Rais wa TFF, Leodegar Tenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya sakata la uchaguzi mkuu wa TFF,kwenye ukumbi wa mikutano uwanja wa taifa.
SAKATA la uchaguzi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limefika patamu baada ya rais
wa TFF, Leodegar Tenga kudai kuwa yupo
tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa
walioenguliwa kuomba upya marejeo (review)
ya rufaa zao.
Tenga ambae juzi alikuwa na kikao kizito na
kamati zake za uchaguzi kabla ya leo
asubuhi kuwa na kikao kingine Wizarani,alisema binafsi hana uwezo wa kutengua
maauzi ya kamati zake kwa kuwa ni huru
lakini yupo tayari kutoa muongozo kwa
atakayetaka ili aweze kufanikiwa kupata haki
yake.
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es
Salaam leo, Tenga alisema kuwa kwa mujibu
wa katiba yua TFF kamati ya rufaa ndiyo ya
mwisho katika maamuzi lakini mlalamikaji
anaweza kuomba marejeo ili kutafuta haki
yake.
"Jambo la kwanza mtu kama hajaridhika na
uamuzi anaweza kuomba review(Marejeo)
katika kamati ya rufaa, majibu yatakayopata
kama hajaridhishwa tena anaweza pia
kupeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka la
Dunia (fifa) na tatu ni kwenda CAS (mahakama
ya usuluhishi).
"Jambo hili linazungumza kinazi zaidi watu
hawaangalii katiba inasemaje, lugha za kejeli
zimekuwa zikitumika kiasi kwamba maamuzi
yaliyofanywa tunaonekana kana kwamba sisi
wote ni wapumbavu, watu wanaotaka kutusaidia
kukuza mpira wetu (wadhamani) hawawezi kuja
kama kuna migogoro.
"Nipo tayari kufanya kila njia kuhakikisha
tunatoa msaada kwa kila anayetaka kamati ya
rufaa itakaa kesho kupitia review (marejeo) ya
watu wawili ambao wameomba.
Tenga aliwataja walioomba marejeo ya rufaa
hizo kuwa ni Jamali Malinzi ambaye alienguliwa kwa
kigezo cha kukosa uzoefu wa miaka mitano
kwenye masuala ya soka ikiwa ni pamoja na
kupinga mabadiliko ya katiba ya TFF na Hamad
Yahaya ambaye alienguliwa kuwania nafasi ya
mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu.
"Sisi tupo tayari kutoa msaada kwa ambaye
hajaridhishwa na uamuzi wa kamati ya rufaa
kwa kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa
kufuata katika kutafuta haki zao wanatakiwa
kujenga nguvu ya hoja na si hoja ya
nguvu,".alisema Rais huyo.
Kauli ya Tenga imekuja ikiwa ni siku chache
baada ya kamati ya rufaa chini ya mwenyekiti
wake Idd Mtiginjola kumuengua kwenye
kinyang'anyiro cha urais katibu mkuu wa
zamani wa Yanga Jamali Malinzi ambaye pia
amepinga kuenguliwa kwake na tayari
ameshawasilisha ombi lake la kutaka marejeo
ya rufaa yake sambamba na mwenyekiti wa
Mtibwa Sugar Hamad Yahaya ambaye naye
alienguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho
ambacho alikuwa akiwania nafasi ya mwenyekiti
wa bodi ya Ligi Kuu.
Wakati huo huo,Tenga alipangua hoja ya Katibu
Mkuu wa zamani wa Fat sasa TFF Michael
Wambura ambaye alidai katiba imesiginwa kwa
TFF kuikiuka katika mchakato mzima wa
kuifanyia mabadiliko.
Mapema wiki hii Wambura alitoa siku tatu kwa
TFF kuhakikisha inaangalia upya suala la
kuenguliwa kwa Jamali Malinzi na hadi
Jumatatu kama rais Tenga angekuwa hajatoa
kauli yoyote angeenda kufungua kesi
mahakamani ili haki itendeke.
Alisema pia TFF ilikiuka katiba yao kwa
kufanya marekebisho kwa njia ya waraka na
pia kumdanganya msajili wa vyama vya michezo
kuwa mkutano mkuu ulikaa Desemba 15 kitu
ambacho si cha kweli huku kanuni za uchaguzi
zikianza kutumika Januari 7 wakati katiba
imepigwa muhuri wa msajili Januari 12 na
kuiita katiba hiyo ni batili na mchakato mzima
wa uchaguzi.
Akizungumzia suala hilo Tenga alisema "Kikao
sio lazima tukae sasa hivi dunia imebadilika
hata kwa njia ya mtandao watu mnafanya kikao
tulitoa waraka kwa kupiga kura wanachama 70
walisema ndio na 33 wakasema hapana.
"Kamati yetu ya utendaji ndio ilipokea majibu
ya waraka Desemba 15 na haraka ikaanza
kutumika, hatukudanganya na barua
tuliyopeleka Wizarani na taarifa za kikao
zilisema hivyo.
Kuhusu kupigwa stop kwa uchaguzi wa TFF
baada ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya
urais Richard Rukambura kwenda mahakamani
kwa kupinga kuenguliwa kwake Tenga alisema
"Mpaka sasa mimi sijaona samsa ya
mahakamani kwa hiyo siwezi kuzungumza lolote
kwa sasa."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...