukuru kwa uwakilishi huu. Kwa sababu yeyote ile; Papa Benedikti amefanya jambo la kishujaa ktk kujitadhmini na kuachia madaraka. Hongera Sana
ReplyDeleteMimi Mkatoloki wa Tanzania nashukuru kwa uwakilishi huu. Kwa sababu yeyote ile; Papa Benedikti amefanya jambo la kishujaa ktk kujitadhmini na kuachia madaraka. Hongera Sana
ReplyDeleteMfano nikiuliza sasa hapo bendera ya nini itakuwa ni kosa?
ReplyDeleteMdau wa 3 juu NI KUWA BENDERA HAPO INAWAKILISHA NCHI YA TANZANIA PIA KUNA BALOZI (PADRE KUTOKA TANZANIA HAPO VATICAN) NA WAO VATICAN WANAE BALOZI HAPA TANZANIA!!!
ReplyDeleteWAKATI TANZANIA INA WATU WA DINI NA MADHEHEBU MENGI TU, PIA HUKU WENGINE HATA DINI WAKIWA HAWANA KABISA!
Haki haijatendeka kwa hili!
Mwanawane Mdau wa tatu Hiyo Bendera ya Tanzania pana Balozi(ambaye ni Padri au Askofu/Mtanzania) anaiwakilisha Tanzania huko Vatican, na pia pana Balozi(Padri au Askofu/Mzungu) wa Vatican anaiwakilisha hapa Tanzania!!!
ReplyDeleteMdau wa tatu 3 juu Suala la uwepo wa Bendera ya Tanzania hapo lina siri kubwa sana.
ReplyDeleteMambo kama haya yanatakiwa yajadiliwe kwenye Katiba mpya!
Bendera ya Tanzania kuwepo VATICAN hiyo ni sawa!!!
ReplyDeleteLakini Tanzania kuingia Uanachama wa OIC hiyo hapana?