Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi - ZANZIBAR 

WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, amesema leo kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku. Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya makapaa.

Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea. Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.

 Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo. Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.

Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo. Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hawa ni watu wachache(kigenge cha wahuni) wanaofanya matendo kinyume na sheria kwa kuwachonganisha watu,inabidi wazibitiwe mapema kwasababu wataalibu amani yetu

    ReplyDelete
  2. Majibu mepesi katika suala kama hili hayana nafasi. Genge la wahuni? Hata kidogo...Wanajua nini wanatafuta. Wamejiandaa....Chui anayemchokoza mwanakondoo....Unatarajia nini? Hebu tuwe serious sasa. Serikali Amka....kuiomba jamii moja ikae kimya wakati inateketea hii ni dhulma tosha.Mnataka kilipuke msicho kitarajia? No! No.

    ReplyDelete
  3. Siyo kikundi cha wahuni hii ni planned.Mwanadamu hatashindana na Mungu hata siku moja kwa maana siku zake zimeandikwa kiganjani mwake.Kusudi la Mungu halitazuiwa na mwanadamu hata shetani hawezi.Ni sawa na kupiga ngumi kwenye ukuta wa moto.Walikuwepo wengi kama hawa lakini ni nani ajuae mahali walipo sasa?Bila shaka kama hawakuzitubia dhambi zao,mahali pao ni jehanamu ya moto.Watanzania tuache udini hautatusaidia hata kidogo.Mungu awabariki ndugu zangu.

    ReplyDelete
  4. Mlinzi gani huyo bomu kabisa. Anajificha na kusubiri nini kitokee, badala ya kupiga simu moja kwa moja police mara baada ya kuona watu 3 wakiwa maeneo ya kanisani saa tisa usiku.

    ReplyDelete
  5. Nyie wazanzibari msitubabaishe mnajua mnachokifanya huwezi kuwa matukio Kama haya yanafuatana eti hamjui. Mnafikiri ukristu ukiondoka nyie mtabaki? Wenyewe kwa mwenyewe hampatani. haya. MUNGU TUNAOMBA UWAUMBUIE MAADUI HAWA MBELE YA MACHO YETU AMIN.

    ReplyDelete
  6. Hivi ni vikundi vya wahun ambavyo vinahatarisha amani ya nchi kwa bendera ya udini mimi ni muislam ila napinga vikali vitendo vya kuchoma makanisa na kushambulia viongoz wa dini serikal chukua hatua mapema juu ya hawa watu najua hamshndw kuwakamta kama mkiwa seriuos na jambo hili na wananch wafichuen hao wahun kama mnawafahmu

    ReplyDelete
  7. Mwenzako akinyamaza na akavumilia haimaanishi ni nyonge na hana nguvu...ila imani yake haimruhusu kufanya mambo tofauti na mafundisho ya mungu. Serikali naomba muwakamate hao wahuni na wafadhili wao na muwaweke hadharani tuwajue

    ReplyDelete
  8. Haya matukio ni lazima yana chanzo na sababu zake. lazima tutafakari na kuzuiya kabla ya athari kubwa kutokea.

    Haki dini! ndoo ndoo.

    ReplyDelete
  9. Hakuna Dini ianyokubaliana na 'UHALIFU'!

    Hata iwe Dini ya kuabudu Moto ama mawe.


    Hawa watu lazima wapatikane kwa gharama yeyote ile!

    ReplyDelete
  10. Wazanzibar acheni ujinga!

    Eti nini Ukristo Zanzibar?

    Hivi hamkumbuki ya kuiwa Kanisa la kwanza Afrika ya Mashariki lilijengwa Zanzibar?

    Hamkumbuki ya kuwa Wamishionari walifikia Zanzibar ktk hii Afrika ya Mashariki?

    Dunia ina nchi kama IRAQ,MISRI,JORDAN,LEBANON,PALESTINE na JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN ambako hata Wakristo wapo!

    Sasa itakuwa Zanzibar?

    ReplyDelete
  11. Nduguzangu wazanzibari hakuna kitu kibaya kama kumwaga damu ya mtu hivyo mnajipaliia laana na dhiki kuu msiyoitegemea damu ya mtu haita kaa ipoteee bure; subirini majanga toka kwa Muumba.

    ReplyDelete
  12. Walinzi peke yake hawatoshi.

    Wekeni Kamera kwa siri ili ajulikane ni nani Mhalifu.

    Ya nini tabu?

    ReplyDelete
  13. Wazanzibari ndugu zetu!

    Swala zetu zenyewe za kuunga unga, hatujui kama Mwenyezi anazipokea au labda zina kubalika!

    HIVI KWELI TUNAWEZA KURIDHIKA NA KIWANGO CHA UUMINI TUNAOUFANYA KWA SWALA ZETU ZA KUUZA NA KUNUNUA KATI KATI YA SWALA?, HADI IFIKIE TUKAYAINGIA MAJANGA MAKUBWA KAMA YA KUUWA WENZETU?

    Sasa leo tunakuja kujitwisha mzigo wa mauaji, hivi tutakuwa wageni wa nani baadae mbele ya Mwenyezi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...