Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) Ukonga kabla ya uzinduzi wa Supermarket ya kwanza katika Jeshi la Magereza nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Supermarket ya kwanza ya Jeshi la Magereza nchini.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Military Shop, Afzal Meghji akimuonyesha bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya duka hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na maafisa magereza (hawapo pichani) kabla ya kufungua Supermarket kubwa ya kisasa ambayo itawawezesha maafisa hao, askari na familia zao kupata huduma ya kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, John Minja na kulia ni Mwekezaji Mkuu wa Kampuni ya Military Shops ambaye ndiye aliyewekeza katika Supermarket hiyo, Sadrunin Virji. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmauel Nchimbi akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja akipokea zawadi kutoka kwa mke wa Mwekezaji Mkuu wa Supermakert hiyo, Gulshan Virji (kulia).
 Baadhi ya maafisa na askari Magereza wakinunua bidhaa mbalimbali katika Supermakert hiyo baada ya kuzinduliwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa tatu kutoka kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (wa kwanza aliyekaa kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa mbalimbali wa magereza pamoja na wageni waalikwa.
 PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mbona hamsemi DUKA liko wapi jamani?

    ReplyDelete
  2. Asingeweza kuifungua Duka hili mzawa?

    ReplyDelete
  3. lipo ukongo ndani ya jeshi,huduma karibu na jeshi kwanza,wateja ni baadaye.

    ReplyDelete
  4. Enzi za Mwalim maduka ya jeshi, magereza na polisi ndio yalikuwa na bidhaa. Kama sio askari ulikuwa huli, hufui, hukogi na huvai!!

    ReplyDelete
  5. Ni kweli habari hainyeshi mahali duka lilipo lakini ukiwa makini ktk picha utaona liko Ukonga. Usiwe mvivu kusoma na kuona!!!

    ReplyDelete
  6. ukonga husomi habari yote ukaelewa

    ReplyDelete
  7. Angalia picha ya mwisho imeandikwa branch

    ReplyDelete
  8. Wadada wa magereza; tunajua hamna pesa ya ku-shop suppermarket. Japo mmoja kajitutumua kachukua maji kachupa ka 1/2 lita

    ReplyDelete
  9. Sie wengine tunasoma NUKTA NUNDU hivyo amechemsha kwa kuto kuandika duka liko wapi. Emmanuel Nchimbi tunamjua, kwannini Mumtaje lakini mshindwe kutuambia duka liko wapi?

    ReplyDelete
  10. We anony wa kwanza a ha ubaguzi. Nani amuse a muwekezaji siyo mzawa?

    ReplyDelete
  11. yaani jamani hata kauwekezaji kaduka nako magereza hamuwezi wenyewe??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...