Mkurugenzi Mtendaji wa Kampauni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche (wa tatu kushoto) akikabidhi funguo kama ishara ya kukabidhi basi la Taifa Stars kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Leodgar Tenga (wan ne kushoto) wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhii basi hilo makao makuu ya TBL Jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kaviske, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Kushilla Thomas, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen, Mchezaji wa Taifa Stars aliyewawakilisha wenzake, Erasto Nyoni, Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Ofisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo Tanzania, Chalukulu John na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni.
Kocha wa Timu ya Taifa Kim Poulsen akishuka kutoka kwenye basi jipya la Taifa Stars lililolabidhiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Washangiliaji mbalimbali wa Taifa Stars wakati Kilimanjaro Premium Lager ilipokabidhi basi jipya kwa Taifa Starsaifa katika makao makuu ya TBL Ilala leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nilifikiri wangewapatia wanafunzi wanaonyanyaswa na daladala!

    ReplyDelete
  2. Basi ndio hilo TFF mmepewa!

    Lakini Uchaguzi wa TFF kwa Raisi wa Michezo na Uongozi wa Michezo unakuwa kama Uchaguzi wa Kisiasa vile?

    ReplyDelete
  3. Mambo kama haya ya Udhamini wa Mabasi kwa TFF ndiyo yanachangia kila mtu kutaka Uongozi TFF!

    Utaratibu huu ndio unawadumaza Viongozi wa Shirikisho wasiwe na uwezo wa kufikiri na kuwa wabunifu.

    Kwa nini Hawa wadhamini wasitatute njia ingine ya kuendeleza Michezo, na wakawaacha TFF wanunue mabasi kwa hela ya kudunduliza wanayopata kwa magawio ya michezo inayopigwa ktk Ligi?

    ReplyDelete
  4. Takrima ya Kiaina yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...