Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiweka saini Itifaki ya Amani na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Uwekaji saini huo ulifanyika katika Hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Membe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzake wa nchi za EAC wakiwa wameshikilia Itifaki hiyo mara baada ya kusainiwa
Mhe. Membe akipitia Itifaki hiyo kabla ya kusainiwa huku Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akishuhudia.
Mhe. Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wake Bw. Haule. Mwingine katika picha ni Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Picha nyingine ya Mhe. Membe na Katibu Mkuu wake Bw. Haule na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi wa Uganda.
Mhe. Membe akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.
Picha zaidi za mahojiano kati ya Mhe. Membe na Waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Amani na Usalama?

    Safari ndefu tungali tunayo ktk eneo letu la Afrika ya Mashariki!

    Kama tunavyoshuhudia mauaji na uhalifu vinavyojiri nchini.

    -Mapigano baina ya watu kwa Misingi ya Dini huko Besere sere-Geita.

    -Uharamia wa Wanyama pori unaohisiwa kusukumwa na Makundi ya kuvuka Mipaka Afrika ya Mashariki.

    -Wizi wa Makontena ya Madini yakiwa njiani kwenda ng'ambo.

    -Mauaji ya Viongozi wa Dini Visiwani.

    -Kumwagiana tindikali n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...