Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu akiongelea juu
madhumuni ya ziara yake leo asubuhi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Pangani. Mhe. Jaji Kiongozi alitembelea ofisini hapo kabla ya kuelekea
Mahakama ya Wilaya ya Pangani.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Ltn, Chiku Gallawa akiongea na Ugeni wa Viongozi mbalimbali wa Mahakama ukiongozwa na Mhe. Jaji Kiongozi katika ziara yake mkoani Tanga. Mhe. Mkuu Mkoa pamoja na Mhe.Jaji Kiongozi wamesisitiza juu ya uimarishaji wa ushirikiano katika utendaji kazi.(picha na Mary Gwera,Mahakama ya Tanzania).
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani, Mhe. Frank Moshi akitoa mkono wa salamu kwa baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani Mara baada ya kuwasili Leo asubuhi Mahakamani hapo pamoja na msafara wa Mhe. Jaji Kiongozi, Mhe. Moshi ameteuliwa hivi karibuni kuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Pangani baada ya kustaafu kwa Mfawidhi wa Mahakama hiyo, nyuma ya Mhe. Moshi ni Mkurugenzi wa Mahakama za Mwanzo nchini, Mhe. Euphemia Mingi, Kushoto kwa Mhe. Mingi ni Naibu Mkurugenzi wa Mahakama za Wilaya hadi Rufani, Mhe. Eddie Fussi. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...