TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA VISIWANI ZANZIBAR,INATUHABARISHA KUWA PADRI EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA KATOLIKI HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFARIKI PAPO HAPO ASUBUHI HII WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.

SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRI HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA MPAKA SASA. 

MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA TUKIO HILO WALIKUWA NI WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA VESPA WAKATI PADRI HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI NA KANISA HILO.

 GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA TUKIO HILO NA TAARIFA ZAIDI ZITAWAJIA KILA ZITAPOPATIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Nasikitika sana kwa matukio haya nchini kwetu!!

    ReplyDelete
  2. So sad jamani rest in peace padre

    ReplyDelete
  3. Tumefika pabaya. Nani aliyetufikisha hapa? Tutatokaje sasa? Nchi inaelekea pabaya. Poleni wale wote mlioguswa na msiba huu.

    ReplyDelete
  4. waache mfumo kristo ili haya yasiendelee kutokea, vinginevyo huu ndo mwanzo wa ukombozi wa waislamu...siku zote nimekuwa niacha komenti zangu humu kuwa lazima kieleweke na hakuna kulala.
    mwachieni ponda na waislam wote mnaowashikilia bila sababu...wauaji wanapewa dhamana watumishi wa Allah wanabambikiwa kesi na kunyimwa dhamana. hatutaki tena....

    sina uhakika kama mauaji haya yamefanywa kwa mtazamo wa kidini lakn hilo pia lawezekana sana tu

    ReplyDelete
  5. Tanzania eehhe nchi yangu eeehh,tunaelekea wapi jamani,kwanini tunauwana kikatili kama hivi,cha kushangaza matukio mengi ya ajabu ajabu yanajitokeza zanzibar ambapo tulikuwa tunakuita kisiwa cha amani iko wapi ile amani.mungu amlaze pema padri Mushi.Amen.

    ReplyDelete
  6. Iyo amani viongozi wanayozungumzia ni hipi?

    ReplyDelete
  7. Haya ni matunda yaliyopandwa kwa muda mrefu now boko haramu tayari in TZ. Bwana Mungu uliye katika kiti chako cha enzi pokea roho ya mtumishi wako

    ReplyDelete
  8. His face is very peaceful he is in heaven

    ReplyDelete
  9. Rest in Peace Father. Mungu wetu atupe busara kuhandle yanayotokea kwetu wakristo wkt huu

    ReplyDelete
  10. hii sasa inakuwa zali, juzijuzi padri mwigine alipigwa risasi akanusurika huko zenji, wakasema vibaka walikuwa wanataka kumpora sadaka! huyu je?

    ReplyDelete
  11. Jamani hebu tuambieni huko Tanzania siku hizi kunafananaje, maana mpaka naogopa kurudi huko Tanzania nahofia maisha yangu?
    Kila kona wanapigana na kuuana?

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha sana kwa nchi iliyojaa amani kama hii kutokea matukio ya kikatili,wahalifu watafutwe sheria ifate mkondo wake!

    ReplyDelete
  13. This marks the beging of the end of peace in Tanzania, RIP Father Mushi, this was simply summary execution, most likely due to his religion.

    ReplyDelete
  14. Waacheni wazanzibari waishi maisha wanayoyataka kuishi.

    ReplyDelete
  15. Lord have mercy!

    ReplyDelete
  16. Michuzi naomba usibanie comment yangu hii roho inaniuma sana.Sitaki kuhumu lakini hii inaweza kuwa mambo ya Uislamu na Ukiristu.Kama ni mambo ya Uislamu na Ukiristu,Mimi lawama zote nazimwaga kwa Rais Kikwete na serikali yake yote kwa kuachia huu USHENZI uendelee kushika kasi kila kukicha.Watanzania hatukuwa na huu USHENZI wakati wa kipindi cha Awamu tatu za mwanzo.Na hii ni changamoto kubwa kwa Rais ajaye.Nawapo pole familia ya Padri Mushi na kanisa Katoliki kwa ujumla

    Mungu ibariki Tanzania

    David V

    ReplyDelete
  17. RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA
    NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE.
    APUMZIKE KWA AMANI – AMINA.watendaji wa uonevu huo sio kutaka ubaya ila kutaka nchi iwe na ugomvi,inasikitisha sana matukio ya kidini yanayotoea kila kukicha kisa watu wachache wenye sababu zao binafsi.

    ReplyDelete
  18. kama vipi, wapeni Zanzibar yao. wasituharibie amani kwa kuua wabara wetu! Sasa ni mambo gani haya?

    ReplyDelete
  19. Mungu ibariki Tanzania we are heading the wrong direction..!!

    ReplyDelete
  20. God please! This is it. What happened to Amani, Upendo name Umoja nchini Tanzania?
    This needs to stop immediately. Mtumishi wa Mungu huyu jamani ana kosa gani? RAISI KIKWETE WHERE ARE YOU?
    May the almighty God rest father E. Mushi`s soul in eternal peace.Gone too soon father.

    ReplyDelete
  21. MAMBO YANAANZA HIVI WMISHOWE TUTAKUWA KAMA RWANDA WATUSI NA WAHUSI.REST IN PEACE PASTOR.MDAU LEICESTER.

    ReplyDelete
  22. Mbona tafakari imetawala hapa? Kwani kuna fact kwamba ameuawa kwa sababu ya udini? Na wewe Muislamu mwenzetu (comment namba 4) uwe unatumia hikma kidogo. Dini haikufundishi kuua watu ovyo. Acheni mambo ya kuiga hayo. Sasa mtu ameshakufa, faida iko wapi?

    ReplyDelete
  23. Jamani, Tanzania si ile Tanzania ya enzi zile. Hii chuki ya kidini imezidi. Si uTanzania. Tunasahau maana ya 'NDUGU'!!!

    Rest is Eternal Peace Father Mushi.

    ReplyDelete
  24. jamani tusisahau ule usemi alotuachia bwana yesu usemao, anaekuibia koti mpe na shati lake, vile vile akupigae kofi upande huu mgeuzie na mwengine. HAYA NI MAFUNZO YANAYOTUFUNZA KUWA NA SUBIRA NA UVUMILIVI NA KUMZARAU SHETANI ANAETAKA KULETA VITA YA KIDINI KWETU WATANZANIA

    ReplyDelete
  25. Sipendi kuamini kwamba waislam wenye hekima na wasomi wanachochea hayo! Nawaomba viongozi na waislam wenye ubinadamu kuangalia haya.

    ReplyDelete
  26. (anony 4) pole sana!!
    mungu akupeleke jehanam sasa!! "mfumo kristo" ni nini katika zanibar ambayo 95% ya watu ni waisilam?? rais, makamu, mawaziri wote, makatibu wakuu wote, mkuu wa polisi, wakuu wa taasisi zote ni waisilamu, wewe tu ndio huna kazi, elimu, hela, wala meendeleo yeyote kwa kuwa hujasoma!! hata huku bara; rais, makamu, mawaziri65%, wakuu wa taasisi zote muhimu, IGP, makatibu wakuu 70% ni waislamu!!
    ungekuwa na akili kidogo tu ungejua Bakhressa, Manji, Mohamed enterprises, Zakaria, Suleiman-Jee, sio wakristo na wanafanya mambo makubwa!! wewe tu ndio huna akili!! ukombozi wako ni sasa ni kumkubali yesu tu, maana ndiye mwenye uwezo wa ku-deal na watu kama wewe!!
    "hakuna kulala" kuna maana gani wakati unakoroma??
    Ponda ni mhalifu kama ulivyo wewe!!
    siku ya siku hata wewe utaondoka!
    tumia akili yako japo ndogo.

    ReplyDelete
  27. Inaelekea kuna wachache wanaotoka kuturudisha miaka ya wakati wa ujima, lakini si rahisi kwa tanzania ya leo.

    Mbona huu upuuzi hautokei nchi za mashariki ya kati ambako kuna misikiti na makanisa na dini ya nchi ni waisilamu? Mbona Seyyid Said aliruhusu makanisa?

    Watu wachache hamuwezi kutishia amani kwa kupiga bastola hovyo - wala si washika dini wa kweli motoni kunawangoja!

    ReplyDelete
  28. Tatizo kubwa la wtz kwa sasa ni udini na hii itatugharimu sana!

    Ni tabu sana kumkuta mtu ambae yuko'objective' ktk kuzungumzia mambo ya dini!

    wapo washaoanza chokochoko za kuchinja kwa kushindwa kuwavumilia wenzao,

    Naamini kesho na wenzao watadai haki ya kupumzika Ijumaa na mwaka mpya wa kiislamu.

    Wengine humu wanashauri nchi hii igawiwe eti tu kwa sababu za dini nadhani hiyo sio akili!

    Lakini nadhani tatizo kubwa la Watanania ni ile hali ya kudhani kwamba Waislamu wote wa TZA wanatoka Z'bar wakati kumbe Bara ina Waislamu kwa mamilioni!

    Jamani tusihesabu watu kwa kuangalia waofisini mwetu, Wtza wengine hawakupata fursa hiyo!...nendeni mtaani!

    Kwa mfano ikiwa MKWAWA, FUNDIKIRA, BUSHIRI nk.walikua waislamu inakuwaje tufikirie waislamu bara wamekuja baada ya muungano?

    ReplyDelete
  29. Mimi naona bora Mapadri wetu wasiende Zanzibar. Maana huku kuuana kunakoendelea si dalili nzuri....Hapa kuna mkono mzito...Tanzania sasa imekuwa na hurka ya namna hii hata vizazi vinavyochipuka hali ni hii. Tuache mbali na mauaji, hata mauaji ni ufisadi wa aina yake...Nenda pale UDSM UCC. Wachapa kazi wazuri wameonewa , wamenyanyaswa na hata mipango ya kuwaua inatumika wakiona waliyemlenga anakuwa mbishi wa kuachia ngazi

    ReplyDelete
  30. Waona wengine na fikra zao mbovu! Wakristu ndio waliyomshikilia Ponda? au Serikali na Mihimili yake hasa wa mahakama ni wa Kikristu? Hii ya mwachieni Ponda imetoka wapi. Napenda kuamini aliyeandika hapo juu ni mmoja wa washiriki wa mikakati ya kuuwa Wakristu. Kupitia cyber intelligence serikali imtafute huyu atueleze bayana. Azungumzaye yana ashiria ukweli alio nao

    ReplyDelete
  31. Ngoja nikumbushe methari kidogo,usipoziba ufa -utajenga ukuta.Haya mambo yameanza muda mrefu tu na yanachekewa tu,yameanza na mihadhara ya kuchambua dini,mfano mwembe yanga,magomeni na sehemu nyingi tu.Watu walianza kwa kuendesha mahubiri ya kuchambu dini nyingine kwa kutumia masipika na hakuna aliyekemea mambo kama haya.
    Tangu nyakati kama hizi chuki ilianza kuumbika miongoni mwa wakiristo na waislam maana hakuna mtu anayekubari dini yake kusemwa vibaya.
    kule zanzibar makanisa yamechomwa,padri yule kapigwa risasi,na leo mwingine kauwawa kabisa.
    Kule mwanza watu wameendesha mabishano nani achinje nani asichinje,mpaka maisha ya watu yakapotea.
    kumekuwepo na hali ya kutishia kila ijumaa,watu wanafunga maduka ,mji unakimbiwa na shughuri za uzalishaji zina simama kabisa.

    Mbagala wamechoma makanisa na kuteketeza mali za watu ,na huu ni mwanzo tu.

    Hebu tuangalie sasa nani alaumiwe? kwa uelewa wangu chombo cha usalama wa taifa kipo na kina mtandao mpana sana ,sidhani kama kuna jambo laweza kutokea wasilijue, je walikuwa wapi mpaka ufa unabomoa nyumba sasa!!!! jeshi la polisi lipo na lina wapelelezi wengi tu, ikulu ipo na kila taarifa najua wanapelekewa ,hapa nina shaka na maamuzi ya mkuu wa nchi na vipaumbele vyake.
    Nimesikiliza vyombo vya habari kuwa kuna watu toka nje wanakuja kutusaidia kutafuta chanzo cha tatizo hili,hii ni aibu sana kwa taifa letu,yaani tumeshindwa wenyewe kuwabaini ! tuna polisi wa upelelezi,tuna usalama wa taifa ,ulinzi shirikishi,hawa wote wameshindwa kazi mpaka tukodi watu toka nje? kama nchi yetu imeshiriki kwenye operesheni kubwa za kimataifa tena kwa ufanisi mkubwa ,iweje jambo hili litushinde!!!!!
    Nimemkumbuka sana mzee Nyerere,nilitamani arudi wiki moja tu kisha aondoke tena! hatahivyo mzee mkapa na mzee mwinyi nawaombeni sana wazee wangu msaidieni huyu bwana ili ajue cha kufanya naina kazidiwa,anamambo mengi na misiba ni mingi sana hataimaliza.Nawaombeni wasaidizi wa raisi mwakilisheni kwenye mambo kama haya ya misiba ili apate muda wa kutulia ofisini apambanue mambo kwa upana,nampenda ni mtu wa watu.Hata biblia kitabu cha kutoka,Ethiro alipomtembelea Musa (mkwewe) alimkuta akikaa tangu asubuhi mpaka jioni akiamua kesi za watu,akamshauri atafute watu wa kumsaidia ,hivyo basi nani alaumiwe kila mtu apime kulingana na maelezo yangu.

    ReplyDelete
  32. Tumechoshwa nauaji ya viongozi wetu wa kanisa.Wakristo wote sasa tuungangane kwa kufunga kwa maombi mazito ili Mungu wetu awe jibu kwa hao wauwaji. Amen

    ReplyDelete
  33. Kwanini tuhukumu mauaji haya ni ya kidini au kwakua ni Zenj ya 95% waislamu.

    Je ni Mapadre wangapi wameuwawa kwa njia tofauti na hakuhusishwi na dini.
    Tusubiri sheria iliyopo iamue.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...